Alipokamatwa nilisema there was a 'fault charge sheet ab initio' yaani kosa la msingi katika kuandaa shitaka hili tangu mwanzo. Kitu muhimu kwangu sio Liyumba kuwa is clean, bali haki zao za msingi kwenye kosa wanaloshitakiwa nalo ambalo sio kosa kweli.
Niliposema hayo, nilishutumiwa sana na kuitwa fisadi. Niliyoyasema sasa yanaanza kutimia, bado kina Mramba pia kesi itatupwa!.
Kwa kina Liyumba ilihitaji tuu simple logic, majengo pacha yalipitishiwa budget ya awali kugharimu bilioni 90. Kazi ilipoanza gharama zikaongezeka mpaka zilipofikia.
Walipowashitaki, wamewashitaki kwa gharama zote tangu mwanzo na sio zile za zida tuu.
Nikasema, angetokea mwanasheria makini, akatafuta hizo fedha zote za thamani ya majengo pacha, serikali ikarudishiwa na majengo pacha yakageuka mali ya Liyumba!.
Kosa la msingi ni kuwashitaki wakina Liyumba kusababisha hasara ya thamani ya kazi iliyofanyika na majengo yanaonekana, huku madai yakionyesha yote ni haswara tupu as if hakuna kilichofanyika.
Usahihi wa madai ya serikali ungekuwa kama ifuatavyo.
1. Kwanza angetafutwa mthamini kuyathamini hayo majengo yametua gharama halisi za kiasi gani.
2. Baada ya kupata gharama halisi, unatoa zile gharama zilizolipiwa.
3. Tofauti ya gharama halisi na kilicholipiwa ndio hasara/10% ama ulaji.
Kesi inge-base hapo angalau ingekuwa kesi ya ukweli.
Na wakiachiwa kama wakili wao mzuri, waifungulia serikali kesi na wanalipwa fidia.
Nilisema PCCB wana kiherehere cha kufungua kesi kwa papara ili kurudisha imani ya wananchi kwa serikali yao ambayo ilishuka sana.
Hii serikali yetu ni ya ajabu sana, wakati wa rada, kelele zikapigwa ni ya kijeshi na haina maslahi kwa taifa. serikali ilitia pamba masikioni. leo rada haifanyi kazi, pesa zimeliwa na taifa limekula hasara.
Hata huko kumtafuta Vithlani sio kwa kesi ya bei ya rada ambayo tumelizwa, bali kwa kutosema ukweli kwa PCCB.
Ndege ya rais watu wamepiga kelele, Bwana Mapesa, John Cheyo akatoa mpaka ushahidi wa website gharama ya ndege ni nusu ya bei tunayotaka kuuziwa. Serikali ilitia pamba masikioni na kuendeleza manunuzi, ajenti ni huyo huyo Vithlani na Somaiya wake.
Deal ya rada imebumbuluka kwa sababu BAE shirika la serikali na walioibumbulua ni waingereza wenyewe kupitia SFO. Ya Gulf Sream ni kimya...ulaji wa kiulaini.
"Hii ndio Tanzania yetu, Kikwete Rais Wetu na CCM Chama Chetu''.
Tanza..nia.. Tanzania...,.