Lowassa aikana Richmond, asema alijiuzulu kwa heshima ya serikali na chama chake!

Lowassa aikana Richmond, asema alijiuzulu kwa heshima ya serikali na chama chake!

Watanzania tusiongozwe na hisia bali imani ya kweli na inayofuata misingi ya haki...Lowasa alipewa chance na chama chake (wafuasi wa kundi lake ndani ya CCM) kujisafisha ili kutimiza azma yake ya kuchukua nchi 2015....
Kwa kuwa haki haikutendeka katika kutekeleza maazimio ya kamati iliyochunguza Richmond...basi ndivyo hivyo haki itakavyokiukwa katika kumfanya Lowasa kuchukua nchi 2015....
CCM itafanya kila namna kwa kipindi hiki kilichobaki ili kuhakikisha anapata suuport ya chama...ikiwezekana ngoma itabaki kwa wananchi...na hata kama wananchi watamkataa..basi yale ya kura za kichina!
 
Jana Mh Edward Lowassa hatimaye alitamka maneno yanayomfanya kuonekana hakushiriki katika ufisadi wa Richmond kwa kumpa lawama (zote) Rais Jakaya Kikwete.

"Alibi" ya Lowassa kuwa alimpigia simu Rais kutaka kusitishwa kwa Richmond baada ya yeye kugundua mapema kua ilikua na dosari haileti mantiki yeyote zaidi ya kumuonyesha lowassa kuwa ni mpiganaji tu wa kisiasa na wala siyo kiongozi mahiri wala safi.

kama Rostam ndiyo anatajwa kuwa msukaji mkubwa wa mpango wa Richmond (mpaka kusafiri Marekani kutafuta hawa "wawekezaji") na ni Rostam huyu huyu aliyemsukuma Kikwete amweke Lowassa Waziri Mkuu na ni Rostam huyu huyu swahiba mkubwa kisiasa na kibiashara na Lowassa itakuaje Lowassa anayeaamini siasa za kulindana amtose Rostam kwa kumshauri kwa uwazi mkubwa Kikwete kuwa Richmond ivunjwe? hii inanipa jibu moja tu Lowassa na Rostam walijua lazima wawe na kinga kama hili suala feki ikijulikana na hapo ndipo walipopiga hii simu kwa JK( kama "alibi") akiwa anakula "raha nje ya nchi "anasherehekea" bado ushindi wa Urais uliosababishwa na hawa maswahiba wake huku wakiwa wanaonyesha wasiwasi Kidogo wa mkataba huu (huku wakijua Rais ana maslahi yake katika hili na atakua mzito kukubaliana moja kwa moja na hili la kusitishwa kwa mkataba huku na wenyewe wakiwashinikiza wahusika wengine hapa Tanzania kuupitisha mkataba ).

Unataka kuniambia katika suala zima hili Lowassa alimpigia simu boss wake simu moja tu tena akiwa nje ya nchi kuonyesha wasiwasi wa dili hili ambalo yeye alikua hapati "vijisenti" vyetu vyovyote na kuna hatari ya kutumiwa yeye na ofisi yake kumuaribia kisiasa kama ikija gundulika? Lowassa ana akili zaidi ya hizi na hii inaonyesha kuhusika kwake m1 kwa m1 na Richmond na kwamba hili aliloongea jana ni "alibi tu iliyopikwa kama tahadhari ikiwa Richmond ingekuja kunuka....

Mkuu huku ndiko kutafakari tunakotakiwa tukufanye, sio tu kukubali kauli za kujisafisha na kuzipokea kama kasuku kisha kuzisambaza. Ndio maana Nyerere alipenda kusema "watanzania wenye akili wakaliona hilo". Kwanza ufisadi wa EL si katika Richmond tu. Aliosemwa na wahindi ananuka rushwa Richmond wala haikuwapo. Alipkataliwa na Nyerere hafai kuwa kiongozi wa nchi Richmond haikuwapo. Kwa hiyo usafi wa EL hautokani na simu anayodai kumpigia JK juu ya Richmond.
 
Ni vizuri tumefahamu kwamba na kikwete alihusika, tene mhusika mkuu katika kashfa hiyo. Wakiendelea kulumbana tutafahamu mengi. yetu masikio!!!
 
Ukimya wa Chadema katika sakata la kujisafisha kwa Lowasa inaonekana ni jinsi gani wanavyomuunga Mkono basi kwa heshima na tahadhima tunakuomba Mkuu Lowasa umwage ugali na Mboga CCM na uhamie Chadema kujakujenga chama. Ur my next president wengine wote wanaigiza big up Lowasa umeshinda vita
 
haya ni maneno ya Next president Lowasa aliyoyatamka jana akiwa Singida katika harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la KKT naomba kumnukuu " Kwa wale mnaofatilia siasa za Tanzania mnajua ni jinsi gani nilivyoshutumia kwa kashfa za kifisadi( RichMond) lakini kupitia sala zenu na zangu namshukuru Mungu ameanza kujibu maombi yangu kwani ushindi umeanza kupatikana na nitashinda makofi na vigelegele" mwisho wa kunukuu
 
Lowasa hana makosa, hakutendewa haki hata kidogo. Tuishi kwa kumuogopa Mungu, kama kuna kundi linapanga njama chafu mbele ya kiumbe cha Mungu kisicho na makosa, basi subiri uuone jinsi ukweli utakavyojitenga na uwongo. Nuru na giza havitakaa pamoja hata siku moja. Lowasa atashinda kwa hili nina hakika 110%
Usiwe mjinga wewe Kidatu, Lowasa anazo hatia kibao ila anajifanya mnjanja, ukisoma post za nyuma utaona!!!!!!Wacha huyu mwizi atoswe tumsahau, kwa nini unatetea mwizi lakini au huelewi wizi wake tukutajie???????????

 
Lowasa karibu Chadema
Wewe ni maghamba namba moja unamkaribisha Lowasa aende wapi,labda unayo CHADEMA nyingine!!!!!! Umesahau kuwa Mhs Slaa alisema akishika Urais Lowassa atakuwa wakwanza kutangulia lupango fisadi mkubwa!!!!!!!!!!

 
Kabota nitakubota, hata kama kiroboto,
Yote unayolumbata, si chochote ni kokoto,
Huna mpata na kata, nijuacho u limpyoto,
Kabota acha unywanywa, naona unatumiwa.

Lowassa bado fisadi, hata mmpambe vipi,
Kambota wewe hasidi, watumika kama nepi,
wajiona wafaidi, kumbe kesho ni makapi,
Kabota acha unywanywa, Lowassa akutumia.

Wauliza nalipwaje, Nani huyo anilipe?
Sijalipwa hata punje, mie mwezio si kupe,
Shurti nijikunje, niishi si kwa mahepe,
Kabota acha ushamba, Lowassa atakuponza.

Naijua Richmond, Richmond ni Lowassa,
Kikwete ni Richmond, Richmond ni mkasa,
Kambota nawe ni bundi, Richmond takutesa,
Japo wachumia tumbo, Kambota acha ujuha.

Utajaliwa ja ng'oda, Siku yako ikifika
Ja ng'oda utakonda, Lowassa akikutoka
Ukuuishie ukuda, ubaki kulalamika
Fisadi hana rafiki, Jifunze kwake Lowassa

Mambo yalipombana, Kikwete kaumuumbua,
Hawa marafiki sana, Itakuwa wewe bua,
Leo sana wajiona, ujinga wakusumbua,
Kambota acha ujuha, Lowassa hasafishiki.

Huna mpaka na nune, Kambota wala jaani,
Leo wewe ujivune, kumbe wenda majilini,
Sema sana utukane, itafika arobaini,
Kambota acha ujuha, Lowassa hasafishiki.

Kaditamati natua, mbele sitaendelea,
Kwa hapa naomba dua, wadudi anisikia,
Ninamuomba mulua, Kambota aone jua,
Kambota chumia tumbo, hebu tumia ubongo.

MHANGO WAJUA NINI?

Nkwazi nakuuliza, nini kimekuingia?
Mwenyewe wajishangaza, kubisha usiyojua
Kwa hoja nakuchakaza, hili unalitambua?
Mhango wajua nini? Zaidi ya kutumiwa?


Nakuuliza hasidi, nijibu nikulipue
Nitoe na ushahidi, watu wote wakujue
Watumiwa kama pedi, kanusha nikuumbue
Nyumba unayoringia, mimi ni mjenzi wake.


Lowassa mchapakazi, Leigwani maridadi
Tena yu baba mlezi, wa viwango na spidi
Muda wake hapotezi, Kulumbana nawe kidi
Nkwazi unachekesha kumtuhumu Lowassa.


Unalipwa bei gani, kwanini jibu hunipi?
Nimekutoa manani, wamung'unywa kama pipi
Unazungumza nini?, msimamo wako upi?
Nkwazi wanichekesha, kupungukiwa na hoja


Richmond mali ya mtu, Kikwete namtangaza
Punguza roho ya kutu, uongo kuutandaza
Wewe ni kidudu mtu, kwa hoja nakuchakaza
Mimi naitwa Kambota, "Kabota" waweweseka


Kwa hoja nakuadhibu, tamati nimefikia
Nakufundisha adabu, Zinduka umesinzia
Kwa hoja wewe ni bubu, leo nakupasulia
Nkwazi wajua nini? zaidi ya kutumiwa?
 
Simtetei EL lakini kukataliwa na Nyerere sio kigezo tosha, kwa kifupi ni kwamba watanzania tutafute ufisadi mwingine wa EL uliomfanya akawa tajiri lakini si Richmond, hiyo ni ya JK kama sivyo na yeye alipaswa kujibu mapigo kwenye mkutano wa NEC lakini kwa kunyamaza inadhihirisha anahusika, kwani utajiri wa R1 wa haraka namna hiyo unatoka wapi??
kwa hiyo ulitaka mwenyekiti aanze kusutana na mjumbe mkutanoni sio?mdau pale sio kwenye baraza ya kahawa lazima ufahamu hilo lowassa yeye alikuwa ananung'unika tu wala hakuuliza swali lililohitaji majibu....
 
Usiwe mjinga wewe Kidatu, Lowasa anazo hatia kibao ila anajifanya mnjanja, ukisoma post za nyuma utaona!!!!!!Wacha huyu mwizi atoswe tumsahau, kwa nini unatetea mwizi lakini au huelewi wizi wake tukutajie???????????


Mbona umemstahi kamanda?ungemwambia asiwe mjinga kama mwanaume wao wa shoka lowassa ambae mwalimu nyerere alikua wa kwanza kumwita lowassa mjinga alipomwambia mzee kawawa na yeye asiwe "mjinga" kama lowassa!
 
Ndugu zangu Edward Ngoyay Lowassa ana dhamira ya dhati kuwa rais wa 5 wa Tanzania,na katika hili ana uhakika anashinda.Miaka 16 sasa ameitumia kujipanga na kutimiza ndoto yake.Miaka yote hiyo ameitumia kuweka watu wake katika chama,serikalini,idara ya usalama wa taifa na karibu katika kila nyanja!Watu hapa mnaotumika mtabisha lakin huo ndo ukweli!ametumia gharama kubwa na hayuko tayari dhamira yake hiyo ishindwe!Sie tulioko jikon tunayajua yote!Watanzania ni wazi Lowassa atakuwa rais wa nchi hii!!

Hoja:Rais ambaye amepigana na kupata wapinzani wengi katika kuufikia urais,je atatimiza matakwa ya wananchi?na kama watu wamempinga lakin amepigana na kuukwaa,nadharia ya pschology inasema mtu huyu ni mtu wa kutimiza matakwa yake!sasa matakwa ya mtu huyu ni yapi katika urais wake?na tudiscuss sasa!!!
 
katika gazeti la leom la tz daima lowassa ananukuliwa akisema:mwenyekiti utakumbuka kwamba mimi nilishaamua kuvunja mkataba huu wa Richmond,mapema lkn baada ya kuzungumza na wewe ukiwa nnje ya nchi ulisema tusubir ushauri wa makatibu wa wizara iweje leo nibebeshwe tuhuma hizi? Lowassa aliendelea kuuliza ni kitu gani ambacho alifanya bila rais kujua au kumwelkeza kufanya? kwa stahili hiinaamini Rais bado ana deni kwa jamii ya watz,pamoja na wasaidiz wake kujaribu kumnasua kwenye kashfa hii na pia kauli zake za maramara kuwa haijui Richmond hatimaye Lowassa amewaeleza watz kuwa kwenye jambo hili wewe ndo mhusika wa kwanza,lowassa ameamua kuutua mzigo alioubeba kwa mda mrefu,ni heri report hii irudi bungeni wahusika wote wahojiwe kama ni serikali ianguke:

nawasilisha
 
Hayati mwalimu Julius K.Nyerere Alishawahi kusema ''MTU ANAYEPAKIMBILIA IKULU NI WA KUMWOGOPA KAMA UKOMA'' na alidhibitisha maneno yake pale alipomkataa LOWASSA kwenye uraisi mwaka 1995! hivi Leo Huyu LOWASSA anautafuta uraisi kwa nguvu ya pesa huku akikumbushia baadhi ya mambo yake mazuri aliyoyafanya akiwa waziri mkuu!

Akumbuke sasa hivi Watanzania wameamka kama wananchi pale Ilemela mwanza walimkata DIALLO basi hicho ni kiashirio tosha kwamba sasa hivi wananchi hawaangalii una shs ngapi,C.V yako bali wanaaangalia uadilifu,msimamo na vision kama kiongozi! na
 
Wewe ni maghamba namba moja unamkaribisha Lowasa aende wapi,labda unayo CHADEMA nyingine!!!!!! Umesahau kuwa Mhs Slaa alisema akishika Urais Lowassa atakuwa wakwanza kutangulia lupango fisadi mkubwa!!!!!!!!!! Slaa hana uwezo wa kumpeleka Lowasa Mahakamani kwani Yeye na Mbowe ni wezi wakubwa sisi tuliopo chadema tunawafahamu. Mh Lowasa usisite kujiunga na Chama cha chadema kwani ni kimbilio la vijana na sio ngome ya wanafiki kama Slaa na mbowe karibi sana ili tuwatimue hawa wanafiki waende zao kwa magamba kwani wana hisa zao huku. Viongozi gani hawana misimamo mara wanamtambua JK mara NO, mara hawataki mswaada wa katiba mara tumekubaliana their very poor tunakuomba Lowasa ujinge nasi ili tuwe na kiongozi mwenye msimamo na mtendaji kama wewe Waziri Mkuu mstaafu utakayekumbukwa daima katika taifa la bongo
 
kuna taharifa kwamba siku ya mkutano wa NEC,Vyumba vingi vya wahariri wa Habari waliweza kumsikia live kutoka Dodoma kwa planned IT technology na ni kipind kile tu yeye anaongea!!hiyo yote ni kwamba aweze kusikika neno kwa neno habari ilipotiwe kama ilivyokuwa planned!!
FEDHA HAISHINDWI KITU!!!!!ENDELEA!!UEPIGA HATUA KATIKA KUJISAFISHA
 
kuna taharifa kwamba siku ya mkutano wa NEC,Vyumba vingi vya wahariri wa Habari waliweza kumsikia live kutoka Dodoma kwa planned IT technology na ni kipind kile tu yeye anaongea!!hiyo yote ni kwamba aweze kusikika neno kwa neno habari ilipotiwe kama ilivyokuwa planned!!
FEDHA HAISHINDWI KITU!!!!!ENDELEA!!UEPIGA HATUA KATIKA KUJISAFISHA

What is wrong with this?
 
What is wrong with this?
kwani huoni kosa mambo ya kikao ni siri ya kwenye kikao,na kuna msemaji wa mambo yalnayojadiliwa kwenye kikao,,kilichofanywa ni ukosefu wa maadili kwani neno moja hutafsiriwa tofauti ikiwa kila mtu atasema
 
Lowassa hasafishiki hata kwa tenzi na mashairi pamoja na ngonjera pia muziki wa dansi!
 
Back
Top Bottom