Mwanademokrasia
New Member
- Nov 28, 2011
- 1
- 0
Jana Mh Edward Lowassa hatimaye alitamka maneno yanayomfanya kuonekana hakushiriki katika ufisadi wa Richmond kwa kumpa lawama (zote) Rais Jakaya Kikwete.
"Alibi" ya Lowassa kuwa alimpigia simu Rais kutaka kusitishwa kwa Richmond baada ya yeye kugundua mapema kua ilikua na dosari haileti mantiki yeyote zaidi ya kumuonyesha lowassa kuwa ni mpiganaji tu wa kisiasa na wala siyo kiongozi mahiri wala safi.
kama Rostam ndiyo anatajwa kuwa msukaji mkubwa wa mpango wa Richmond (mpaka kusafiri Marekani kutafuta hawa "wawekezaji") na ni Rostam huyu huyu aliyemsukuma Kikwete amweke Lowassa Waziri Mkuu na ni Rostam huyu huyu swahiba mkubwa kisiasa na kibiashara na Lowassa itakuaje Lowassa anayeaamini siasa za kulindana amtose Rostam kwa kumshauri kwa uwazi mkubwa Kikwete kuwa Richmond ivunjwe? hii inanipa jibu moja tu Lowassa na Rostam walijua lazima wawe na kinga kama hili suala feki ikijulikana na hapo ndipo walipopiga hii simu kwa JK( kama "alibi") akiwa anakula "raha nje ya nchi "anasherehekea" bado ushindi wa Urais uliosababishwa na hawa maswahiba wake huku wakiwa wanaonyesha wasiwasi Kidogo wa mkataba huu (huku wakijua Rais ana maslahi yake katika hili na atakua mzito kukubaliana moja kwa moja na hili la kusitishwa kwa mkataba huku na wenyewe wakiwashinikiza wahusika wengine hapa Tanzania kuupitisha mkataba ).
Unataka kuniambia katika suala zima hili Lowassa alimpigia simu boss wake simu moja tu tena akiwa nje ya nchi kuonyesha wasiwasi wa dili hili ambalo yeye alikua hapati "vijisenti" vyetu vyovyote na kuna hatari ya kutumiwa yeye na ofisi yake kumuaribia kisiasa kama ikija gundulika? Lowassa ana akili zaidi ya hizi na hii inaonyesha kuhusika kwake m1 kwa m1 na Richmond na kwamba hili aliloongea jana ni "alibi tu iliyopikwa kama tahadhari ikiwa Richmond ingekuja kunuka....
Usiwe mjinga wewe Kidatu, Lowasa anazo hatia kibao ila anajifanya mnjanja, ukisoma post za nyuma utaona!!!!!!Wacha huyu mwizi atoswe tumsahau, kwa nini unatetea mwizi lakini au huelewi wizi wake tukutajie???????????Lowasa hana makosa, hakutendewa haki hata kidogo. Tuishi kwa kumuogopa Mungu, kama kuna kundi linapanga njama chafu mbele ya kiumbe cha Mungu kisicho na makosa, basi subiri uuone jinsi ukweli utakavyojitenga na uwongo. Nuru na giza havitakaa pamoja hata siku moja. Lowasa atashinda kwa hili nina hakika 110%
Wewe ni maghamba namba moja unamkaribisha Lowasa aende wapi,labda unayo CHADEMA nyingine!!!!!! Umesahau kuwa Mhs Slaa alisema akishika Urais Lowassa atakuwa wakwanza kutangulia lupango fisadi mkubwa!!!!!!!!!!Lowasa karibu Chadema
Kabota nitakubota, hata kama kiroboto,
Yote unayolumbata, si chochote ni kokoto,
Huna mpata na kata, nijuacho u limpyoto,
Kabota acha unywanywa, naona unatumiwa.
Lowassa bado fisadi, hata mmpambe vipi,
Kambota wewe hasidi, watumika kama nepi,
wajiona wafaidi, kumbe kesho ni makapi,
Kabota acha unywanywa, Lowassa akutumia.
Wauliza nalipwaje, Nani huyo anilipe?
Sijalipwa hata punje, mie mwezio si kupe,
Shurti nijikunje, niishi si kwa mahepe,
Kabota acha ushamba, Lowassa atakuponza.
Naijua Richmond, Richmond ni Lowassa,
Kikwete ni Richmond, Richmond ni mkasa,
Kambota nawe ni bundi, Richmond takutesa,
Japo wachumia tumbo, Kambota acha ujuha.
Utajaliwa ja ng'oda, Siku yako ikifika
Ja ng'oda utakonda, Lowassa akikutoka
Ukuuishie ukuda, ubaki kulalamika
Fisadi hana rafiki, Jifunze kwake Lowassa
Mambo yalipombana, Kikwete kaumuumbua,
Hawa marafiki sana, Itakuwa wewe bua,
Leo sana wajiona, ujinga wakusumbua,
Kambota acha ujuha, Lowassa hasafishiki.
Huna mpaka na nune, Kambota wala jaani,
Leo wewe ujivune, kumbe wenda majilini,
Sema sana utukane, itafika arobaini,
Kambota acha ujuha, Lowassa hasafishiki.
Kaditamati natua, mbele sitaendelea,
Kwa hapa naomba dua, wadudi anisikia,
Ninamuomba mulua, Kambota aone jua,
Kambota chumia tumbo, hebu tumia ubongo.
kwa hiyo ulitaka mwenyekiti aanze kusutana na mjumbe mkutanoni sio?mdau pale sio kwenye baraza ya kahawa lazima ufahamu hilo lowassa yeye alikuwa ananung'unika tu wala hakuuliza swali lililohitaji majibu....Simtetei EL lakini kukataliwa na Nyerere sio kigezo tosha, kwa kifupi ni kwamba watanzania tutafute ufisadi mwingine wa EL uliomfanya akawa tajiri lakini si Richmond, hiyo ni ya JK kama sivyo na yeye alipaswa kujibu mapigo kwenye mkutano wa NEC lakini kwa kunyamaza inadhihirisha anahusika, kwani utajiri wa R1 wa haraka namna hiyo unatoka wapi??
Usiwe mjinga wewe Kidatu, Lowasa anazo hatia kibao ila anajifanya mnjanja, ukisoma post za nyuma utaona!!!!!!Wacha huyu mwizi atoswe tumsahau, kwa nini unatetea mwizi lakini au huelewi wizi wake tukutajie???????????
Mbona umemstahi kamanda?ungemwambia asiwe mjinga kama mwanaume wao wa shoka lowassa ambae mwalimu nyerere alikua wa kwanza kumwita lowassa mjinga alipomwambia mzee kawawa na yeye asiwe "mjinga" kama lowassa!
kuna taharifa kwamba siku ya mkutano wa NEC,Vyumba vingi vya wahariri wa Habari waliweza kumsikia live kutoka Dodoma kwa planned IT technology na ni kipind kile tu yeye anaongea!!hiyo yote ni kwamba aweze kusikika neno kwa neno habari ilipotiwe kama ilivyokuwa planned!!
FEDHA HAISHINDWI KITU!!!!!ENDELEA!!UEPIGA HATUA KATIKA KUJISAFISHA
kwani huoni kosa mambo ya kikao ni siri ya kwenye kikao,na kuna msemaji wa mambo yalnayojadiliwa kwenye kikao,,kilichofanywa ni ukosefu wa maadili kwani neno moja hutafsiriwa tofauti ikiwa kila mtu atasemaWhat is wrong with this?