Bilashaka siku inakwenda vyema
Pamoja na kwamba kwasasa kuna michuano mikubwa kabisa ya mchezo huu tunaoupenda lakini naona shauku, macho na masikio yetu tumeyaelekeza zaidi kwenda usajili wa timu yetu ya Liverpool.
Kuna kitu kimoja ambacho jamvi letu hapa la wanaliverpool limekifumbia macho. Sijui ni kutokana na hasira au labda ni kukosa namna ya kuanza kukiongelea. Au labda ni kukosa maneno sahihi ya kukiongelea. Kwa vyovyote vile ilivyo mimi naona kuna kila sababu ya kuliongelea swala hili.
Mnamo dakikia ya 79 ya mchezo kati ya Uruguay na Italy kuna kitendo kilitokea ambapo mcheza wa Uruguay, Luis Suarez alionekana kumngata mchezaji wa Italy, Giorgio Chiellini. Immediately, kamati ya maadili ya FIFA ilikaa, and within few days yalitoka maamuzi kwamba kamati hiyo imejiridhisha without no doubt kwamba Lui alimngata chiellini kwa makusudi!
Na kutokana na hilo basi Lui anafungiwa mechi 9 za kimataifa na kitendo bila kuchelewa, alitakiwa kuondoka kwenye kambi ya timu ya Taifa. Secondly, anafungiwa kucheza mpira kwa miezi minne (that means hataweza kucheza professional football until October 26). Thirdly, kwa kipindi hicho cha kufungiwa, hatoruhusiwa kufanya training to wachezaji wenzake wa Liverpool. Fourthly, wakati wa kifungo hatoruhusiwa kuingia big stadiums kuingalia timu yake ikicheza! Kama hiyo haitoshi, anatakiwa kulipa fined ya kiasi kisichozidi £66,000
Mataifa mengine wanaongelea kupitia vyombo vyao na ninajua kuna ambao hawataki hata kusikia kuhusu tukio hili lakini siyo vibaya tukaongelea the all scenario as JF Liverpool family. The magnificent; MosDef; Belo; Pazi; Janjaweed; Gwamahala; Black Kid; Ed n Edd nEddy; The Boss; Amanijua; reynod
na wengine
vipi, busara zenu zikoje kwenye hili?