Kuna hii ngonjera na propaganda ambayo imetawala vichwa vingi vya mashabiki wa mpira kuwa E.P.L ndiyo ligi ngumu zaidi duniani.
Kila siku huwa tunawapa facts huku kuwa England sio ligi ngumu bali timu zake zinakaribiana viwango watu wanakuwa wabishi hata unapowapa facts.
Bahati nzuri huu mwaka Timu ya Liverpool imekuwa katika kiwango bora na cha juu kushinda timu nyingine zote ndio tunaona sasa ukweli kuwa hii ligi huwa sio ngumu bali timu zinafanana viwango.
Tokea umeanza kushabikia mpira wa miguu ni mwaka gani ambao umeona katika Ligi 3 kubwa za ulaya ( La liga, Bundes liga na E.P.L )timu inayoongoza kwa pointi inaipita timu inayofuata kwa zaidi ya pointi 20 !!! Hata kule Serie A ambapo juve anachukua kwa miaka kama 7 mfululizo hili jambo ni nadra kutokea hata kwenye zile farmers leagues .
Je , hii Liverpool ndiyo timu bora kuwahi kutokea ulaya?
Jibu ni Hapana, Timu bora kuwahi kutokea ulaya katika karne ya 21, kwa maoni ya wengi ni ile Barcelona ya Pep Guardiola (2008-2011) ambayo ilisomba makombe yote unayojua ndani ya msimu mmoja, Hii timu na ubora wake wote haikuwahi kuongoza kwa pointi 20+ ...
Mashabiki wengi wa soka wakawa wanatoa kejeli eti Barcelona ile Pep ingepata tabu England, mi nikawa najiuliza kama Liverpool tuu hii ya kina Henderson, Wijnaldum , Milner inawatesa hivi ingekuja Barca ya ile ya kina Xavi na iniesta si isingefungwa kabisa hata misimu 3, maana katika timu hii ya Liverpool inayotesa sahizi ni wachezaji wawili tuu wangeweza kucheza ile Barcelona na wenyewe ni beki kisiki VVD na kipa wao Allison baasi, wengine kama captain wao Henderson hata benchi asingekaa.
Sasa iweje Liverpool ambayo tunaambiwa iko kwenye ligi ngumu zaidi ulaya iongoze kwa pointi 20+ kitu ambacho hata hakitokeagi kwenye ligi ya ureno ?
Mashabiki wa England sijui mtakuja na utetezi gani !!
Yaani tofauti ya pointi kati ya wa 1 na wa 4 ni pointi 32[emoji23][emoji23][emoji23], Halafu unaambiwa hiyo ndiyo ligi ngumu zaidi Duniani
Liverpool imeiumbua E.P.L....aibuuuuu
View attachment 1344079View attachment 1344081View attachment 1344086
Sent using
Jamii Forums mobile app