Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Kwema Wakuu!
Logically, Ikiwa Rais hashtakiwi hiyo itamaanisha Hafuati na hayupo chini ya Sheria.
Ikiwa mtu hayupo chini ya Sheria hiyo itamaanisha hatokani na Sheria.
Hii ni kusema, ikiwa watu watamchagua mtu awe Rais au kiongozi ambaye hatashtakiwa kwa Sheria itamaanisha hawakufuata Sheria yaani hawakumchagua huyo mtu au huyo kiongozi.
Neno uchaguzi, humaanisha Uhuru wa Maamuzi.
Sheria huhusu uchaguzi, Uhuru wa watu kujiamulia mambo Fulani kwa Makubaliano. Sheria ni makubaliano ya watu ambayo huwaongoza.
Kwa Lugha nyepesi Sheria ndio Njia, muongozo ambao watu huitumia kupitia kuelekea Kule wanakotaka. Lakini kwenye Njia hamwezi kuwa wote mbele, lazima mumchague kiongozi ambaye atakuwa mbele yenu kuwaongoza.
Mtu kuwa mbele haimaanishi yupo juu ya Sheria, kwamba hafuati Sheria nope!
Mtu yeyote ambaye hashtakiwi huyo ni mungumtu. Yaani mtu ambaye yupo juu ya Sheria huyo ni mungumtu.
Zamani Wafalme walikuwa miunguwatu wenyewe wakidanganya watu kuwa Wana divine power.
Mtu ambaye yeye hashtakiwi lakini anaongoza wanaoshtakiwa huyo anafanya uhalifu.
Kuongozwa na mtu ambaye hashtakiwi ni kukolonaiziwa.
Sheria inahusu mambo Makuu yafuatayo;
1. Makubaliano
2. UHURU
3. AKILI
4. HAKI
5. KWELI (MANTIKI)
6. MUKTADHA
Hakuna mtu mwenye akili timamu au mwenye HAKI ambaye atakubaliana na mtu mwingine kuwa Wachague kiongozi atakayewaongoza lakini huyo kiongozi awe juu ya Sheria. Hayupo huyo mtu.
Kwa Sababu kiakili kumfanya mtu awe na kinga ya kutoshtakiwa ni kumfanya awe mungu wenu. Na wenye Hali na akili kamwe hawawezi kuruhusu Jambo hilo.
Kimabavu, bila makubaliano, kwa dhulma wanaweza kukaa watu Fulani wasiowaadilifu wakaunda utaratibu wakauita Sheria(ingawaje sio Sheria) na kumfanya mtu kuwa mungu yaani aliyejuu ya yote, asiyeshtakiwa.
Na watu wote ambao watakaoshiriki kwenye kuweka huo utaratibu watapoteza sifa ya kuwa waadilifu, wenye HAKI, na wataingia kwenye kundi la watu wenye Njama, mipango ovu, na kujigeuza MIUNGU Watu.
Vijana lazima waelewe kuwa, utakapofika eneo ambalo kuna watu wasioshtakiwa Basi hapo ujue haupo sehemu Salama. Lazima tahadhari iwe kubwa zaidi.
Watu makini, hawawezi tegemea msaada wowote wa HAKI na kisheria kutoka kwa watu wenzao wasioshtakiwa kwa Sheria.
Yaani, huwezi tegemea msaada WA kisheria kwa mtu ambaye yeye hayupo chini ya Sheria Never ever.
Labda unachotaka ni upendeleo, kuhurumiwa n.k.
Hata ukipewa msaada wa kisheria au ukipewa HAKI na mtu ambaye hayupo chini ya Sheria usije ukajidanganya mtu huyo ni MWEMA.
Hiyo itatokana na yeye alivyoamka siku hiyo.
Acha nipumzike sasa
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam