Upo sahihi Edwards hua ana staili yake ya kusaka wachezaji lakini tutakumbaliana hio staili yake ina favour zaidi FSG kuliko sisi Mashabiki maana tuna EPL moja ndugu tangu atue Klopp, tupime ubora wake kwa makombe anayoleta klabuni na si vinginevyo ndugu, nakua na maoni tofauti kidogo nikilinganisha tulipo kwa kucheki EPL na UCL nk inanipa ugumu sana kuona kama kweli tulistahili tu kupata kombe moja epl chini ya Klopp na kwa mwendo huu wa usajili naona Slot akipita mule mule kwa Klopp aisee. Ni kweli sio kila changamoto inakua solved na usajili lakini tazama asubuhi ya leo unaamka kusoma Morton na Bajetic wapo mbioni kusepa Liverpool wakiwa angalau ndio pekee wenye vi element ya uDm ndani yao maana Edo sitegemei atupe gemu za kutosha huku Gravenberch akiwa ndio makeshift wa Slot.. May we be lucky aisee otherwise its real danger gemu zikianza kuchanganya sioni tukikwepa ya Atlanta.
Kuna Ederson pale Atlanta alikua Upgrade ya hawa wa kwetu lakin utasikia Liverpool hainunui ili mradi kununua na hapo Kipara anasaka EPL ya tano hatanii aisee...
Tukumbali kua wasidikizaji hakuna namna.
Soon Slot atapewa wake up call ataelewa why Klopp had to quit akiwa na the so called complete squad.. Maana kama kweli kikosi ni complete iweje tumalize nafasi ya 3 na kakombe kamoja huku tukikosa mengine matatu...
Kuna mahala Klopp alipishana na Edwards maana iweje Edwards alivyorejea na Klopp akasepa labda Klopp aliona mambo yakusubiri usajili mwaka yanarejea na alishachoka.
YNWA
Mimi naweza kuwa na sababu kadha wa kadha, niki judge kitabu kwa its cover. Klopp alikuwa ndiye mwenye kusema huyu asepe na huyu abaki. Kama ni hivyo hauoni ni sahihi kusema Klopp alitusababisha maumivu kuwakumbatia Injury prones wengi wenye huge wages??
Ox
Keita
Thiago
Matip
Hapo utasema unaweza kugombea chochote?? Mid yako ni Hendo, Milner, Jones,Elliot, na late Fabinho?? Kweli?? Ilikuwa uwongo.
Ukiangalia hapo Kipara alishaachana na Fernandinho, Ferdinand, Toure, Karibu miaka 5 huko nyuma, hao ni viungo tu backline karibu yote iliyompa 2-3 EPL alishaibomoa, kaleta damu changa miguu ya chuma anakiwasha, sisi tunajipa muda labda msimu huu watakaa sawa. Hapa ndipo tulikosea sana sana.
Halafu kati ya Klopp na Edward, Klopp ndio wa kwanza kuondoka na sio baada ya Edward kurudi.
Kumbuka Klopp alitaka kuondoka toka November wakambembeleza January akaja kufunguka, Edward alianza kufuataa Feb mpaka Marcha akakubali the deal. Utofauti wa Edward na Klopp upo kwenye usajili. Edward hakutaka Henderson, Milner na Gomez waongezwe mkataba, Na akatoa optiona zake, Bruno Guimaraes na Enzo Fernandez replacement ya Hendo na Milner, but we all know nani alishinda battle na nani alishinda vita, Edward lost the battle but won the war, Klopp won the battle but lost the war.
Kwa hapa tu ilikuwa ngumu kwa sytem ya Klopp uwe vile vile season in season out.
Mtu kama Salah achunguzwe fitness yake sio mchezo.
Henderseon ( as a team captain, aka geuka injury prone last two season, Klopp alizidi kumuamini huku stats zake zikionesha haziibebi timu)
Mane, Fabinho massively dropped their forms.
Klopp system ilihitaji atleast 2-3 players fresh legs after atleast two seasons, ila hatukufanya hivyo tuliishia kuwa na kina Melo, Kabak, Davies hapa hata kama ni wewe Pep unafanyaje,, ?? Una vuta wine unakunywa pole pole unajua atanisumbua mechi tutakayokuta baasi huko kwingine nitamuacha tu.
Huge praise kwa Klopp kukomaa na Pep licha ya kuwa na Mediocre players.
Sitaki kusema lolote kuhusu signing but what i feel, tutakuwa na less injuries with less long term injuries.