macho_mdiliko
Platinum Member
- Mar 10, 2008
- 25,191
- 48,765
Jambo la maana analoweza kujiuliza huyo Lusinde ni: ''Je, background yake imemsaidia kuwa mbunge bora anayetetea maelefu ya maskini wanaoishi kama yeye alivyoishi ukitilia maanani ana expirience ya hayo maisha? Jibu ni HAPANA. Baada ya kupanda amewasahau walio kwenye maisha ya umaskini. Sijawahi kumwona wala kumsikia akipigania maskini wa Tanzania kama mbunge! Hili linafanya hiyo historia yake ya maisha isiwe na maana yoyote!Sasa pascal hiyo ni historia ya maisha mbn umempamba ata ana uwezo mkubwa me nlijua utaongelea national issues kujenga hoja au vitu constructive
Binafsi simpendi kabisa Kibajaji ila huwezi kumng'oa Kibajaji kwa gia ya usomi wa huyo Profesa Kabudi, hiyo ni moja ya sababu iliyomngowa mzee Malecela.Mkuu Pascal na wanajukwaa,binafsi nakubali kwamba huyu kibajaji ana uwezo wa kujenga hoja hasa kwa masuala anayokuwa na uelewa nayo.Jambo nisilokubaliana naye ni kuwa na mdomo mchafu.Ni huyuhuyu kibajaji ametumika mara nyingi kuzima hoja zenye maslahi ya umma pale bungeni tena kwa maneno ya shombo na kejeli.Hata wakati wa bunge maalum la katiba huyu alikuwa miongoni mwa wachache waliojivika miwani ya mbao na kupinga vipengele ambavyo vilikuwa na umuhimu wa kubadilishwa kwenye katiba kama madaraka makubwa ya rais.Ni huyuhuyu CCM wanamtumia sana kwenye mikutano ya kampeni kutukana wapinzani akitumia lugha za kejeli hata Kinondoni ameonekana kwenye majukwaa lakini nenda jimboni kwake hali ni mbaya.Kwa taarifa yako jimbo la Mtera analoongoza linaweza kuwa miongoni mwa majimbo yenye wananchi masikini wa kutupwa lakini yeye kutwa ni kuitetea serikali ya CCM na kusafiri kwenda kuwapigia kampeni wagombea wa CCM maeneo mengine.Nguvu anazotumia kuwananga na kuwatusi upinzani angezitumia kidogo tu jimboni kwake umasikini ungepungua kwa kiasi kikubwa.Vipo vijiji kule kwake mfano Igandu,Ndebwe ambako wananchi wanafuata maji hadi umbali wa zaidi ya kilometa 10 lakini yeye kazi kutetea serikali ya chama chake utafikiri yeye ni waziri asiye na wizara maalum.Kazi ya kuisimamia na kuikososoa serikali kwake haipo na kwa taarifa tu,2020 ajiandae kupumzika maana Prof Kabudi anakwenda jimboni na kwa elimu yake ya darasa la tatu labda akagombee udiwani kwa sababu Ukuu wa wilaya na mkoa anatakiwa angalau awe na shahada.
Watanzania wengi waliopata mafanikio kwa kutokea kwenye maisha ya chini wana tabia ya ku-exaggarate na kuongopa kuhusu maisha yao ya nyuma baada ya kupata mafanikio. Kama mtu alikuwa anakunywa chai ya rangi atasema alikuwa anakaa siku saba bila kula!Muongo sana huyo. Leo anasema alipelekwa dar na mama fulani kwaajili ya kubeba mizigo, kuna siku alisema alipelekwa dar na rafiki yake kuuza kahawa. Ni muongo wa kutupwa, hapo mwisho wa yote utasikia atakavyojisifu kuwa ana V8 mbili, moja anatumia yeye nyingine mkewe.
Hili ndio tatizo la wapiga kura wa maeneo hayo. Hawajielewi na hawajitambui!Binafsi simpendi kabisa Kibajaji ila huwezi kumng'oa Kibajaji kwa gia ya usomi wa huyo Profesa Kabudi, hiyo ni moja ya sababu iliyomngowa mzee Malecela.
Kwenye kura za maoni Kibajaji aliwauliza wapiga kura kuna mwenye degree wapiga kura kimya, kuna mwenye diploma wapiga kura kimya, kuna form six wote kimya kuna form wote kimyaa, akawaambia sasa nyinyi darasa la saba mimi ndio mwenzenu dalasa la saba mwenzenu, kupigwa kura tingatinga chali.
Kabudi aingie jimbo hilo hilo kwa nyingine na siyo usomi ataduwazwa na hatoamini macho yake.
Ni hili ndio tatizo lake kubwa. Historia yake haina maana yoyote kwani hana rekodi ya kupigania wanyonge.Anaweza akawa timamu na iq kubwa lakini tatizo ni pale wanapokuwa na uchungu zaidi na ccm kuliko mama TANZANIA
Huyu huyu aliyewashawishi watu wake wa Mtera kuwa wale watafiti kutoka Arusha kuwa ni wanyonya damu wakawaua na kuwachoma moto. Ndiyo huyu anayesema Paskali Mayalla kuwa ana IQ ya juu sana kiasi anafaa kuwa wa kuigwa.Luside huyu huyu
Mkuu yeye ameishamaliza kusoma na mafanikio yake ni hayo kutoka machinga hadi ubunge tena wa Jamhuri katika chama cha CCM,ameoa,ana mali nyingi,alimuangusha kirahisi Waziri Mkuu mstaafu Mzee Malicela,kwenye kura za maoni tu.Livingstone bado ana nguvu na uwezo wa kifedha kujiendeleza kieleimu. Kama kweli na IQ kubwa na hamu ya elimu kwa nini sasa asijiendeleze? Eric Shigongo alipotambua kuwa ana uwezo wa akili na kifedha ameenda shuleni. Yeye nini kinamzuia kwenda shuleni tuone hiyo IQ yake? Huyu mtu ana maneno mengi sana na anataka kuaminisha umma wa vijana wa Tanzania elimu ya darasani si kitu cha muhimu sana.Watu kama hawa wanaweza kuonekana wa maana kwenye nchi chache, lakini mwisho wao ni mwanguko mmbaya- anagalia Jacob Zuma, kwa mfano
Unamchongea, chakubanga atamroga sasa hivi.Umeongea ukweli una uwezo mkubwa sana wa kupambanua mambo na kujenga na kuwasilisha hoja kwa lugha inayoeleweka...ni moja kati ya asset za chama tena yule alipaswa kuwa katibu mwenezi wa chama
Chakaza asante sana mpaka nimecheka wakati nina maumivu! Haya ndio maisha yetu halisi ya Bongo! Maneno na wenye maneno ndio wanathaminiwa kuliko matendo na wenye vitendo! Na mbaya zaidi ndio waliojaa kwenye siasa ambayo ndiyo inaongoza kila kitu.Huyu huyu aliyewashawishi watu wake wa Mtera kuwa wale watafiti kutoka Arusha kuwa ni wanyonya damu wakawaua na kuwachoma moto. Ndiyo huyu anayesema Paskali Mayalla kuwa ana IQ ya juu sana kiasi anafaa kuwa wa kuigwa.
Namshauri Paskali aende kwenye vijiwe atakutana na waswahili wanauelezea mpira na mbinu zake kuliko Wenger kiasi unajiuliza jee kwa nini Arsenal wasimchukue huyu na kumfukuzilia mbali Wenger!
Lusinde kuwa wazir wa wizara yeyote ile ni Joke hata unaibu ni mashaka...INFACT ANATAIWA KUWA WAZIRI WA ELIMU AU SHERIA KAMA WABUNGE WALIVYOOMBA...NAAMINI MH MAGUFURI ATACHUKUA MAPENDEKEZO YA WABUNGE HAO NASISI NA WEWE TUTA MUUNGA MKONO.
Mkuu Mgoloko, yes anaweza kuwa zero, pia ni kweli simjui vizuri, bali nimemsikiliza leo historia yake, alipotoka na mahali alipo sasa, wengi watakubaliana na mimi, kuwa, this man is genius!. Yes ni mropokaji na mpayukaji, hiki ndicho Watanzania wanachokitaka!.Paskali hyo kibajaj ni zero kabisa tatizo humjui vizri
Huyo ana tofauti ndogo na Joseph kibwetele! Ingekuwa serikali nyingine muda huu angekuwa jela alisababisha hasara kwa serikali baada ya gari kuchomwa moto na watumishi kuuawa halafu unasema ana IQ kubwa Paskali umechanganyikiwa nini?Jamaa amemaliza, kiukweli huyu Jamaa ni very interesting person, ana kipaji cha juu sana cha kujieleza, pia ana powers fulani za success. Kuna watu wameacha shule, au kuishia darasa la saba kutokana na mahangaiko tuu ya maisha lakini wana I.Q kubwa. Huyu Jamaa ana I.Q kubwa sana, angesoma elimu ya darasani, angekuwa profesa!, uthibitisho wa I.Q hiyo, ni kupitia kwa Binti yake aitwae Penina, yuko kwenye top 5 ya vichwa mkoa wa mzima wa Dodoma!.
Hongera sana Mhe. Livingstone Lusinde, kuna kitu najifunza kwako!.
Asanteni kufuatilia.
Paskali