Lowassa aikana Richmond, asema alijiuzulu kwa heshima ya serikali na chama chake!



Hawana nyimbo hawa wafuasi wa lowasa kawapanga kumsafishia njia ya kwenda kutufisadi haswaaa!
Watamnadi saana but hatapata urais kamwe
 
Wameniudhi sana NEC ya CCM. Badala ya kuikabidhi dola watuhumiwa wa ufisadi ili sheria ichukue mkondo wake wao wanalirudisha suala hili kwenye CC yao. Tumefikaje hapa pa kubembeleza wahalifu kiasi hiki? Waachieni akina Mramba basi ah!
 

Kama kuna kaukweli hivi!!!
 
hawa wanajaribu sana kucheza na akili za Watanzania na kwa bahati mbaya huko kwenye mikutano ya CCM wamejaa mbumbumbu watupu. Hawa ndio walikaa kikai cha kwanza wakatutangazia wanataka kujivua Magamba.

Ugonvii mkubwa wakatukana na matusi makubwa makubwa huyo Nape alikuwa mru mdogo tu. Nakumbuka kiongozi mmoja akasimama na kuwataja hadharani kuwa Rostam, Chenge na Lowassa ndio wanakiharibu chama na wakafikia maamuzi ya chama kujivua gamba.

Wakavunja sekretariet na ndio kuchaguliwa akina Malima, Chiligati na Nape leo tena wanawageuka baada ya kuahirisha mikutano mingapi?.. Kila kukicha wanakuja na jipya hivi hawa jamaa wanafikiri sisi wajinga sana au?

Haya miezi sita tu iliypita sii ndiouwa fahari ya chama kujivua magamba! leo tena nyoka kujisafisha ni asili yake imekuwa magamba ya Mamba ndio kinga yake..
 
Vita vya panzi neema kwa kunguru.....Lowasa mwaga vitu waTZ tujue ukweli
 
Mkandara,
Sekretarieti iliyopo sasa ya akina Mukama, Chiligati, Nape, January na Mwigulu itaondoka mapema kabla ya 2012 kama hawana "guts" za kujiondoa wenyewe. Hawana "support" ya yeyote mle ndani ya CCM. Wamezingirwa. Dhambi ya kumtelekeza Mpendazoe inawatafuna baadhi yao.
 
Nape ameambiwa apeleke ushahidi wa kumtuhumu lowassa ni fasadi na akishindwa achukuliwe hatua za kinidhamu ambazo kwa vyovyote vile ni kuachichwa cheo cha katibu mwenezi.
Atautoa wapi ushahidi wakati bunge na hansad zinamsafisha EL hii maana yake ni kwamba hana cheo ni sawa na kuambiwa na mganga upeleke miguu ya nyoka ili mgojwa apone.
 
Atautoa wapi ushahidi wakati bunge na hansad zinamsafisha EL hii maana yake ni kwamba hana cheo ni sawa na kuambiwa na mganga upeleke miguu ya nyoka ili mgojwa apone.

ha haaaa haaaaa

nimekusoma mkuu
 
Nawezaje kuipata ripoti hio ya 1997 ya huyo Mzee? Ilihusu nini hasa? Content yake je? Mkapa alisaidiaje? Kwa nini alimsaidia? Ilikua na athari gani? Kwa hio si kweli kwamba JK ndio kiongozi mwenye mvuto? wala sio chaguo la Mungu? Mmmmh
Kwa taarifa tu baada ya ripoti hiyo ya mwaka 1997 iliyotolewa na Daud Mwakawago, huyo Daud Mwakawago hatunaye tena, yupo ahera.
 
Atautoa wapi ushahidi wakati bunge na hansad zinamsafisha EL hii maana yake ni kwamba hana cheo ni sawa na kuambiwa na mganga upeleke miguu ya nyoka ili mgojwa apone.
Watu waendelee tu na maovu yao nchi hii. Ipo siku. Nani alijua Hosni Mubarak wa Misri atafikishwa mahakamani akiwa kwenye machela? Nguvu zote alizokuwa nazo Gadafi na familia yake ziko wapi sasa?

Wao wawachezee WATANZANIA tu. Kutoka NEC warudi CC, kutoka CC warudi kamati ya "MAADILI", kutoka huko waende sekretarieti, kutoka sekretariet warudi CC, safari ianze upya.
HAKUNAGA kama LOWASA nchi hii!
 

Hapa Jamii forums tupo watu wa viwango tofauti. Kuna wanaochangia mada kwa ushabiki na kuna wachambuzi makini. Mada yangu ya hapo chini hata kama haijaeleweka kuhusu Mzee ruksa lakini ina akisi kitu fulani kinachoendana na Lowasa kwamba Ruksa alijiuzuru uwaziri na Lowasa hali kadhalika.

Tufanye uchambuzi kwa kuchunguza sarafu p[ande zote, si upande mmoja tu na kutolea hitimisho ni mtazamo finyu mno. Hata unayemwona mbaya wako akifanya mazuri mpongeze huo ndio ustarabu kwani mazuri anayofanya au atakayofanya ni kwa manufaa yetu sote.

 
niliwaeleza kuwa Lowasa hakukurupuka kufanya maamuzi magumu,na alisha wahi kuliongelea hili juu ya kwanini haufunja mkataba,ila kwa kuwa Kijana Nape anafanya kazi kwa kulipiza kisasi alitaka kumuumbua Lowasa pasipo kuelewa msingi mzima wa tatizo la kampuni tata,safi Lowasa

Bado sijaona waziri mwenye maamuzi magumu kama wewe tukiachana na marehem Sokoine
 
Duh!

Ama kweli watanzania tu wavivu wa kufikiri na mbilikimo wa mawazo.

Pamoja na Lowassa kuongea kwa uwazi bado mnadai ni fisadi!. Tena ni maswali hayo hayo mlikuwa mnauliza, mkishajibiwa mnageuka.
Huo sio uspin doctor bali ni upuuzi na kuwa na uwezo mdogo wa kufikiria.
 
Yaani mmeumbuka kweli kweli.

WAPI WAPI HALISI?? lol

Halisi mkuu njoo basi tumvue Lowassa Gamba maana ni Fisadi fisadi fisadi.

Sometimes wakuu wengi humu nashindwa kuwaelewa, nahisi hata JF wengi wetu tunatumia matumbo kufikiri. Baada ya Lowassa kuongea ndo nimeanza kuwaelewa baadhi yenu.

Anyway Mungu atawalipa hapa duniani.
 

siku zote mi nilidhani weye ni CDM kumbe ni CCM ... btw! Lowasa anajaribu kujikosha... ili JK aonekane ni mbaya!

kama kweli kosa halikuwa lake .. kwanini alijiuzulu... ile sababu aliyotoa ati "chanzo ni uwaziri mkuu ni danganya toto"




 


mkuu wewe kama mimi......juzi niliandika tena kwa herufi kubwa kuwa LOWASA HANG'OKI CCM...Mheshimiwa halisi alkaniambia kaka safari hii huyu bwana kakalia kuti kavu atang'oka.lakini ndo hivyo mzee mzima anapeta...kuhusu kikwete sina la kuongeza maana singanture yangu inaongea yote....
 
Lowassa = Sokoine
Kwa lipi FairPlayer! Haya kapata nafasi kuyasema jana tangu 2006?
- Alimpigia simu JK ili avunje mkataba. JK akamkatalia. Kwa nini asijiuzulu wakati huo?
- Kule kuisafisha kashfa hii kwa kutumia TAKUKURU yetu kulifanywa na nani?
-Alipewa nafasi tele na Sitta tena yenye kinga kamili. Akaiacha. Kaamkia NEC jana!
- Mwambie afunguke zaidi. Anadai katukanwa. Aende hata mahakamani angalau.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…