goroko77
JF-Expert Member
- Jul 9, 2019
- 8,845
- 13,072
Hbr za muda huu
Niko Hapa natazama Bunge la 12 mkutano wa saba , kikao Cha la kumi na moja , mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chini ya Waziri Jenister Muhaghama
Alipewa nafasi bwana Lusinde kuchangia katika mjadala unaoendelea badala ya kujikita katika hoja iliyopo mezani yeye amebaki kumtetea Hayati Magufuli na kusema kuwa ndugu Zitto aache upuuzi wake wa kumsema marehemu Magufuli kwani marehemu hasemwi na kumtaka kufuta kauli yake ya kusema wanaopenda sana Magufuli wakazikwe nae huko Chato, alisisitiza Sana kwa jazba bila hofu
Wakati jamaa anachangia hoja zake Bunge lilikaa kimya sana hakuna aliyempenyeza taarifa wala Mwenyekiti wa Bunge hakutoa neno la kumtaarifu ndugu Lusinde kujikita ktk hoja na kuachana Mambo ya kumjadili mtu pale jamaa alipewa muda kutoa yake ya moyoni na kumtaka ndugu Zitto kuomba msamaha kwa Mama Janeth Magufuli na familia yake kwa udhalilishaji anaoufanya.
Niliona kabisa kuwa jamaa anampenda sana Hayati Magufuli na yeye amesema wasi kabisa kuwa yeye anampenda na aachwe na Zitto afundishwe adabu. Lusinde anaongea as if kwamba hajui kuwa ktk kipindi cha Hayati Magufuli alitumika kuwatukana viongozi walioko sasa hivi madarakani haswa wa chama jamaa anaongea kwa kujiamini Sana na kutokujali
Asilimia 80 mpaka 90 ya Wabunge na Mawaziri wanamkubali sana Hayati Magufuli hata Jenister ni Magufuli forevermore yule.
Pia soma > Zitto: Wanaompenda Magufuli wakazikwe naye Chato, alikuwa Rais fisadi zaidi kuwahi kutokea Tanzania