Amanijua
JF-Expert Member
- Mar 7, 2014
- 1,776
- 1,619
binafsi simtaki balo kwa kulinganisha na aliyetoka balo hajawai kufikia kiwango cha suarez alichokionyesha msimu uliopita, jamaa sio mpiganaji ni lizito sana
Yaani hapa unajaribu kutuonyesha jinsi gani uwezo wako wa kufikiri ulivyokua mdogo.
Katika maisha ya kawaida kila binadamu ni unique by nature,ndo maana kama wewe unaitwa NGUVU basi tambua kwamba huwezi kufanana na Amanijua hata kama mnafanya kazi moja,mnakula pamoja,mnaishi nyumba moja au mumezaliwa sehemu moja.
Na hata kama kuna mtu mwingine anaitwa NGUVU basi tambua kwamba hawezi kuwa sawa na wewe kwa vitu vingi sana.
Suarez ni mchezaji,amezaliwa Uruguay,ana miaka 28,ni mweupe,anapenda kung'ata,ni mchoyo,ni mfupi,ana watoto wawili,ana ndoto za kuchezea barcelona na mengine mengi,lakn Baloteli ana miaka 24,ni mrefu,ana mtoto mmoja,ni mtukutu,mkorofi,anachezea Italy na mengine mengi.
Nimeandika hivyo ili kuweza kukuonyesha jinsi gani binadamu wanavyotofautiana.
So habari za kulinganisha mtu mmoja na mwingine ni ufinyu wa mawazo,maana kuna mengi ambayo MB anayo Suarez hana na yapo ambayo Suarez anayo lakn huwezi kuyaona kwa Baloteli.
Mwisho ni kwamba mpira ni biashara na wapenzi wa timu tutabaki na liverpool yetu hata kama mchezaji fulani ataondoka kwa kuwa ndo biashara ilivyo.