Liwale: Kijana anatafutwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za mauaji ya mke wa mtu

Inasikitisha sana, walikua na yao mpaka kuuwana...
 
Polisi Lindi wanamtafuta Saidi Haji Ngamila (30) wa Kijiji cha Barikiwa Wilaya ya Liwale kwa tuhuma za kumuua Mke wa Mtu (Mwajuma Ally Lipala miaka 49 ) ambaye alikua Mchepuko wake kwa kumkata na kitu chenye ncha kali na kutengenganisha kichwa na kiwiliwili na kisha kuchimba shimo na kumfukia.

Mume wa marehemu Rashid Ally Mkumba (69) amesema Aprili 14,2022 yeye na Mkewe walikwenda kwenye shamba lao la mahindi na mihogo kwa ajili ya ujenzi wa kibanda cha kulinda wanyama waharibifu lakini wakati anaendelea na ujenzi Marehemu alimuaga kuwa anakwenda kukata nyasi za kuezekea kibanda lakini hakurudi tena.

Baada ya kutorejea kwa Mke wake, Rashid alikwenda kutoa taarifa kwa uongozi wa kijiji ambapo juhudi za kumtafuta zilianza na ilipofika Aprili 16,2022 mwili wake uligundulika kufukiwa pembeni mwa nyumba ya Mtuhumiwa Saidi Haji Ngamila ambapo Kamanda wa Polisi Lindi Mtatiro Kitinkwi amesema uchunguzi wa awali umeonesha wawili hao walikuwa Wapenzi.

Kamanda Kitinkwi pia amesema polisi kwa kushirikiana na ndugu wa Marehemu waliikuta mundu ya kukatia nyasi aliyokuwa anaitumia Marehemu siku aliyotoweka na viatu alivyovaa mara ya mwisho vilikuwa nyumbani kwa Mtuhumiwa.
 
Duuh🙄
Dhambi inaua!
 
Duh wananzengo wa Liwale mmekuaje tena ata kanda maalum wanashangaa?
 
49-30=19! Nani zaidi?
Kwa mume umri wa babake, kwa hawara umri wa mwanaye!

Kwa hiyo tuseme, alikuwa akilelewa na wakati huo akilea kimapenzi.

Nyumbani akibembelezwa kwa udogo wake, kwa hawara anaenda kubembeleza ki ben10 chake.

Movie kaiharibu huyo dogo kuua!
 
Back
Top Bottom