Livingstone Lusinde, japo ni darasa la saba tuu, ni kichwa mbaya!, ana uwezo mkubwa na pia ana powers fulani!.

Livingstone Lusinde, japo ni darasa la saba tuu, ni kichwa mbaya!, ana uwezo mkubwa na pia ana powers fulani!.

Mkewe Edna kaishia darasa la nne, yeye aliishia darasa la 3, hivyo wakichanganya ndio inakuwa darasa la saba. Amesema jambo moja la muhimu sana, yeye na mkewe wana elimu kubwa sana isiyo rasmi. Kama serikali ingetumia mbinu za kuitap hii elimu isiyo rasmi ya Watanzania wasio na elimu ya darasani, wanaweza kufanya mambo makubwa, kuliko ma profesa wenye elimu za kwenye makaratasi!.

P.

Livingstone bado ana nguvu na uwezo wa kifedha kujiendeleza kieleimu. Kama kweli na IQ kubwa na hamu ya elimu kwa nini sasa asijiendeleze? Eric Shigongo alipotambua kuwa ana uwezo wa akili na kifedha ameenda shuleni. Yeye nini kinamzuia kwenda shuleni tuone hiyo IQ yake? Huyu mtu ana maneno mengi sana na anataka kuaminisha umma wa vijana wa Tanzania elimu ya darasani si kitu cha muhimu sana.Watu kama hawa wanaweza kuonekana wa maana kwenye nchi chache, lakini mwisho wao ni mwanguko mmbaya- anagalia Jacob Zuma, kwa mfano
 
Le Mutuz naye anadanganya alikuwa analala stand ya bus New York, hawa watu wa Mtera ni waongo sana.
Naona broo wetu kadumbukia kabisa kwenye T.V na kichwa na miguu , hizi ni kama zile drama za Msukuma, alijielezaaga wakati watu wanajuaga maujanja yake wametulia tu.
 
Hakuna neno la Mjinga lisilo na Faida kwa mwerevu.........................

Kibajaji ni mjinga!
 
Livingstone bado ana nguvu na uwezo wa kifedha kujiendeleza kieleimu. Kama kweli na IQ kubwa na hamu ya elimu kwa nini sasa asijiendeleze? Eric Shigongo alipotambua kuwa ana uwezo wa akili na kifedha ameenda shuleni. Yeye nini kinamzuia kwenda shuleni tuone hiyo IQ yake? Huyu mtu ana maneno mengi sana na anataka kuaminisha umma wa vijana wa Tanzania elimu ya darasani si kitu cha muhimu sana.Watu kama hawa wanaweza kuonekana wa maana kwenye nchi chache, lakini mwisho wao ni mwanguko mmbaya- anagalia Jacob Zuma, kwa mfano
Kweli kabisa mkuu.
 
Jamaa amemaliza, kiukweli huyu Jamaa ni very interesting person, ana kipaji cha juu sana cha kujieleza, pia ana powers fulani za success. Kuna watu wameacha shule, au kuishia darasa la saba kutokana na mahangaiko tuu ya maisha lakini wana I.Q kubwa. Huyu Jamaa ana I.Q kubwa sana, angesoma elimu ya darasani, angekuwa profesa!, uthibitisho wa I.Q hiyo, ni kupitia kwa Binti yake aitwae Penina, yuko kwenye top 5 ya vichwa mkoa wa mzima wa Dodoma!.

Hongera sana Mhe. Livingstone Lusinde, kuna kitu najifunza kwako!.

Asanteni kufuatilia.

Paskali
Ukitazama kijana ambaye anemaliza darasa la saba, akaingia garage kama saidia fundi, akakaa kwa miaka 20, akiwa garage, halafu umlete kijana ametoka chuo kikuu kasoma automotive,
Nisaidie kupata majibu. Nani zaidi
Practically!!!
 
Ukiniambia leo hii nichague kati ya Dr. Hassan Abbas ( Msemaji wa Serikali mwenye Elimu ya Darasani na ya Kutukuka kabisa ) na Livingstone Lusinde ( Mbunge wa JMT jimbo la Mtera mwenye Elimu ya wasiwasi na duni iliyojaa Milima na Mabonde ) nani kati yao naona ana uwezo mkubwa wa akili, uthubutu, kujiamini na ushawishi mkubwa katika Jamii na ambaye kiukweli hakuletwa hapa duniani kwa bahati mbaya tu bali Mwenyezi Mungu alikuwa na ' makusudi ' yake bila Kupepesa macho, Kutikisa masikio na Kumung'unya maneno haraka na upesi sana nitamchagua Mbunge Livingstone Lusinde ( Kibajaji )
 
Nimeangalia hicho kipindi,kuna jambo kubwa sana la kujifunza,kuna haja ya kubadili mentalit kuhusu watu wasiopata nafasi ya kukaa darasi haina maana hawana akili,wasomi wengi hujijengea atittude ya academic arrogant(ce) na wanaishia hapo tu....mifano iko mingi kwa watu waliofika mbali na wana elimu duni....
 
Sasa paskali mbona unamuaibisha hadharani,sisi wengine hatukujua kama ni std seven,pamoja na sifa zote bado ana huo upungufu wa kukosa elimu,hawezi kudadavua yanapokuja mambo yanayohitaji skuli
sio std seven ni std3 yani aliishia pale kwenye kujifunza habari za mr and mrs Daudi....hakupata nafasi hata ya kujua habari za kipeuo cha kwanza na cha pili hahahaaa
 
Mkuu Pascal na wanajukwaa,binafsi nakubali kwamba huyu kibajaji ana uwezo wa kujenga hoja hasa kwa masuala anayokuwa na uelewa nayo.Jambo nisilokubaliana naye ni kuwa na mdomo mchafu.

Ni huyuhuyu kibajaji ametumika mara nyingi kuzima hoja zenye maslahi ya umma pale bungeni tena kwa maneno ya shombo na kejeli.Hata wakati wa bunge maalum la katiba huyu alikuwa miongoni mwa wachache waliojivika miwani ya mbao na kupinga vipengele ambavyo vilikuwa na umuhimu wa kubadilishwa kwenye katiba kama madaraka makubwa ya rais.Ni huyuhuyu CCM wanamtumia sana kwenye mikutano ya kampeni kutukana wapinzani akitumia lugha za kejeli hata Kinondoni ameonekana kwenye majukwaa lakini nenda jimboni kwake hali ni mbaya.

Kwa taarifa yako jimbo la Mtera analoongoza linaweza kuwa miongoni mwa majimbo yenye wananchi masikini wa kutupwa lakini yeye kutwa ni kuitetea serikali ya CCM na kusafiri kwenda kuwapigia kampeni wagombea wa CCM maeneo mengine.Nguvu anazotumia kuwananga na kuwatusi upinzani angezitumia kidogo tu jimboni kwake umasikini ungepungua kwa kiasi kikubwa.

Vipo vijiji kule kwake mfano Igandu,Ndebwe ambako wananchi wanafuata maji hadi umbali wa zaidi ya kilometa 10 lakini yeye kazi kutetea serikali ya chama chake utafikiri yeye ni waziri asiye na wizara maalum.

Kazi ya kuisimamia na kuikososoa serikali kwake haipo na kwa taarifa tu,2020 ajiandae kupumzika maana Prof Kabudi anakwenda jimboni na kwa elimu yake ya darasa la tatu labda akagombee udiwani kwa sababu Ukuu wa wilaya na mkoa anatakiwa angalau awe na shahada.
 
Mkewe Edna kaishia darasa la nne, yeye aliishia darasa la 3, hivyo wakichanganya ndio inakuwa darasa la saba. Amesema jambo moja la muhimu sana, yeye na mkewe wana elimu kubwa sana isiyo rasmi. Kama serikali ingetumia mbinu za kuitap hii elimu isiyo rasmi ya Watanzania wasio na elimu ya darasani, wanaweza kufanya mambo makubwa, kuliko ma profesa wenye elimu za kwenye makaratasi!.

P.
Saa nyingine kuna kitu kinaitwa bahati kaka asichanganye bahati ambayo siyo wengi wanaipata na jitihada ya mtu. Watoto wa mjini wanaita zali
Kuna watu wamejihangaisha kupita yeye lakini bado hata kusimama hamna. Ni vijana wangapi wa kimachinga wana struggle?
Angekuwa na akili angejiendeleza kwani ana fursa nzuri ya kijiendeleza sana sana ni bingwa wa matusi
 
Nimeangalia hicho kipindi,kuna jambo kubwa sana la kujifunza,kuna haja ya kubadili mentalit kuhusu watu wasiopata nafasi ya kukaa darasi haina maana hawana akili,wasomi wengi hujijengea atittude ya academic arrogant(ce) na wanaishia hapo tu....mifano iko mingi kwa watu waliofika mbali na wana elimu duni....
Nafas si ameipata ya UBUNGE
 
Anaweza akawa timamu na iq kubwa lakini tatizo ni pale wanapokuwa na uchungu zaidi na ccm kuliko mama TANZANIA
 
Back
Top Bottom