Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

BR aliyewahi kufanya kz chini ya Mourinho Eti asiwe anatabilika ktk mbinu Zake! Teh Teh Teh Teh

Kufanya kazi chini ya Mouthrinho siyo issue...the guy (BR) is something else tactically.
Anyway our focus now is Big Sam...West Ham.
 
LIVERPOOL 4 VS TOTTENHAM 0 (30Mar2014)
Alama zangu za viwango kwa wachezaji wa Liverpool

1. Simon Mignolet – 7
Kipa hakupata misukosuko sana ingawa tuliona umahiri wake alipookoa shuti la Bentaleb. Alikuwa ametulia na distribution zake zilikuwa zina macho

2. Glen Johnson – 8
Anastahili kupata lama 8. Krosi yake ndiyo iliyozaa goli la kwanza na kutoa nuksi. Ushirikiano wake na Sterling ulionekana kuwapa shida walinzi wa Spurs. Rose had a hard time!

3. Daniel Agger – 8
Kempteni msaidizi amekuwa akisakamwa sana kwamba kiwango chake hakiridhishi. Jana hali ilikuwa tofauti kabisa. Utulivi na pasi zake ziliweza kujenga mashambulizi kuanzia nyuma.

4. Martin Skrtel – 7
Kila mmoja atakubali kwamba blocking aliyoifanya against Eriksen was a goal opportunity. Alifanikiwa kumweka mfukoni Soldado kama alivyofanya kwa van persie…

5. Jon Flanagan – 7
Bwana mdogo kiwango kinazidi kupanda. Aliweza kumzibiti Eriksens wakati akiwa na nafasi nzuri. Ila wengi tutamsifu alipouwahi mpira ambao ulikuwa na madhara sana endapo Soldado angeufikia…was it penalty?...hivi aaron lennon alikuwepo uwanjani? …ahahahahahaaa

6. Stephen Gerard – 8
“Captain Fantastic” kama kawaida with a cool head ameonyesha ni kitu gani kinastahili kufanywa na mtu mzoefu in crucial moments. Wakati wote amekuwepo kusaidi defenders and things looks very secured when he was around. Well done Stevie G!

7. Philippe Coutinho – 8
A little Brazilian wizard, wote tulishuhudia distribution zake zilivyokuwa zikizaa matunda. Hivi unajua kwamba goli alilolifunga alitoka na mpira toka katikati ya kiwanja? Amazing!

8. Jordan Henderson – 8
Engine room ilifanya kazi yake kuhakikisha hakuna midfielder wa spurs anayepumua. Bilashaka eriksen atajilaumu sana kusajiliwa na spurs kwa kuikataa Liverpool. Baada ya kuwa cleared kwamba goli ni la kwake na siyo Suarez then I bealive ataongeza juhudi kwenye mazoezi ya free kicks

9. Raheem Sterling – 9
Ukimweka pembeni Elpistorelo, Raheem Sterking nimempa marks za juu kwasababu naamini anastahili. Alivyochangia kwenye goli la kwanza. Alivyowatoka mabeki na kupiga kross iliyotua kichwani kwa Surez na kuokolewa na Loris. Speed & pass accuracy. Hata pale kocha alipombadilisha na kumrudisha kati baada ya kumtoa couti, dogo aliendelea kuleta balaa. But I still think he should have score when he was face to face with Lloris

10. Luis Suarez – 9
Yamesemwa mengi na yanaendelea kusemwa mengi. Hakuna asiyejua heshima aliyonayo Robbie fowler kwenye ulimwengu wa soka. Definately, inahitaji mashine, jembe la ukweli kuweza kumzidi gwiji Fowler. Kama unabisha kwamba surez siyo mashine then, rudia kuangalia tena mechi ya jana...baada ya filimbi ya mwisho waangalie danny rose, kaboul, dawson walivyokuwa wamechakaa kwa shughuli waliyo kutana nayo toka kwa the Gladiato!!!

11. Daniel Sturridge – 8
Liverpool so far ni timu ambayo haichezi tu mpira bali inatoa burudani at the same time. Burudani hii, haitoki kwa couti, elpistolero au sterling peke yao, ila pia kwa mshambuliaji tegemeo kwa taifa la England. Kocha anamtumia kama central striker lakini he always interchange his position with Suarez. Nina hakika mabeki wa spurs wana kitu cha kuhadithia

Aione Ntuzu...!
 
Last edited by a moderator:
We nawe umezingua kabla ya Rogers alikuwepo king Danglish kabla ya Roy hogson na ndio Benitez kutoka kwa Gerald Hollier
mkuu ommy ingekuwa vizuri Kabla kurukia maneno watu ungechunguza watu walikuwa wanasema nini? Mpaka yalifikia hapo zaidi ungeyawacha tu Mbu aliuliza kwa kusudi akasema najuwa watu watakuwa Hawana kumbukumbu tena Manager Kabla ya Rogers alikuwa nani? Na aliuliza kwa utani na sio Kama watu hatujui ila sababu tumetaka kumjibu kwa ujeuri ndo tukaruka na kusema Benitez alileta CL makusudi na yeye kaelewa Kama tuna leta jokes kaka hapa pazoeee hizi zote ni Banter za utani. Haina haja mtu kumuhakikishia umeanza ushabiki lini Kama enzi za Toshiba au. Candy au Carslberg au Bank Ads wewe shabikia tu hata Kama umeanza Leo haina ubaya LFC YNWA! Upendo muhimu Humu watu kutaniana kawaida ndomana Ntuzu anashinda Humu na maji anapewa kiu kinamuumiza Chelsea japo maji ya Shingo, Ntuzu vipi upo hehehe..
 
  • Thanks
Reactions: Mbu

Aione Mbu...!
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: Mbu
Brendan Rogers akibeba kombe mtasikia jinsi media za UK zitakavyoanza kuchonga umuhimu wa kuwa na makocha wa kibritish na zitawasakama makocha wa kigeni kama wanavyowasakama wachezaji wa kigeni
media ni kweli kuna British na Kuna. English Kama ni British Sir Alex ni British na Kenny ni British na George Graham ni. British walishinda League na. Shankly ni Britiswalishinda League wote ukichunguza ni Scotish England au English wao Hawana ma Manager wazuri Rogers ndio British ila Sio English angekuwa. English ndio angepambwa anapewa sifa sababu alivyoisafisha timu na hakutoka timu kubwa, British Muengereza hampambi Scotish wala Irish English Manager wazuri alikuwa Bob paisley na Brian Clogh na wote hawa walijifunza kwa ma. Scotish duniani ma Manager wazuri ni Italy timu kubwa na ndogo na Holland Mie English mmoja tu angepewa nafasi angefanya vizuri ni Glenn Hoddle jamaa smart Sema alivyosema kuhusu vilema ilimponza jamaa anapesa ndomana Hana muda wakurudi football waliobakia English Manager hakuna kitu Kama Big Sam na. Parades hapa EPL manager ni Arsene. Wanger tu sasa hivi.
 
Kila mwanaliverpool ana hamu sana ya kuona timu yitu inaendelea kushinda na hatimae kutwaa ndoo ya BPL. Kutokana na hilo basi kila mmoja anajitahidi kutoa mchango na fikra zake ili kuweka hai matumaini ya ubingwa. Hiyo paragraph ya mwisho umesema we should be defensive minded… well bilashaka sababu iliyokusukuma kufanya mabadilia ya Sakho for Agger na Lucas for Allen or Couti ni kwaajii ya kuimarisha ulinzi.
Mimi naomba nitofautiane na wewe kwenye hili kwasababu zifuatazo.
1. Liverpool formation, confidence, fluidity and mentality
Kwa kipindi kirefu wapenda soka tumekuwa tukiiona timu ya barca ikicheza soka safi ya kupendaza na kufunga magoli jinsi wanavyotaka. Hayo ni matunda ya wachezaji kukaa pamoja kwa muda mrefu na hivyo kuelewana. Jambo hili limeanza kujitokeza kwenye timu ya Liverpool ingawa wachezaji hawajaa pamoja kwa muda mrefu kama wale wa barca. Long passes ambazo zimekuwa zikipigwa na either Gerrard ama coutinho zimekuwa zikifika miguuni mwa either suarez ama Sturridge/sterling. Hilo ni moja ya tunda la ushirikiano unatokana kucheza pamoja. Nafikiri utakumbuka goli alilofunga suarez dhidi ya Cardiff, sturridge akito assist ya kisigino bila kuangalia nyuma. Ile siyo bahati bali mahusiano ya kiuchezaji. Kwa bahati mbaya Sakho na Lucas wamekumbwa na majeruhi yaliyowafanya kukaa nje kwa muda mrefu na hivyo kukosa nafasi ya kuwa pamoja na wenzao.

2. Agger vs Sakho
Kwa kuzingati hayo niliyoyainisha hapo juu. I would prefer to continue with our vice captain. Mechi ambayo inaweza ikanipa wasiwasi na kufikiria kumchezesha Sakho instead ni mechi ya west ham. Sababu nyingini ni uzito wa Sakho kwenye maamuzi. Agger got quick feet na hilo limekuwa likisaidi kwenye kuanzisha mashambulizi toka nyuma. Goli kipa yeyote anategemea sana mawasiliano mazuri na endelevu kwa mabeki wake. Kwa kumbadilishia Mignolet CB’s kila wakati kunamfanya kushindwa kuwa na command ya territory yake.

3. Lucas/Allen
Jana (Liver4, spurs 0) tumeona kocha hakuanzisha chaguo lako “Lucas” probably ni kwasababu ya speed and fluidity aliyoitaka. Lucas yuko slow tabia ambayo inakatisha mshambulizi. Pamoja na kuwa slow lakini pia Lucas is not a good passer like coutinho. Allen is a good passer but couti is more skilful and he can score as well

4. West ham vs Liverpool
Bilashaka uliona kilichotokea kwenye mechi ya west ham vs chelsick. Big sam alimua kupanga basi mpaka spesho mouth akaenda kushtaki kwa waandishi wa habari!..ehehehehe mkuki kwa nguruwe…
I am sure west ham watafanya the same thing kwasababu they know the can’t take a chance and open up against the deadliest SAS. Kwanini tusifungulie full cylinder kama tulivyofanya kwa Aseno? Wasiwasi ni hw to deal with long balls to andy…

5. Liverpool vs Chesick
Hapo tegemea basi zakutosha. I beat spesho mouth anaweza asipange striker hata mmoja and instead atajaza holding midfielders wote aliyonao. Sasa kama wao watakuwa defensive like that, then kwanini sisi tuwe tena defensive? Tuko nyumbani and we should Attack! Attack! Attack! Mpaka kibabu Terry kijifunge…ehehehehehehe

6. Liverpool vs Man city
This has to be a wonderful game. Confidence iliyopo iendelee kujengwa kwa kuendelea kucheza mchezo wa kushambulia from the start. Kuna kamchezo Brendan amekuwa akikifanya na mimi nimekashtukia. Kuna wakati huwa anamhamisha sterling to wing na kumchezesha middle, nyuma ya central striker. He has been very effective on that position sababu ya pace, dribbling and killer passes. Yaya tumemshuhudia akichoka mapema, Fernandinho anatumia nguvu nyingi bila maarifa. Milner is too direct. Liverpool should not sit back but pressing high. This should be a mach of the season. But I will protest if FA selects Webb to referee
But I have some reservations..I love Agger, however I think he should be benched for Sakho..alafu Lucas should return to the team too but I dont know at whose expense.

I think for the remaining 6 games, our starting line up should be:

Mingolet.

Johnson Sktrel Sakho Flanagan

Lucas, Henderson Gerrad

Sturridge, Suarez, Sterling/Coutinho.

Brendan anampenda sana Allen..sidhani kama anaweza muweka bench hata kwa mechi mbili mfululizo.

Mnaonaje?

we need to be more defensive minded...especially against Chelsea and Man City..against West Ham and the like, we can afford a very strong attacking line up like today.
 
Mkuu Ntuzu, una kikosi gani ambacho kinaweza kuitisha Liverpool pale Anfield?????..Au ile misese yako mitatu pale Mbele??..Torres, Etoo na Demba Ba, ambao sidhan hata imefikisha magoal 20 kweny league msim huu..???.Au kina Willian na Mwenzake Ramirez wanaocheza mpira kama wanapakua mizigo sokon???..Nguuuuvu nyiiiing, akili kidogo, Maskini yule Willian zaman alikuwaga fundi sana alikuwa anapiga mpira laini kama wa kina Coutinho, Alcantara, Iniesta, Ozil, Silva, Carzola, Lakin tangu aje hapo Chelsea anapiga mpira MGUMU saaaana...MATA angekaa hapo chini ya huyo Morinyo angepotea saaana....
 
Me nadhan ugenini kutumia formation ya 4-3-3 ni risky sana, so naamini kabisa BR atamdrop coutnho au Sterling, ili kutoa nafas kwa Allen au Lucas, Kucheza na SG katkat pale, ili kuControl kiungo pale katikati..Na nadhan Allen atafaa zaid, kwasababu ni good passer na anauwezo wa kumilik mpira na kupunguza pressure, Lets be realstic here, Nadhan Lucas kiwango chake kimepungua sana Msimu huu, yaan ni kama Skrtel ilivyokuwa last season..Nadhan hata ile game ya Jana, Spurs walivyomtoa Bentleb na kumwngza Dembele, BR naye fasta fasta akamtoa Countinho na Kumwingza Allen, ili kubalance kiungo.
 
Mkuu Ntuzu, una kikosi gani ambacho kinaweza kuitisha Liverpool pale Anfield?????..Au ile misese yako mitatu pale Mbele??..Torres, Etoo na Demba Ba, ambao sidhan hata imefikisha magoal 20 kweny league msim huu..???.Au kina Willian na Mwenzake Ramirez wanaocheza mpira kama wanapakua mizigo sokon???..Nguuuuvu nyiiiing, akili kidogo, Maskini yule Willian zaman alikuwaga fundi sana alikuwa anapiga mpira laini kama wa kina Coutinho, Alcantara, Iniesta, Ozil, Silva, Carzola, Lakin tangu aje hapo Chelsea anapiga mpira MGUMU saaaana...MATA angekaa hapo chini ya huyo Morinyo angepotea saaana....

Teh Teh Teh Teh! Ivi wewe unakikosi gani cha kuisumbua Chelsea?

Nimepita ktk machinjio ya hatari tena yenye safu za kushambulia zenye uchu Lkn wamechemka!

Machinjio ya Etihad wote nyie mmeacha point 3 na vipigo vikibwa Lkn hiyo unayoiita miseseta na Mourinho walitua pale Etihad na wakavunja rekodi! Sembuse wewe jogoo uliezeeka?

Chelsea kila mchezaji anakufunga Kwahiyo km tukitua hapo sijui umkabe nani umuache nani? Sio nyie akishikwa zombi mnyonya damu na yule mnyaturu Wa kiingereza Daniel Basi Hakuna tena mpachika magoli!

Teh Teh Teh Teh
 
mkuu ommy ingekuwa vizuri Kabla kurukia maneno watu ungechunguza watu walikuwa wanasema nini? Mpaka yalifikia hapo zaidi ungeyawacha tu Mbu aliuliza kwa kusudi akasema najuwa watu watakuwa Hawana kumbukumbu tena Manager Kabla ya Rogers alikuwa nani? Na aliuliza kwa utani na sio Kama watu hatujui ila sababu tumetaka kumjibu kwa ujeuri ndo tukaruka na kusema Benitez alileta CL makusudi na yeye kaelewa Kama tuna leta jokes kaka hapa pazoeee hizi zote ni Banter za utani. Haina haja mtu kumuhakikishia umeanza ushabiki lini Kama enzi za Toshiba au. Candy au Carslberg au Bank Ads wewe shabikia tu hata Kama umeanza Leo haina ubaya LFC YNWA! Upendo muhimu Humu watu kutaniana kawaida ndomana Ntuzu anashinda Humu na maji anapewa kiu kinamuumiza Chelsea japo maji ya Shingo, Ntuzu vipi upo hehehe..

Teh Teh Teh Teh!

Naona mmekua mnaongea sn! Jogoo kafufuka!
 
Teh Teh Teh Teh! Ivi wewe unakikosi gani cha kuisumbua Chelsea?

Nimepita ktk machinjio ya hatari tena yenye safu za kushambulia zenye uchu Lkn wamechemka!

Machinjio ya Etihad wote nyie mmeacha point 3 na vipigo vikibwa Lkn hiyo unayoiita miseseta na Mourinho walitua pale Etihad na wakavunja rekodi! Sembuse wewe jogoo uliezeeka?

Chelsea kila mchezaji anakufunga Kwahiyo km tukitua hapo sijui umkabe nani umuache nani? Sio nyie akishikwa zombi mnyonya damu na yule mnyaturu Wa kiingereza Daniel Basi Hakuna tena mpachika magoli!

Teh Teh Teh Teh

Eti Mnyaturu wa Kiingereza...nimecheka kweli! Unautani na kamanda Mangu au Tundu Lissu mkuu.

All in all pale Anfield lazima mkae tu!
 
Mimi bado I have memories of Heysells in 1985............RIP all Liverpool brothers and sister who lost their lives that night.
 
hahahah..We Ntuzu, Huyo Man City anaekupa kiburi kisa eti ulimfunga, Nae alikaa kwa team kama Cardiff na Sunderland, asa sembuse wewe na wale wamakonde wako kibao wale ambao babu zao walikimbilia Brazil wakat wa buashara ya Utumwa kipich hichooo, Wanacheza mpira mgumu kama nn, Afu me syo kama Manure au Arsenal, nlikufuka kifo cha kawaida tu Etihad pale 2-1...
 
Yaani Ntuzu, ChelshiT mkitufunga Pale Anfield, Nahamia Mgambo JKT ya Tanga moja kwa moja......

HUWEZI KUNIFUNGA...
 
Eti Mnyaturu wa Kiingereza...nimecheka kweli! Unautani na kamanda Mangu au Tundu Lissu mkuu.

All in all pale Anfield lazima mkae tu!

Umefurahi? Teh Teh Teh Teh, haya ndio mambo ya mpira!

Jamani Ivi niwambieje ndio mnielewe? Mnaikumbuka vzr Liver ya Benitez? Ile ndo ilikua bomba kucheza nayo sio hii yenu ya sasa! Lkn tulikua tunakutana USO Kwa USO mpk Benitez kukaa kwenye kiti anashindwa! Anakaa kwenye majani na miwani yake! Kamuulize Johan Rise Kwanini aliondoka Liver?

Chezea Chelsea weye?! Chelsea ndio kiboko Yao ulaya! Waulize B Munich, Fc Barc, Napoli etc!
 
hahahah..We Ntuzu, Huyo Man City anaekupa kiburi kisa eti ulimfunga, Nae alikaa kwa team kama Cardiff na Sunderland, asa sembuse wewe na wale wamakonde wako kibao wale ambao babu zao walikimbilia Brazil wakat wa buashara ya Utumwa kipich hichooo, Wanacheza mpira mgumu kama nn, Afu me syo kama Manure au Arsenal, nlikufuka kifo cha kawaida tu Etihad pale 2-1...

Teh Teh Teh!
Wamakonde wng wanatisha sn! Yani siku hiyo vile viberenge vyenu Au Pikipiki boxer zenu Coutinho na Rahim watapotea kabisa! Chezea Ivanovic na Azz?!!!! Teh Teh Teh!

Johnson na Flagan wajiandae kuwazuia akina Hazard na Willian Au Schurlle
 
hahahah..Ntuzu, huyo Hazard na mwenzake schurlle ile jmos Vs Crystal palace Mbona walikuwa wanakimbia kimbia tu uwanjani...???

RedCafu (Flanagan), Anawasubiri saaana, manake ndo sehem zake za kuchukulia sifa hizo...
 
Back
Top Bottom