Livingstone Lusinde, japo ni darasa la saba tuu, ni kichwa mbaya!, ana uwezo mkubwa na pia ana powers fulani!.

Livingstone Lusinde, japo ni darasa la saba tuu, ni kichwa mbaya!, ana uwezo mkubwa na pia ana powers fulani!.

Sasa pascal hiyo ni historia ya maisha mbn umempamba ata ana uwezo mkubwa me nlijua utaongelea national issues kujenga hoja au vitu constructive
Jambo la maana analoweza kujiuliza huyo Lusinde ni: ''Je, background yake imemsaidia kuwa mbunge bora anayetetea maelefu ya maskini wanaoishi kama yeye alivyoishi ukitilia maanani ana expirience ya hayo maisha? Jibu ni HAPANA. Baada ya kupanda amewasahau walio kwenye maisha ya umaskini. Sijawahi kumwona wala kumsikia akipigania maskini wa Tanzania kama mbunge! Hili linafanya hiyo historia yake ya maisha isiwe na maana yoyote!
 
Mkuu Pascal na wanajukwaa,binafsi nakubali kwamba huyu kibajaji ana uwezo wa kujenga hoja hasa kwa masuala anayokuwa na uelewa nayo.Jambo nisilokubaliana naye ni kuwa na mdomo mchafu.Ni huyuhuyu kibajaji ametumika mara nyingi kuzima hoja zenye maslahi ya umma pale bungeni tena kwa maneno ya shombo na kejeli.Hata wakati wa bunge maalum la katiba huyu alikuwa miongoni mwa wachache waliojivika miwani ya mbao na kupinga vipengele ambavyo vilikuwa na umuhimu wa kubadilishwa kwenye katiba kama madaraka makubwa ya rais.Ni huyuhuyu CCM wanamtumia sana kwenye mikutano ya kampeni kutukana wapinzani akitumia lugha za kejeli hata Kinondoni ameonekana kwenye majukwaa lakini nenda jimboni kwake hali ni mbaya.Kwa taarifa yako jimbo la Mtera analoongoza linaweza kuwa miongoni mwa majimbo yenye wananchi masikini wa kutupwa lakini yeye kutwa ni kuitetea serikali ya CCM na kusafiri kwenda kuwapigia kampeni wagombea wa CCM maeneo mengine.Nguvu anazotumia kuwananga na kuwatusi upinzani angezitumia kidogo tu jimboni kwake umasikini ungepungua kwa kiasi kikubwa.Vipo vijiji kule kwake mfano Igandu,Ndebwe ambako wananchi wanafuata maji hadi umbali wa zaidi ya kilometa 10 lakini yeye kazi kutetea serikali ya chama chake utafikiri yeye ni waziri asiye na wizara maalum.Kazi ya kuisimamia na kuikososoa serikali kwake haipo na kwa taarifa tu,2020 ajiandae kupumzika maana Prof Kabudi anakwenda jimboni na kwa elimu yake ya darasa la tatu labda akagombee udiwani kwa sababu Ukuu wa wilaya na mkoa anatakiwa angalau awe na shahada.
Binafsi simpendi kabisa Kibajaji ila huwezi kumng'oa Kibajaji kwa gia ya usomi wa huyo Profesa Kabudi, hiyo ni moja ya sababu iliyomngowa mzee Malecela.

Kwenye kura za maoni Kibajaji aliwauliza wapiga kura kuna mwenye degree wapiga kura kimya, kuna mwenye diploma wapiga kura kimya, kuna form six wote kimya kuna form wote kimyaa, akawaambia sasa nyinyi darasa la saba mimi ndio mwenzenu dalasa la saba mwenzenu, kupigwa kura tingatinga chali.

Kabudi aingie jimbo hilo kwa gia nyingine na siyo usomi ataduwazwa na hatoamini macho yake.
 
Muongo sana huyo. Leo anasema alipelekwa dar na mama fulani kwaajili ya kubeba mizigo, kuna siku alisema alipelekwa dar na rafiki yake kuuza kahawa. Ni muongo wa kutupwa, hapo mwisho wa yote utasikia atakavyojisifu kuwa ana V8 mbili, moja anatumia yeye nyingine mkewe.
Watanzania wengi waliopata mafanikio kwa kutokea kwenye maisha ya chini wana tabia ya ku-exaggarate na kuongopa kuhusu maisha yao ya nyuma baada ya kupata mafanikio. Kama mtu alikuwa anakunywa chai ya rangi atasema alikuwa anakaa siku saba bila kula!
 
Maisha hayana formula.
Hii ndiyo kanuni ya Poise .

Japo, kamwe hatutafanana njia za mafanikio ndiyo maana maisha yanakosa formula katika kutoka kimaisha.
 
Binafsi simpendi kabisa Kibajaji ila huwezi kumng'oa Kibajaji kwa gia ya usomi wa huyo Profesa Kabudi, hiyo ni moja ya sababu iliyomngowa mzee Malecela.

Kwenye kura za maoni Kibajaji aliwauliza wapiga kura kuna mwenye degree wapiga kura kimya, kuna mwenye diploma wapiga kura kimya, kuna form six wote kimya kuna form wote kimyaa, akawaambia sasa nyinyi darasa la saba mimi ndio mwenzenu dalasa la saba mwenzenu, kupigwa kura tingatinga chali.

Kabudi aingie jimbo hilo hilo kwa nyingine na siyo usomi ataduwazwa na hatoamini macho yake.
Hili ndio tatizo la wapiga kura wa maeneo hayo. Hawajielewi na hawajitambui!
 
kama ni drs la vii,hamna kitu,na bungen anapitisha asichokijua.Nimaneno naporojo nyingi do zinamfanya aonekane mjuaji.
 
Karne ya 21 kushabikia Darasa la 3 ni upungufu wa madini kichwani!!

Hizo ni bahati tu.... Bahati ya mwenzio usilalie mlango wazi!!

Mbona matajiri wengi hii Tz ni std 7, akina Mwita Gachuma, nk. Hii haimaanishi wasomi hawana maana!! Thubutu!!

Pia hawa std 3, 4 & 7 wengi walikuwa Majambazi. Ila mtu akisha toka ata anza kusimulia ONLY the POSITIVE side.

Mf...Masanja ana hela tu nzr na sasa ni mchungaji. Mfuate sasa akusimulie, historia yake ya Maisha! Movie yake utaipenda ni zaidi ya KIKOREA.

Ww kama Mwandishi ulipaswa uchunguze kwanza kabla ya kuulisha umma na kuaminisha umma kuwa Elimu si chochote!!

Hii nchi inaendeshwa kisomi, ndio maana ipo!!
 
Maisha ni safari ndefu haijalishi una elimu au huna elimu ili mradi tu ufikie mafanikio ya malengo yako ya maisha duniani.
 
Luside huyu huyu
Huyu huyu aliyewashawishi watu wake wa Mtera kuwa wale watafiti kutoka Arusha kuwa ni wanyonya damu wakawaua na kuwachoma moto. Ndiyo huyu anayesema Paskali Mayalla kuwa ana IQ ya juu sana kiasi anafaa kuwa wa kuigwa.
Namshauri Paskali aende kwenye vijiwe atakutana na waswahili wanauelezea mpira na mbinu zake kuliko Wenger kiasi unajiuliza jee kwa nini Arsenal wasimchukue huyu na kumfukuzilia mbali Wenger!
 
Livingstone bado ana nguvu na uwezo wa kifedha kujiendeleza kieleimu. Kama kweli na IQ kubwa na hamu ya elimu kwa nini sasa asijiendeleze? Eric Shigongo alipotambua kuwa ana uwezo wa akili na kifedha ameenda shuleni. Yeye nini kinamzuia kwenda shuleni tuone hiyo IQ yake? Huyu mtu ana maneno mengi sana na anataka kuaminisha umma wa vijana wa Tanzania elimu ya darasani si kitu cha muhimu sana.Watu kama hawa wanaweza kuonekana wa maana kwenye nchi chache, lakini mwisho wao ni mwanguko mmbaya- anagalia Jacob Zuma, kwa mfano
Mkuu yeye ameishamaliza kusoma na mafanikio yake ni hayo kutoka machinga hadi ubunge tena wa Jamhuri katika chama cha CCM,ameoa,ana mali nyingi,alimuangusha kirahisi Waziri Mkuu mstaafu Mzee Malicela,kwenye kura za maoni tu.
 
Umeongea ukweli una uwezo mkubwa sana wa kupambanua mambo na kujenga na kuwasilisha hoja kwa lugha inayoeleweka...ni moja kati ya asset za chama tena yule alipaswa kuwa katibu mwenezi wa chama
Unamchongea, chakubanga atamroga sasa hivi.
 
Watanzania wengi wenye miaka 30+ au 35+ wametokea ktk mazingira magumu sana.
Wengi wamepambana sana kufanikiwa.

Wala haiana haja ya kumsifia sana, wengi tumetokea huko japo vikwazo vimetofautiana kidogo.

Pia wanasiasa wengi wanataka waonewe huruma.
Kichwa mtu ambae hathamini elimu na watu walio soma? Mfano alisema ama mshangaa Professor anaetaka kupima udongo wa shamba lake wakati yeye amelima hapo kwa miaka mitatu bila shida, huyu mtu hana uelewa mkubwa kiukweli.

Kwa mfano tu huo wa kupima udongo, yeye anaamini aridhi anayo lima itaendelea kuwa na rutuba miaka yote tu au ata liacha shamba na kulima sehemu nyingine na hajui kama atakuwa anafanya uharibifu wa mazingira.
 
Huyu huyu aliyewashawishi watu wake wa Mtera kuwa wale watafiti kutoka Arusha kuwa ni wanyonya damu wakawaua na kuwachoma moto. Ndiyo huyu anayesema Paskali Mayalla kuwa ana IQ ya juu sana kiasi anafaa kuwa wa kuigwa.
Namshauri Paskali aende kwenye vijiwe atakutana na waswahili wanauelezea mpira na mbinu zake kuliko Wenger kiasi unajiuliza jee kwa nini Arsenal wasimchukue huyu na kumfukuzilia mbali Wenger!
Chakaza asante sana mpaka nimecheka wakati nina maumivu! Haya ndio maisha yetu halisi ya Bongo! Maneno na wenye maneno ndio wanathaminiwa kuliko matendo na wenye vitendo! Na mbaya zaidi ndio waliojaa kwenye siasa ambayo ndiyo inaongoza kila kitu.
 
Huyo hana uwezo wowote domo tu..bongo ukiwa na domo ndo utaishi sio smart head ya kufanya world changers decisions
 
INFACT ANATAIWA KUWA WAZIRI WA ELIMU AU SHERIA KAMA WABUNGE WALIVYOOMBA...NAAMINI MH MAGUFURI ATACHUKUA MAPENDEKEZO YA WABUNGE HAO NASISI NA WEWE TUTA MUUNGA MKONO.
Lusinde kuwa wazir wa wizara yeyote ile ni Joke hata unaibu ni mashaka...
 
Paskali hyo kibajaj ni zero kabisa tatizo humjui vizri
Mkuu Mgoloko, yes anaweza kuwa zero, pia ni kweli simjui vizuri, bali nimemsikiliza leo historia yake, alipotoka na mahali alipo sasa, wengi watakubaliana na mimi, kuwa, this man is genius!. Yes ni mropokaji na mpayukaji, hiki ndicho Watanzania wanachokitaka!.

Kipimo cha maendeleo ya kweli ni mafanikio na changing life style na doo vyeti mtu alivyohitimu. Huyu jamaa is a big success!. Being a school dropout, toka kuuza kahawa hadi kuwa mtungasheria, sio kitu kidogo!.
P
 
Jamaa amemaliza, kiukweli huyu Jamaa ni very interesting person, ana kipaji cha juu sana cha kujieleza, pia ana powers fulani za success. Kuna watu wameacha shule, au kuishia darasa la saba kutokana na mahangaiko tuu ya maisha lakini wana I.Q kubwa. Huyu Jamaa ana I.Q kubwa sana, angesoma elimu ya darasani, angekuwa profesa!, uthibitisho wa I.Q hiyo, ni kupitia kwa Binti yake aitwae Penina, yuko kwenye top 5 ya vichwa mkoa wa mzima wa Dodoma!.

Hongera sana Mhe. Livingstone Lusinde, kuna kitu najifunza kwako!.

Asanteni kufuatilia.

Paskali
Huyo ana tofauti ndogo na Joseph kibwetele! Ingekuwa serikali nyingine muda huu angekuwa jela alisababisha hasara kwa serikali baada ya gari kuchomwa moto na watumishi kuuawa halafu unasema ana IQ kubwa Paskali umechanganyikiwa nini?
 
Back
Top Bottom