Hivi alikuwa mchoyo au sisi mashabiki ndo tulikuwa tunataka amu assist MANE kwasababu tu za ubaguzi wetu? Maana kama alikuwa anaongoza kwa assist Uchoyo uko wapi?
Afadhali Mkuu umeongea.
Walitaka atoe assist hata kama anaona mpira utakwenda kupotea .
Asipotoa assist,akapiga chenga akafunga tunasema Salah ni mwamba sana.
Akipiga bahati mbaya asifunge,tunasema Salah mchoyo.
Hata Mane mwenyewe mbona kuna muda huwa anakuwa mchoyo,anataka afunge yeye..yaani ukiconcentrate kumuangalia mtu mmoja mwanzo mwisho,lazima utafika point utamuona kama mchoyo
Kiufupi uchoyo pale mbele ni unkwepable[emoji23] inevitable,hauepukiki.
Kuna muda Salah alishafyatuka yupo mbele sana,anapiga pass kwenda upande mwingine,unashangaa wale wenzie bado hata hawajafika,,mpira unawazidi speed na hatimaye unapotea.
Akisema aendelee kupiga nao chenga na kujaribu kufunga ,akiwa anawasubiri wengine wasogee ndio hayo unasikia eti Salah mchoyo.