Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Mzee Kaa mbali kabisa Liverpool imeshatoka huko Sasa hivit

Tumia akili kichwani tunaangalia tunapoenda sio nyuma klopp kaferi aende wake wengine full stop
Sasa wewe unayejuwa tunapoenda hebu tuambie tunaenda wapi? Nimekwambia kabla ya Klop zaidi ya miaka 20 na zaidi tulifanya nini? hakuna lolote, Klop ndio pekee alileta muendelezo kwa miaka mingi na low budget watu kama Benitez walishinda mwaka mmoja to champions league lakini hakukuwa na muendelezo wa mafanikio.
 
Wenye team wenyewe pale Liverpool na washabiki wamelia kuhusu Klop wewe ndio unadhani akili za ushabiki wa Simba na Yanga ndio Liverpool.
 
Kashabikie rede mpira hujui Kaa mbali na mpira mzee mpira watu tunaangalia Sasa hivi unafanya nini usilete habari za kusema miaka 20 ilikuaje
 
Mzee Kaa mbali kabisa Liverpool imeshatoka huko Sasa hivit

Tumia akili kichwani tunaangalia tunapoenda sio nyuma klopp kaferi aende wake wengine full stop
Haya mzee wa kuangalia tunapoenda tuambie unamtaka nani? au umekariri tu
 
Wenye team wenyewe pale Liverpool na washabiki wamelia kuhusu Klop wewe ndio unadhani akili za ushabiki wa Simba na Yanga ndio Liverpool.
Wewe akili huna mpira hauna huruma ya kusema miaka 20 ilikuaje watu tunaangalia Sasa hivi unafanya nini kashabikie rede Naona mpira hujui
 
Kashabikie rede mpira hujui Kaa mbali na mpira mzee mpira watu tunaangalia Sasa hivi unafanya nini usilete habari za kusema miaka 20 ilikuaje
Sasa wewe unayetabiri ya mbele umekuwa mganga wa kienyeji? wewe umesema Klop hafai nimekwambia ulikuwa wapi wewe kabla ya Klop? nafasi zetu zilikuwa huko 6 tumejitahidi 5
 
Sasa wewe unayetabiri ya mbele umekuwa mganga wa kienyeji? wewe umesema Klop hafai nimekwambia ulikuwa wapi wewe kabla ya Klop? nafasi zetu zilikuwa huko 6 tumejitahidi 5
Nimeshakuambia kashabikie rede na dada zako
 
Wewe akili huna mpira hauna huruma ya kusema miaka 20 ilikuaje watu tunaangalia Sasa hivi unafanya nini kashabikie rede Naona mpira hujui
Sasa kafanya nini? tuko nafasi ya pili tofauti point moja sasa ulitaka iweje zaidi ya hapo? hebu tuambie ulitaka team iwe wapi.
 
Kocha Gani kujifanya mjuaji kumbe hamna kitu asepe tu akili yake imeshazeeka inahitaji kupumzika
 
Juzi hapa tulikuwa tunagawa dozi mfululizo na kuongoza ligi, tukawa tunalia Klopp kwanini Mungu ameruhusu kuondoka mwisho wa msimu.

Tumepoteza mechi chache leo tumejeuka tunasema Klopp hafai ni takataka aondoke haraka sana.

Kweli binadamu ni kiumbe cha ajabu sana hata ukicheza kwenye maji atasema unamtimulia vumbi
 
Labda wewe sio Mimi huyu kocha ni zero kabisa ameshatukosesha makombe mengi sana Kwa uzembe wake asepe Hana faida kama haleti makombe ya maana
 
Dah.!! Mpira una ukatili kweli. Nilikuwa busy kwa muda nimepata muda wa kuja huku ila ndio nakuja kinyoooooooonge.


Greetings to y’all.

Anyway sitii neno 2nd leg mwezi March mpaka sasa tunacheza kama kukamilisha ratiba tu.

Ynwa
 
LAWAMA.

Kwanza nizipeleke kwa Klopp kisha wachezaji.

Kuna namna namuona Klopp yupo na sisi physically ila mentally kuna mahali yupo. Hii inachangiwa na kuondoka kwake kabla ya kuondoka. Atleast January to February kulikuwa na uhai ila kwa sasa, sioni rythym kwenye team, wachezaji hawana focus na team kwa kadiri siku zinavyosonga mbele. Why? Wengi hawajui hatima yao itakuwaje, Klopp akiondoka.

Tactically Klopp ameshindwa kutengeneza good setups za kuzuia. Kumbuka ishu ya ulinzi inaanza ma system nzuri kisha individuality especially kwenye soka la kisasa. 2024 we have kept 2 clean sheet (correct me if im wrong). Kumbuka tumekuwa na best line up yetu na tuliendelea kuruhusu magoli. Na bad enough tunaruhusu magoli ya aina ile ile kila mechi. Je Klopp na wenzie hawaoni hili??
Playing high line sometimes is a disaster to us, too many spaces left behind lines, means Klopp ameshindwa kui-set team yake kuwa compact enough. Mechi mbili za City na ile Spurs ndio niliona compactness hatukuacha nafasi nyingi kwenye mistari yetu, najiuliza why tushindwe kufanya hivi kwenye mechi nyingine?

Last four games ama poor line up selection like he did yesterday match or poor subs like he did vs Utd FA match and yesterday match. Klopp ameshindwa kuset good team, upgrading monster mentally and has already satisfied.

Hii ndio inafanya niamini Klopp hayupo nasi tena kifikra isipokuwa kimwili tu. He is just like let season end faster.

Blame to Players.

Chances creating we are the best [emoji736] total excellent[emoji736] but conversion rate totally poor [emoji777]. Tumekuwa wabovu sana katika kukwamisha mpira wavuni.

Big chances creation we are 1st kwa EPL, but conversion rate we are 11th.

Expected Goals (xG) we are 1st but 2nd in goal scoring,

Shots 1st but shot conversion 14th, hizi data zinaogopesha sana kwa timu inayowania makombe, bahati mbaya zaidi ni wabovu kuzuia na kufunga ni wabovu pia. Diaz, Nunez, Gakpo and even Salah and Szobo wameingia kwenye huo ugonjwa wa kukosa magoli mepesi na magumu.




Hapa mkombozi ni Jota our clinical finisher.
Sijui huwa wanawaza nini mbele ya goli, wanajawa wenge na ile hali ya kutaka ku prove watu wrong ndio inawapoteza zaidi. Ukiacha poor line up selection first half chances would put game on the bed. Mechi mbili za utd kipindi cha kwanza kilitosha kumaliza mechi, mechi ya jana 2 goals lead mechi ingeisha ile.

Last two matches we had two errors lead to goals. Quansah vs utd, Szobo vs Atalanta.

Eishhh..!!! upepo mbovu sana huu, finger crossed uishie mechi ya jana.

Huu ni msimu tumekuwa na 4 v 2, 5v2 nyingi za counter attack ila end product sasa dah.!!! Kama Diaz tu dribbling za maana sana chenga nzuri, energy, pace vyote vya uhakika ila end product sasa dah.!





If we had good high conversion rate ya big chances created, lawama zingikuwa chache sana by now.

Precaution:

We might end up parade with Carabao, If things won’t be taken serious.

YNWA.
 
itakuwa akili ya kushikiwa kuhesabu makombe ya Pep kuwa ni makombe ya Arteta.

Sijasema ni Makombe ya Arteta bali nimesema ni Mafanikio ya Arteta.
Huwezi kuhesabu Makombe ya City wakati Arteta yupo bila ya kumuhesabu na yeye.

Sikulazimishi uamini hivyo lakini ndiyo ilivyo.

Kwa Klopp tulimuheaabu Buvac alipokuwa msaidizi wake hivyo na kwa Pep Arteta yupo.

Na hoja yangu ya msingi mimi sijajadili Makombe bali nilijadili ukubwa wa Ligi usinihamishe kwenye Mada tafadhali.

Nilichohoji mimi ni hype anayopewa Amorim kupitia Takwimu zake za Ligi ya Matopeni ni kwamba hazina uhalisia linapokuja suala la EPL.

Wewe ukaleta habari za Arteta, nikakujibu Arteta ametoka EPL, ndiyo hapa ukaja na habari za Makombe jambo ambalo halikuwa hoja yangu.

Wala hoja yangu haikuwa kumkataa Amorim kwasababu sijasema kuwa hafai, bali nimehoji jinsi anavyokuwa over hyped kupitia Ligi ya Mchangani.

Hata Gerrard, Brendan Rodgers walikuwa na Takwimu za kutisha kule Scotland lakini EPL ni kituko.

Na ndiyomana nimemtolea mfano Andre Villas Boas.

Huwezi kufananisha Mtu aliyetoka Ligi ya Mchangani na Artena aliyetoka kuwa Kocha msaidizi ndani ya EPL tena kutoka top team.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…