Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Captain Marvelous

kuna paid article naandaa somewhere kuhusu Nunez.

So, how do you see Nunez now? compared na wakati wa Klopp na sasa? ame-improve? if so, what has changed? Slot amemuongezea kipi?

And, future yake unaiona at LFC?
Nunez agent of chaos.
Hana regular starting berth under Slot thus scoring just 2 and an a 1 assist and with Gakpo na Diaz playing as they are well Nunez has fallen below the pecking order as of now.
At Liverpool's his role its a bit different compared na Benfica where he had wing backs and Ramos and Rafa Silva playing in his strength under 442 or 343 formation and his numbers are there to tell especially his second season he was voted best player in the league and scored 26 league goals in 28 games akiwa mfungaji bora wa ligi .
Misimu yake miwili Benfica ligi kuu alifunga goli 32 na assist 14 katika gemu 57 huku gemu akianza gemu 43 na kupewa sub gemu 14 na gemu moja akianzia benchi hivyo utaona akiwa Ureno alicheza dakika nyingi na magoli pia yalikua mengi msimu wke wa pili. Msimu wa kwanza 2020 aliumia na kupata corona hivyo alifunga goli 6 tu. Baada ya kupona hakufunga goli kwa miezi minne na dogo hakuchoka wala kukataa tamaa kwani msimu uilofuata ndio alijitangaza vyema kama strika chipukizi kwa kufunga magoli muhimu Ureno Benfica alichukua ubingwa na champions league akiwafunga Liverpool, Barcelona, Ajax nk nk.
Nunez anang’aa zaidi akicheza lone 9 jambo ambalo Liverpool ni ngumu ukiwa na epic Salah akiwa focal points wa timu hivyo Klopp alijaribu kila namna ku accommodate wote na kwa matokeo tofauti.

Nunez ana ma shoti ya kila engo akitumia mguuu wa kulia na pia ni mzuri mipira ya kichwa.. Ana mishe haswa pale mbele, anahitaji utulivu wa maauzi sahihi wakati sahihi.

Pale ureno hakua na majukummu ya kurudi nyuma kusaidia timu alibaki kule kule mbele kwa kua ni waumini wa kaunta atack wakitumia overlapping full backs.


Ligi Kuu Uingereza amecheza gemu 75 ameanza gemu 44 ametokea benchi gemu 28 huku akifunga goli 21 na assist 12. Amekua akicheza aidha winga wa kushoto au mshambuliaji wa kati. Hua anapedelea kucheza winga wa kushoto tunaposhambulia ili kufungua njia kwa wengine wafunge akiwavuta pembeni mabeki kusud akina Salah etc wapate space za kushambulia.

Mapungufu yake yapo tukianza na la nidhamu tangu atue Liverpool amecheza foul 62 akipewa kadi za njano 12 na nyekundu 1.
Mapungufu mengine amecheza offside mara 53 na hii hapa ndio Slot akomae nae kwani anafanya kila move sahihi kasoro kwenye timing ili akwepe offside trick ya timu pinzani. His offside awareness ndio biggest weakness alionayo hapa Liverpool and the earlier Slot sort that out we have a beast in namba 9.
Pia hajawa clinical akigonga mwamba mara 14 EPL tu. Ina maana Slot na hapa wana kibarua.
Kingine ni klosi zake sio nzuri sana japo sio jukumu lake kuu lakin angalau na hapa Slot apambane nae.
Ukilinganisha na wengine ana goal involvement rate per 90 ipo kama ifuatavyo
Jota 0.36
Nunez 0.25
Gapko 0.23
Diaz 0.80
Salah 0.72
Ukitazama hapo utaona hayupo vimbaya sana compared na dakika anazopata.
Anafunga goli msimu huu kila baada ya dakika 361.
Yupo nafasi ya 56 kwa kufunga kati ya wachezaji 276 EPL.
Assist yupo nafasi ya 41 kati ya wachezaji 276 EPL.
Ana pass completion ya 70.97% needs improvement. Key pass rate ni 0.75.

So anamsaidia aje Slot kwa sasa? With Nunez uwanjani Slot ataona opponent back line inakua pinned kwenye half yao kwa sababu dogo yeye hua anakimbia dakika 90+ hachoki ni pale tu aongeze awareness kukwepa mtego wa offside maana mbio anazo, ana instinct wapi pasi ya Trent etc itatua ishu tu ni wakati gani akimbie. Ni mzuri kutega rebounds shot lakin ishu tu ni accuracy na offside trick.
Tangu atue Slot tunamuona Nunez design kama Firmino in terms of kucheza zaidi kwa ajili ya timu. Tazama stat zake amecheza gemu 10 tu ana tackling 6. Aafu chini ya Klopp kwa misimu miwili alicheza tackling 33 katika gemu 65 hapo utaona Slot anachokitaka ni awe 1st line of defence ili kupoza mashambulizi kwenda kwetu na hii sasa itamfanya awe all round player akiwa threat ndani ya box na nje ya box.

Rekodi Nunez EPL ipo hivi
Offiside 53
Foul amecheza 62
Ametackle 43
Ame block 36
Interception mara 7
Clearance mara 26.
Ina maana Nunez ni work in progress na Slot naanza kumwelewa baada ya kazi nzuriiiiii kwa Gravenberch, Tsimikas, Konate, Diaz na Trent wote tumewaona wamekua next level chini ya Kipara wetu niko na imani Nunez nae atafikia levo hizo.

YNWA
 
asante mkuu
 

Fallen of Nunez at LFC imetokana na
1. Haaland deadly performance
Tukumbuke aliposajiliwa tu ilipigwa battle chonganisha Haaland vs Nunez, reason? Alisajiliwa akiwa goal machine from Benfica majority expected high from him. Price tag ikawa KAMA inaelezea ubora na matarijio yake.
He started very well season after community shield vs City, good performance. Anatokea bench mechi ikiwa 1-1, anatia kichwa inamkuta Diaz ka stretch mkono inamgomga penalty, baadae anatia goli la tatu on his debut. Huku Haaland akiwa na kiwango tofauti na walivyofikiri, his missed with six yard ikaonekana Nunez will shine over Haaland. Game ya kwanza ya Epl anafunga beautiful goal vs Fulham ulimwengu wa mpira ukazidi kumuamini.

2. Red Card

Sasa hapa Nunez alianza kuendewa mrama na mambo. Red card vs Palace hapa ndio ulipoanza upotevu wa Nunez, aliporejea akawa ana kosa nafasi nyingi za wazi huku mshindanishwa nae (Haaland) akawa anaweka tatu tatu, mbili mbili, tokea hapo Nunez hakuwa the same.

Jurgen loves Nunez but Nunez let the gaffer with his misses week in week out halafu ni crucial miss opportunity. Pressure ya Haaland, price tag na ugumu wa ligi.

This season Nunez ameonekana mtulivu sana mguuni na akilini, drop deep defensively play as false 9 imeanza kumkaa. Utulivu umeanza kumuingia, just matter of time we will start to see goals and assists. Last two games angefunga magoli bora sana vs Brighton & Leverkusen.

Ynwa’
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…