Love at first sight

Love at first sight

Kauli zako, misimamo yako, wajihi wako na hulka yako (kimaandishi) inakakisi mtu fulani. Kuna watu humu ndani ni wa kuigwa, inapokuwa ndivyo sivyo, majukumu ya vikongwe siye ni kuwakumbusha tu!
Inaakisi mtu fulani asiye na haki ya kukosea na kupendana na mtu?

Kama kutokosea na kumpenda mtu ni mambo yanayoweza kumfanya mtu akawa SIO mtu wa kuigwa, basi nikupe pole....naishi maisha yangu kama binadamu wengine wa kawaida
 
Mahi 😹😹
Kwahiyo wewe unapenda mjifungie chumbani peke yenu..!! Mnafanyaga vitu gani wenzetu 🤣
 
Hey guys

Imeshawahi kutokea ile hali umemuona mtu mara moja tu ukatamani awe wako?

Imenikuta stendi ya mabus mkoa fulani kuja Dar. Siku nafika pale nikamuona mkaka mmoja amazing,sijui kwanini alikuwa ananiangalia vizuri namna ile...kimoyo moyo nikaweka sala fupi "ee Mungu huyu kaka hata nisipokaa nae seat moja naomba nisafiri nae bus moja tu" halafu nikamalizia na Amen,nikaingia kwenye bus

Nimefika kwenye bus nikakaa nikiendelea kusali sala ile ile ya Mungu asaidie yule kaka kuwepo ndani ya bus nililopo,nikajisemea ngoja nitoke ndani ya bus nijifanye naenda washroom ili nimuone hata mara nyingine,nikatoka nikaenda washroom

Mungu ni mkuu jamani, nilivyotoka washroom nikaingia ndani ya bus nikamuona yule kaka ndani ya lile bus, mimi namba 9 yeye 10

Sikuwahi kuona safari fupi kama ile japo kiuhalisia ni safari ndefu mnoooo, masaa yalikimbia fasta kinyama huku tukiwa tumezoeana kama vile tulikuwa tunafahamiana kabla.

Hiyo ni mwaka mmoja uliopita tarehe kama ya leo,tumekamilisha mwaka with my man 😊😊 Japo haiwahusu wala haiwasaidii kitu lakini nawaambia tu...nampenda huyu mwanaume

Naona kila kitu changu kinampenda,macho yakimuona napata ile amani ambayo siipati kwa yoyote,mwili wangu umemkubali mana nina hisia kali sana juu yake,nikiisikia sauti yake napata ile hamasa ya kuendelea kumsikiliza akiongea hata kama haongei na mimi

Sijawahi kuwa mdau ya ngono lakini tangu nikutane naye nataka kila muda tuwe peke yetu chumbani

Cheers to many years with my man 🥂

Am so in love!
Safi sana
 
Uvivu tu wa kuandika, lakini ilishawahi ni tokea ila mimi nilijiwahi nikasema huyu mtu nisipotumia akili nikatumia moyo atanisumbua mbeleni.

So nikampotezea akadai tuwe marafiki nikakataa ninachoshukuru nilikwepa kuliwa kimasihara,japo nilikuwa nikimuona hadi na sweat gafla.
 
Back
Top Bottom