Liyumba aachiwa lakini PCCB wambeba...


nyambaf! Hao wadada (maCD) wafungue mashtaka kwani walibakwa?
 
Hakimu kesi ya Liyumba kuchunguzwa ?

Idara husika inafuatilia kwa karibu suala la kuachiliwa kwa Liyumba na mwenzake katika kesi iliyoitia taifa hasara ya mabilioni kutokana na uzembe na pengine mchezo mchafu wa rushwa.

Inavyoonekana sasa kinachofuatiliwa ni kama kuna rushwa yoyote iliyotmebea kati ya washtakiwa na watoa hukumu. Uvumi uliopo ni kwamba kuna watu waliokula milioni 200 za kina jamaa na kuwahakikishia kuwa kesi yao itafutwa bila tatizo. Lakini walisahau kwamba issue hiyo sasa ni ya kitaifa na inawafuatiliwa na wazee wa nchi kwa karibu sana. Ajua. Naam, ajua kwa kina jamaa na sasa kazi kweli kweli inahitajika.....
 
Hii kesi ya Liyumba iliharakishwa labda kwa sababu ya kisiasa.
PCCB wangetakiwa kuwa na charge sheet iliyofanyiwa research na investigation ya uhakika. Wanachofanya ni kubahatisha bahatisha. Hii inakuwa kwa sababu wao kama PCCB hawana uzoefu wa kutosha (ingawa wanayo resources). Wakikutana na wanasheria wazoefu , wana chanwa chanwa.
Labda wangechukua/azima uzoefu kutoka kwa watu waliyobobea km SFO, FBI.
Waachane na mambo ya kukaa/kuchunguza mapato ya mechi za mpira / TFF.
Swali moja nauliza ni kuwa kama sikosei BOT imeteua kampuni moja kutoka nje kuchunguza cost ya twin towers ni sahihi na kama kuna udanganifu umefanika, Je hiyo kampuni ikisema costs ni sahihi na hakuna udanganifu , PCCB watakuwa tayari kumsafisha Liyumba?
 
Tupeni yaliyojiri, wako central au Keko?? Wameshaleta mahakamani kusomewa mashtaka mapya??? Michezo ya pwagu na pwaguzi.
 
nyambaf! Hao wadada (maCD) wafungue mashtaka kwani walibakwa?

Any person who intentionally transmits HIV to another person commits an offence, and on conviction shall be liable to imprisonment to a term of not less than five years and not exceeding ten years.( HIV and AIDS (prevention and control) 2008 (47)....tehetehe
 
Last edited by a moderator:

Hii ndio sababu kuu ya kuwakamata. Si unajua tena Heri ili ukubalike na watu ni lazima uonekane kuwa unafanya kazi sasa kama kila siku wanasikia malalamiko ya ufisadi na watuhumiwa hawakamatwi si bora uwaridhishe ili wakuone unafanya kazi (kilichopo nyuma ya pazia -uchaguzi ni mwakani so pengine by the time uchunguzi wa kuwatia lawamani unakamilika huenda ikachukua muda mrefu sana sasa ili upate kura ni lazima uwajibike hata kama ni kwa kukimbizanakimbizana bila kufanya lolote la maana mradi umeonekana uwanja wa mapambano.
 
tuache kuhukumu kwenye mambo tusiayoyajua na kumsifia kikwete bila sababu.

kama hati yab mashtaka imekosewa walipaswa kuachiwa huru kama mahakama ilivyoamua. huku kuwavizia ndo yale ya idd amin jaji anatoa hukumu badala yake yeye anakamatwa na kusewkwa ndani.

ukiangalia mtiririko wa hizi kesi ni uonevu mtupu, kama unajua abc za ujezni kwenye miradi mikubwa wafuatao walipaswa ndo wakamatwe

consultant webb uronu ambaye ndiye aliyekadiria gharama za ujenzi. na ndiye anaidhinisha contractor alipwe kupitia certificates of paynment. kweka na liumba hawana uwezo wowote wa kuidhinisha contractor alipwe bila idhini ya quantity surveyor

kuna kampuni inaitwa mekon architect imeteuliwa kufanya tathmini mpya kuhusu gharama zazilizotumika kujenga yale majengo, ndo kwanza wameanza kazi kwa nini wasingesubiri ripoti yao kabla ya kuanza kurundika watu ndani?
 

I conquer ... the case is being driven politically ... there a number of rights that these guys are being denied from ... our law enforcement organs (police, pccb etc.) waache kufanya kazi kupitia pressure za magazeti na chuki binafsi.

sitetei ufisadi lakini mahakama ndio pekee iamue hivyo kuzingatia haki za watuhumiwa ... tuache ushabiki usio na tija!!
 

Baba huo Ukimwi alipimwa na nani?
 
Tupeni yaliyojiri, wako central au Keko?? Wameshaleta mahakamani kusomewa mashtaka mapya??? Michezo ya pwagu na pwaguzi.

Ngonjera naona bado zinaendelea.....! Jana nilisikia kny vyombo vya habari (ITV & TBC1) kuwa Liyumba kasomewa mashtaka mapya mawili........!

Lakini, yule mwenzie Kweka.....sikusikia lolote.....na ilionekana kulikuwa na ubishi wa utoaji wa dhamana kati ya mawakili wa utetezi na waendesha mashtaka......shauri hilo litasikilizwa hopeful leo!

Hapa ni mazingaombwe matupu kwa kweli!
 
Liyumba alisomewa mashitaka mawili jana kati ya matatu ya awali. Upande wa mashtaki walilumbana na upande wa utetezi kuhusu dhamana ya nusu ya bil. 210. Kesi iliahirishwa hadi leo tarehe 29/5/2009. Dhamana imekuwa ni sh. milioni 300,na masharti mengine ni kama yale ya awali. Kwa kuwa ndugu hawakuwa wanategemea uamuzi huu mzuri, hawakuwa wamejiandaa na documents wala wadhamini hawakuwa wameshafika mahakamani. Kesi imeahirishwa hadi Jumatatu tarehe 1/06/2009 kwa ajili ya dhamana na kutajwa tena.

Kweli kama binadamu nimefurahi sana, hasa nilipowaona ndugu wakikumbatiana na kufurahi nami nimejikuta nikikumbatiana nao, hadi Liyumba mwenyewe. Kama alikula hela hakula peke yake, huo ni mtandao. Binadamu ni lazima tuwe na utu. Acha sasa sheria ichukue mkondo wake tuone mwisho wa kesi hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…