Lowassa aikana Richmond, asema alijiuzulu kwa heshima ya serikali na chama chake!

Lowassa aikana Richmond, asema alijiuzulu kwa heshima ya serikali na chama chake!

Sawa ni ya mwaka 1997, hakukuwa na uchaguzi...

Mimi nataka sana kuiona na tuna haki ya wananchi kuambiwa maanake Lowassa kasahau kama JK bado ni rais na yupo madarakani.. Kwa hiyo ni muhimu aseme kweli JK alifanya nini na alituhumiwa nini kiasi kwamba leo asingekuwepo,... sijui ndio angeuliwa ama kutokuwa rais.. Ukweli tunautaka uwe wazi, na yeye mwenyewe tuna machungu naye bado asifikirie kumtishia JK ndio kamaliza ya kwake.

Mkuu Mkandara,

Jamaa anasahau kuwa kama ni madhambi hayo ya 1997 naye alishiriki kwenye huo uozo, anasahau kwamba tunafahamu ushiriki wake kumweka JK, anasahau alivyotumia media kuchafua wenzake.

Lakini zaidi ya yote anakwepa kuzungumzia mchakato wa kuipa zabuni Richmond kwa sababu anafahamu ushahidi unaomng'ang'ania.

Hana lolote huyo
 
SOURCE: TANZANIA DAIMA 25/11/11.

WanaJF, sasa nitawahoji:
1. Je, baada ya kupasua jipu huko Dodoma, CCM sasa ni wamoja na wamepona kabisa au jipu limegeuka kuwa kidonda ndugu?
2. Kitendo cha Mkapa kumpa mwongozo Kikwete wa jinsi ya kuipotezea hii issue ya ufisadi kinaleta taswira gani juu ya uwezo wa Kikwete kama kiongozi mkuu?
3. CCM waendelee na mfumo wa sasa wa mwenyekiti kuwa ndiye mtendaji mkuu, mkufunzi mkuu, mnadhimu mkuu, judge mkuu na msimamizi mkuu wa mambo yote ya chama?
[/FONT][/COLOR]


Mkuu, japo hayo yote ni maswali ya msingi tunayopaswa kutafakari, lakini hilo la kwenye red tuwaachie wao wenyewe waache wafu wawazike wafu wao: yatuhusu nini sisi chama kinachokufa kianze kutushughulisha akili zetu? Watanzania tumeteswa sana na hiki chama yatubidi sasa tusipoteze akili zetu kwa mambo mafu bali akili zetu zituelekeze kuimarisha chama mbadala hasa hasa kwa ajili ya 2015.

Hata hivyo nimefurahishwa na jinsi Lowassa alivyojipanga na kujieleza ndani ya hilo genge linaloitwa NEC. Tangia mwanzo hili suala la kumvua gamba lilionekana vyema kwamba si uovu wa mtu fulani au watu fulani ndani ya chama. Ni system nzima ya chama na serikali ya hicho chama maana walizoea kuiba bila kukamatwa lakini sasa waliiba pabaya. Waliiba penye injini ya nchi yaani sekta ya umeme na madhara yake hayawezi kufichika. Mgao wa giza ulipoanza kuathiri, na si walala hoi tu, ukaathiri hata wazito wa nchi hii, wangeficha vipi ujambazi huu?

Sasa kuwazulia ufisadi wa chama watu watatu tu Lowassa, Chenge na Rostam ni mazingaombwe kuwazuzua wananchi. Makosa tunayofanya sisi wapiga kura ni kucheza vibwagizo vya CCM. Wakitwambia mkosa ni fulani tu basi tunaimba wimbo wao na tunahamisha hasira zetu kwa chama kuelekea kwa hao watu watatu na voilla wenzenu wanaendelea kuimenya hii nchi wakati mnabaki mnashangaa tu. Sasa Lowassa na Chenge hawataki kufanywa mbuzi wa kafara. Na kwa hilo wako sahihi. Wanatupa urahisi sisi wananchi wa kawaida kuweza kutambua kuwa chama chote kimeoza.
 
Hiyo ndio sisiem zaidi uijuavyo,kigeu geu wanajigeukia,kwenye chama maamuzi hayaeleweki,je?kwenye serikali wanayoongoza si balaa!
 
hivi lowasa hajavuliwa gamba tu...nape vipi umeshindwa kazi...
 
Ngoma inogile asante mkuu kwa update maana huku kwetu hakuna access ya magazeti..well said Lowasa aka kondoo wa kafara naamini lowasa ana mengi zaidi ya hayo..

kwani muda wote EL alikuwa wapi! Kwanini asiseme kwa watanzania?
Hivi wewe na FF ni ndugu?
 
Hakuna wa kumwajibisha mwenzake wote yangeyange wanafanana
 
Hizi habari za kujivua gamba zinanichefua mno kwa sababu naona kabisa ni usanii.

Mkuu, kwale ambao si wanafiki, hii habari ya kujivua gamba inachefua sana; labda kwa akina FF na Wenzake!
 
Muheshimiwa hapo kwenye RED mimi nakukatalia 100% siyo kweli kuwa Mzee ruksa alikuwa chaguo la Mwalimu la hasha...Kulikuwa na zengwe kubwa ndani yake...lakini kulikuwa hakuna jinsi ni lazima ionekane kuwa pendekezo la kwanza ni mzee ruksa....

Chaguo la mwalimu wakati ule alikuwa Waziri mkuu wa wakati ule Salim Ahmed Salimu..Lakini kwa busara zao waliona isingependeza kumpendekeza mgombea wa kwanza awe waziri mkuu badala ya makamo wa raisi na raisi wa Zanzibar kwa wakati ule amabaye alikuwa Mzee ruksa....ndipo alipoitwa mzee ruksa na kuombwa akubaili hilo ombi ...lakini akaambiwa wakati wa mkutano mkuu wa CCM pale Chimwaga atakapo tangazwa kuwa yeye ndio Mgombea uraisi ajaye......baadae yeye ashukuru kwa kumpendekeza lakini atoe udhuru kuwa nafasi hii yeye ahiwezi ni kubwa sana kwake....

Naye mzee Ruksa akapata washauri wakamwambia mzee usiwe mjinga wewe lini tena utakuja kuwa raisi...ndipo yeye alipo simama baada ya kutangazwa kuwa ndio mgombea..badala ya kutoa udhuru yeye alikubali moja kwa moja.....na ndio hapo ilipochipuka uhasama wa chini chini kati ya Mzee ruksa na Mwl...na migongano ya hapa na pale...mwanzoni wa utawala wa mzee ruksa...sasa wewe unatumabia Mzee ruksa alikuwa chaguo la mwalimu hii sio kweli...kama unampigia chapuo Mr Lowasa mpigie tuu lakini sio kwa kisingizio hiki

Mkuu, now you 're talking. Lol!
 
.. kitu nilichopenda toka kwa EL ni kumwambia mkuu wake by then kuwa, uchafu wako wa 97 bado sijaufikia, ua wewe unadhani nimeufikia kiasi cha kunitenga? Kama nimeufikia basi nitose, kama bado basi nilinde nifike ulipo.

.. mana nyingine: Hii ni njia ya kiutu uzima kulalamika na kudai haki ki-uke weza..."mbona mama fulani umemnunulia kanga, nami nataka" i.e jamaa alikuwa nasema kama wewe ulikuwa mchafu umepata, kwa nini mimi hutaki nipate.

naamini wakimyima anachotaka, basi atafanya kama mke mweza: atalalamika mlangoni kwa sauti kiasi cha majirani na watoto kujua yaliyomo ndani ili wamuonee huruma.... kwetu itakuwa kama vita ya pazi.............
 
Hiyo ni sehemu tu ya yale mengi ambayo Lowassa atayaweka wazi kadri siku zinavyozidi kwenda kimaandishi na kisauti pia kuna na hapo ndipo utakapogundua kuwa hakurupuki na ana sababu za kukaa kimya. Walimtoa Sokoine sasa tunae lowassa kumbuka mmsai hakisoma hafanyi ajizi.

Wishful thinking unategemea Lowassa na Kikwete wanalao tofauti? Hizo ni sarakasi za kusafishana ili mmoja ampishe mwenzie aje kuchukua madaraka 2015. Embu nimalizie kazi yangu niende kuanza ijumaa yangu.
 
Nomba wana JF mnielewe, siungi mkono ufisadi na ninamchukia sana fisadi,na kwa kweli kabisa nilikuwa namchukia sana Lowasa kwa sababu ya ufisadi, lakini Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, mimi msamha kwake nimetoa.

Kuna swali ambalo naomba kila mmoja ajiulize,kwa nini Lowasa alipomkumbusha Mwenyekiti wake (JK) kwamba alimpingia simu kumwambia auvunje mkataba wa Richmond mwenyekiti akamkatalia mbona mwenyeki hakani kwamba hakupewa hiyo taarifa? Richmond ni ya JK na Rostam swahiba wake,Lowasa kafanywa mbuzi wa kafara tu!

ASANTE LOWASA KWA KUTUAMBIA UKWELI,INGAWA UMECHELEWA SANA! Tunaomba uweke adharani taarifa hiyo iliyotoka Zanzibar 1997,wao si wamemwaga ugali,mwaga mboga kamanda
 
Mtajuwa sasa kwanini waliomtuma kazi Mwakyembe ...sasa wanataka AFE ......maana ni wazi kuwa pamoja na lowassa kuonekana mbaya ....issue ya Richmond kina mwakyembe na manyanya stella .....walivuta pesa ili wamtose....kutoka kwa JK ....na rule of mafia ina apply ...

Ukiamua kubeba Siri za mafia ...ujiandae kufa......ni wazi Mwakyembe alitakiwa AFE kabla Lowassa hajafunguka (after all hata Lowassa alikuwa AFE ili asifunguke ..Kama sio kuwahi matibabu Ujerumani).......inawezekana hii nayo imemfanya afunguke ili asife na Siri .........
 
Niceeeeee............!!!!! veriiiiiiiii gudiiiiiii, let me add this ujue Lowassa is free from magamba,...

JK kasemaaaaaaa....MWENYE USHAHIDI KUHUSU TUHUMA ZA LOWASSA AZILETE, LA SIVYO WAPAYUKAJI WAKINA NAPE & CHILLI. WATACHUKULIWA HATUA ZA KINIDHAMU, eeeehh bana JK kamaliza kazi, SUMAYE KAPIGILIA MSUMARI WA MOTO, yaani NGUVU YA SUMAYE + LOWASSA ni nomaaaa,

EL FOR PRESIDENT 2015, u hve ma vote, sisikii, sielewiii, sioniii, tunataka Kiongozi mchapa kazi, hata YESU ALICHUKIWA NA KUUAWA, sembuse Lowassa, go buddy....i am done, period..!!!

never ever... over our blood.... that red will never happen
 
wakati haya yanaendelea, the world is watching us! Watakuwa wanajiuliza kuwa hizo kamati zinazokutana zina watu wasiofika hata 50 (makumi tano!) ambao kiukweli wanaonekana wazi kuwa wamepoteza tayari haki ya kuwa viongozi/kuongoza Tanzania kutokana na matendo yao.

Je, hao watu wengine 50,000,000 mbona hawachukui hatua yoyote kuliadabisha kundi hili dogo la wahuni!?

......kweli 'Mitanzania ndivyo tulivyo'!!
Aibu yao aibu yetu
 
hivi lowasa hajavuliwa gamba tu...nape vipi umeshindwa kazi...

Nape ameambiwa apeleke ushahidi wa kumtuhumu lowassa ni fasadi na akishindwa achukuliwe hatua za kinidhamu ambazo kwa vyovyote vile ni kuachichwa cheo cha katibu mwenezi.
 
Ndio ilivyo sikio la kufa halisikii dawa, tena wamefikia hata kumwambia kaa anataka kuhama ahame wao hawatishiki. NI JK huyu huyu majuzi tu alikuwa akisema (kumuunga mkono Nape) ya kwamba wanaotakiwa kuvuliwa magamba wataondoka!.. maskini kabakia mtupu. Sasa mimi naomba sana nijue hiyo report ya kina Daud Mwakawago maadam Lowassa kaisema nadhani wananchi tuna kila haki ya kudai kujua report ile inasema nini...

Hili ndio tishio la Lowassa kwa JK kwa sababu wanajua swala hili ni wachache na Lowassa kasema kwa mafumbo ambayo JK pekee ndiye anajua kinachoendelea - Akiwa na maana mkuu wangu kumbuka tulikotoka! - Na ukiisoma vizuri hii hotuba ni kutaka muafaka baina yake yeye, Mkapa na Sumaye ili kurudisha Ufisadi wao wote kuwa chama kimoja. Lowassa amekuwa mpole kwa JK lakini mkali na mwenye matusi makubwa kwa Nape kiongozi wa chama ambaye anatimiza majukumu yake..

Mkuu,

Siasa zetu ni kazi kweli.Siku Nape alipoteuliwa nilitoa angalizo ambalo leo naona Pasco kwenye ukurasa wa kwanza amelitoa.

Hata Hivyo inaonekana sasa Kikwete ndiye Mwenye hali ngumu zaidi,na akicheza kwa hili hatamaliza madaraka yake.Sasa atamuhitaji Lowassa zaidi kumlinda dhidi ya maadui wa kisiasa wa nje ya chama chake.Mpasuko utakaokuja CCM katika dhana ya kutaka kuleta umoja utakuwa mkubwa zaidi>Upinzani tuendelee kujipanga vyema
 
Back
Top Bottom