It is always tough at Selhurts Stadium for Liverpool.
Mechi kama hii ilitunyima ubingwa 2013/2014. Zilibaki mechi 3,
Chelsea at Anfield
Crystal Palace at Selhurts
Newcastle Anfield
Mechi ya Chelsea tukapoteza 0-2, Demba Ba akiingia kambani after famous Gerrard slip, later on, Willian akamalizia msumari wa pili. Hapo matumaini yakawa a must win for the last two games, ambayo ni C. Palace & Newcastle.
Kipute kikapigwa, mpaka dakika ya 55 ubao ni 0-3, magoli ya Joe Allen, Daniel Sturridge na Luis Suarez( one man army).
All of a sudden vijana katili wa Tony Pulis mwamba mwenye mbinu zake za kupaki bus, wakaanza marejesho bila riba, moja baada ya nyingine. Baadae Pulis kafanya subs zake akamuingiza jamaa mmoja hivi kama ana albinism hivi, anaitwa Dwight Gayle sitamsahau,mpuuzi huyu katili hakumuhurumia hata Stevie G’. Dakika ya 79 wakapata goli moja, tukaona aah, haina tatizo wametuharibia cleansheet tu, aliyeingia D. Gayle akarejesha moja dk ya 81’ he.! tukaanza kuona hali imeanza kuwa mbovu, mpuuze yule akaja kuweka la tatu dk ya 88’ na safari ya Stevie G kulitwa taji la EPL likakomea hapo.
Kuanzia hapo ndipo Selhurts ikaanza kuwa ngumu sana, baada ya kizazi kile cha kina Y. Bolasie, Jason Puncheon winger moja haramu hivi, wakaja kina Zaha, mpaka Olisse na Eze, wamekuwa aakitupa tough tough game sana. Mtashinda lakini mtalala na viatu.
Ndicho wamekifanya leo, tough game with a margin of 0-1, utaelewa nini maana ya pressure. Ubora wa Becker leo umetupa clean three points.
As i said before the game wale jamaa sawa ni kuwafunga mapema kwa kadiri ya iwezekanavyo kwenye 3-4-2-1 yao unaona defensively ni 5-3-2, na ndizo team huwa tuna struggle nao sana, and we did it early 9’ Tsimi, Gakpo wakatengeneza goli zuri sana.
Anachokupa Gakpo sicho anachokupa Diaz ila anachokupa Diaz, Gakpo anaweza kukupa. Why.? Goli alilofunga Jota kama ni Diaz alikuwa kwenye ile situation basi ungetegemea, aendeleze ku hold mpira na kutafuta nafasi ya kufunga. But Gakpo was to quick to see opportunity.
Utofauti wao ni kwenye “maamuzi”, Gakpo ni mwepesi sana wa kuona chances aliyenayo yeye ni ngumu kuliko nikumpa next player thats the different.
Na mechi kama hizi unahitaji one profitable decision.
Kama hauwezi kutengeneza chances basi hakikisha ulichokipata unakilinda, ndicho hufanya Slot sasa hivi, and thats football.
Second half, things weny otherwise sababu ya Macca. Macca yule ndiye “mtuliza bahari” refer after his sub vs NF, alipotolewa yeye uwanja ukainama na wakaanza kufunguka and it paid them, again today after forced sub ya Macca unaona kabisa tumekosa mtu wa kutuliza bahari, we relied on Jones, but he isn’t that guy unaweza kumtegemea through out 90’ mins. Hence unaweza kuwa na tactics zile zile, kila kitu kile kile ila ukimkosa MFANISI wa kutekeleza mbinu zako basi mbinu zako zinafeli.
Palace wakaamua kufunguka na kujaa katikati, baada ya kutest the possibilities na wakaona ooh it might eeh.!!! Lets try we can do it, wakaanza ku press high with loads of no.s, Boom it helped them alot Becker akawa tested mara kama tatu hivi na zote akafanya anayofanya siku zote ‘great saves’. Palace wakaacha kutegeana, wakaamka, wakacheza kama timu, wakaamka kweli kweli, unfortunately to them Becker was under three posts.
Alipotoka Salah upande wa kulia ukawa weak, Diaz alijikuta LW, hauwezi kumlaumu ni ngumu kucheza position ambayo haujaizoea kwa mechi kama ile.
Praise Macca alot, hii ndio cheating code ya Slot, acha Gravern afanye anayofanya though Macca anasema its luck to play with Gravern, but they are all luck for sure.
There is a time you have to lose the battle and win the war, we lost the battle especially 2nd half but we won the war.
Was it a penalty or not,?
Kwa mujibu wa sheria inahitaji mchezaji aliyechezewa foul awe na impact kwenye mchezo huo. Binafsi i said yea its a penalty, but wakaja kusema it is not a penalty because aliyefanyiwa foul hakuwa na impact yoyote na mpira ule. Hata angeachwa asingefanya chochote, thats why it shouldn’t be a penalty as it didnt.
Jaros.
Promising GK hajawa proved kuwa wa level hizo but i like his confidence. Mbele yako kuna Konate na Vvd utakuwa na less pressure.
Je Cleansheet itakuwa ya Jaros au Becker?
Cleansheet atapewa Becker kwa sababu ndiye amecheza mechi nyingi kuliko Jaros, So another cleansheet for Big man Becker.
Get well Soon Becker you are needed alot toward tough two months.
October to 1st December, two good Months for Slot to be tested with his boys, wataulizwa maswali na:-
Madrid
Arsenal
City
Chelsea
Leipzig
Leverkusen
Brighton twice
All are well with RED Army.
Top of the table for almost next two weeks[emoji736]
Cleansheet[emoji736]
Three crucial points [emoji736]
Up Liverpool
Go Slot
Ynwa’