Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Breaking News🚨: Liverpool ready to offer Ibrahima Konate new contract with Arne Slot plotting long-term future for defender.

Konate’s efforts are set to be rewarded with a brand new contract,
With so much focus on the contract situations of Trent Alexander-Arnold, Virgil van Dijk and Mohamed Salah, the fact that Konate’s current deal only runs until 2026 has been overlooked.
Now we are talking.... Don't wait mpaka hawa wachezaji wabakishe siki kadhaa ndio kutoa nyongeza... Mapema mambo yanakua sorted.

YNWA
 
Alisson Becker and Alexis Mac Allister will undergo further assessment to determine the severity of the injuries they sustained during Saturday's 0-1 win at Crystal Palace.

Mac Allister was replaced at half-time at Selhurst Park, while Alisson went down and was unable to continue after 79 minutes of the Premier League fixture.
 
IMG-20241005-WA0040.jpg
 
It is always tough at Selhurts Stadium for Liverpool.

Mechi kama hii ilitunyima ubingwa 2013/2014. Zilibaki mechi 3,

Chelsea at Anfield
Crystal Palace at Selhurts
Newcastle Anfield

Mechi ya Chelsea tukapoteza 0-2, Demba Ba akiingia kambani after famous Gerrard slip, later on, Willian akamalizia msumari wa pili. Hapo matumaini yakawa a must win for the last two games, ambayo ni C. Palace & Newcastle.

Kipute kikapigwa, mpaka dakika ya 55 ubao ni 0-3, magoli ya Joe Allen, Daniel Sturridge na Luis Suarez( one man army).

All of a sudden vijana katili wa Tony Pulis mwamba mwenye mbinu zake za kupaki bus, wakaanza marejesho bila riba, moja baada ya nyingine. Baadae Pulis kafanya subs zake akamuingiza jamaa mmoja hivi kama ana albinism hivi, anaitwa Dwight Gayle sitamsahau,mpuuzi huyu katili hakumuhurumia hata Stevie G’. Dakika ya 79 wakapata goli moja, tukaona aah, haina tatizo wametuharibia cleansheet tu, aliyeingia D. Gayle akarejesha moja dk ya 81’ he.! tukaanza kuona hali imeanza kuwa mbovu, mpuuze yule akaja kuweka la tatu dk ya 88’ na safari ya Stevie G kulitwa taji la EPL likakomea hapo.

Kuanzia hapo ndipo Selhurts ikaanza kuwa ngumu sana, baada ya kizazi kile cha kina Y. Bolasie, Jason Puncheon winger moja haramu hivi, wakaja kina Zaha, mpaka Olisse na Eze, wamekuwa aakitupa tough tough game sana. Mtashinda lakini mtalala na viatu.

Ndicho wamekifanya leo, tough game with a margin of 0-1, utaelewa nini maana ya pressure. Ubora wa Becker leo umetupa clean three points.

As i said before the game wale jamaa sawa ni kuwafunga mapema kwa kadiri ya iwezekanavyo kwenye 3-4-2-1 yao unaona defensively ni 5-3-2, na ndizo team huwa tuna struggle nao sana, and we did it early 9’ Tsimi, Gakpo wakatengeneza goli zuri sana.

Anachokupa Gakpo sicho anachokupa Diaz ila anachokupa Diaz, Gakpo anaweza kukupa. Why.? Goli alilofunga Jota kama ni Diaz alikuwa kwenye ile situation basi ungetegemea, aendeleze ku hold mpira na kutafuta nafasi ya kufunga. But Gakpo was to quick to see opportunity.
Utofauti wao ni kwenye “maamuzi”, Gakpo ni mwepesi sana wa kuona chances aliyenayo yeye ni ngumu kuliko nikumpa next player thats the different.

Na mechi kama hizi unahitaji one profitable decision.

Kama hauwezi kutengeneza chances basi hakikisha ulichokipata unakilinda, ndicho hufanya Slot sasa hivi, and thats football.

Second half, things weny otherwise sababu ya Macca. Macca yule ndiye “mtuliza bahari” refer after his sub vs NF, alipotolewa yeye uwanja ukainama na wakaanza kufunguka and it paid them, again today after forced sub ya Macca unaona kabisa tumekosa mtu wa kutuliza bahari, we relied on Jones, but he isn’t that guy unaweza kumtegemea through out 90’ mins. Hence unaweza kuwa na tactics zile zile, kila kitu kile kile ila ukimkosa MFANISI wa kutekeleza mbinu zako basi mbinu zako zinafeli.

Palace wakaamua kufunguka na kujaa katikati, baada ya kutest the possibilities na wakaona ooh it might eeh.!!! Lets try we can do it, wakaanza ku press high with loads of no.s, Boom it helped them alot Becker akawa tested mara kama tatu hivi na zote akafanya anayofanya siku zote ‘great saves’. Palace wakaacha kutegeana, wakaamka, wakacheza kama timu, wakaamka kweli kweli, unfortunately to them Becker was under three posts.

Alipotoka Salah upande wa kulia ukawa weak, Diaz alijikuta LW, hauwezi kumlaumu ni ngumu kucheza position ambayo haujaizoea kwa mechi kama ile.

Praise Macca alot, hii ndio cheating code ya Slot, acha Gravern afanye anayofanya though Macca anasema its luck to play with Gravern, but they are all luck for sure.

There is a time you have to lose the battle and win the war, we lost the battle especially 2nd half but we won the war.

Was it a penalty or not,?

Kwa mujibu wa sheria inahitaji mchezaji aliyechezewa foul awe na impact kwenye mchezo huo. Binafsi i said yea its a penalty, but wakaja kusema it is not a penalty because aliyefanyiwa foul hakuwa na impact yoyote na mpira ule. Hata angeachwa asingefanya chochote, thats why it shouldn’t be a penalty as it didnt.

Jaros.

Promising GK hajawa proved kuwa wa level hizo but i like his confidence. Mbele yako kuna Konate na Vvd utakuwa na less pressure.

Je Cleansheet itakuwa ya Jaros au Becker?
Cleansheet atapewa Becker kwa sababu ndiye amecheza mechi nyingi kuliko Jaros, So another cleansheet for Big man Becker.

Get well Soon Becker you are needed alot toward tough two months.

October to 1st December, two good Months for Slot to be tested with his boys, wataulizwa maswali na:-
Madrid
Arsenal
City
Chelsea
Leipzig
Leverkusen
Brighton twice

All are well with RED Army.

Top of the table for almost next two weeks[emoji736]
Cleansheet[emoji736]
Three crucial points [emoji736]

Up Liverpool
Go Slot
Ynwa’
 
Saint Anne sometimes lets talk about the reality, kumsema vibaya Allison kama ni kwenye magroup ya whatsapp ungekuwa umeshakuwa removed. Allison ndio Gollie bora duniani. Na kwa mfumo wetu mpaka goli anafungwa elewa uzembe au kukosa umakini unakuwa umeanzia mbele kabisa kwa kina Salah/Diaz/Jota maana ulinzi huwa uaanzia kwa Mastraika. Mpumzishe aisee. 😂😂😂😂
 
Saint Anne sometimes lets talk about the reality, kumsema vibaya Allison kama ni kwenye magroup ya whatsapp ungekuwa umeshakuwa removed. Allison ndio Gollie bora duniani. Na kwa mfumo wetu mpaka goli anafungwa elewa uzembe au kukosa umakini unakuwa umeanzia mbele kabisa kwa kina Salah/Diaz/Jota maana ulinzi huwa uaanzia kwa Mastraika. Mpumzishe aisee. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Heheh

Watoto wa alfu mbili bana, halafu wa kike inabidi uende nao hivyo hivyo”,.. ukiwa serious kichwa kita knock.
 
Heheh

Watoto wa alfu mbili bana, halafu wa kike inabidi uende nao hivyo hivyo”,.. ukiwa serious kichwa kita knock.
Kuna group la Liverpool One Family huwa na copy na kupaste posts zako aisee huwa napigwa sana mawe japo kuna maelezo ya kutosha
 
Kuna group la Liverpool One Family huwa na copy na kupaste posts zako aisee huwa napigwa sana mawe japo kuna maelezo ya kutosha

Heheh kaka mtizamo wa mpira ni tofauti, na inategemea mtu anaangalia kwa angel ipi? Ila ukiona unapingwa sana mambo ni mawili.

1. Sio mambo wanapaswa kuelewa
2. Mambo yamezidi kimo cha fikra zao.


Kwa ufupi tunaelewa yale ubongo unataka kuyaelewa.

Hata humu kuna watu hawamkubali Slot na Gravern thats why ikitokea mambo yameenda kombo utaona reaction zao.

Nilijua Slot anatosha, kumbe bado?! as if Klopp na waliopita were invisible.

Nilijua Gravern atatufikisha salama,. Unaona mtu kama huyu ni shabiki wa LFC lkn humo humo ndani kuna ambavyo havipendi na anatamani viharibike aje aseme nilisema.

‘TUISHI NAO VIVYO HIVYO MKUU’

Ynwa’
 
Saint Anne sometimes lets talk about the reality, kumsema vibaya Allison kama ni kwenye magroup ya whatsapp ungekuwa umeshakuwa removed. Allison ndio Gollie bora duniani. Na kwa mfumo wetu mpaka goli anafungwa elewa uzembe au kukosa umakini unakuwa umeanzia mbele kabisa kwa kina Salah/Diaz/Jota maana ulinzi huwa uaanzia kwa Mastraika. Mpumzishe aisee. 😂😂😂😂
Kuwa removed siyo shida mbona
Mpira lazima tutofautiane mawazo.
Ile goli hata wewe ungefunga,ni mpira tu ulimpitia kichwani..alibahatisha
Ni kama vile Kelleher alivyofunga goli la ushindi la Carabao la penalty ya 11 dhidi ya Chelsea..huku kepa akipaisha mawinguni
Ni kama vile tu baadhi ya watu ambavyo hawamuapprecciate Kelleher..hata adake vipi.. wanasubiri afungwe ili waanze kumnanga kwamba hafai kuwa golikipa wa mechi za ligi kubwa.

Ni sawa pia, watu wanavyomdis Trent,
Lakini pia ni sawa tu na watu wanavyomtukana Klopp Kwa matusi yote, licha ya yeye kututoa matopeni.

Kwahiyo utofauti wa mawazo ni kitu cha kawaida.
 
Back
Top Bottom