Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 239
Mechi ya leo ni moja ya ushahidi kwa nini Liverpool, inashindwa kuchukuwa ubingwa wa ligi kuu ya England kwa miaka 18 sasa: Wanaangalia zaidi kushinda mechi moja moja dhidi ya vigogo ili kufurahisha fans wao kuliko kuwa na mikakati makini na mahesabu kuchukuwa ubingwa. Kwa mfano Msimu huu Man wamefungwa na timu vigogo tu, yaani Arsenal na Liverpool, lakini siyo zile vibonde ambazo ndizo za kujichotea pointi.
Liverpool imefungwa na timu vibonde tu msimu huu -- M'Borough na Spurs na kutoka sare na timu nyingine 10, nyingi zikiwa vibonde. Kuchukuwa ubingwa siyo kuifunga Man au Chelsea tu (ingawa ina raha yake hasa kwa fans). Kuchukuwa ubingwa ni namna ya kuweka mikakati ya vipi kujilimbikizia pointi katika mechi 38.
Kila msimu kuna mashindano manne yaani PL, CL, FA Cup na carling Cup, lakini inavyoelekea hawajui priorities zao na in the end hutoka kapa kila baada ya msimu. Bila shaka mashindano kama vile FA Cup na Carling yanawachanganya. Hapo ndipo Mzee Fergie huonyesha umahiri wake.
Leo Liverpool wamepata ushindi mnono dhidi ya Man, tena kwao na wataushangilia sana ushindi huo huku wanajua kuwa Man watacheka mwisho kwani sasa hivi kilichobakia ni kila timu kuiombea nyingine ifungwe katika mechi zilizobakia -- kitu ambacho ni mtihani zaidi kwa Liveropool kuliko Man. Kwa mfano Man wanaweza kuafford kufungwa hata mechi mbili kati ya zilizobakia (nafikiria Man City na Arsenal) na bado wakaibuka mabingwa.