Lowassa aikana Richmond, asema alijiuzulu kwa heshima ya serikali na chama chake!

Leo umejitahidi angalau kujieleza , hongera Fanya hivihivi kila mara
 
6: Makanisani Roman Catholic & Lutheran churches EL kashamaliza kazi, wanampenda na wengine mfano mzee wa upako, Anthony Lusekelo wazi wazi anampigia kampeni mapemaaaa.....
Askofu wa kanisa katoliki MZA aliwaambia waumini wake wakati wa kuendesha mchango kuwa "wakristo watakuwa tofali moja moja la kumjenga Lowassa!
 
Nakubaliana nawe Mr President. Nasikia pia upo muafaka kati ya wakatoliki na waprotestant kuwa Rais ajaye atoke kwa waprotestanti na si mwingine bali Lowassa ingawa mwanzoni walimtaka Sitta wakaja gundua hana msimamo. Sitta na kundi lake hawatakaa kimya. Wana mpango wa kuyaanika yote yaliyobaki kwenye ripoti ya Richmond hata kama yatamuumiza JK.
 
Nape ni mtu niliyemwaminia sana CCM kuwa ni asset kubwa yenye very bright futute, alipoanza kupuliza vuvuzela la kujivua gamba, kuna kitu nilimweleza humu humu jf, sasa kimetimia!.

Masikini Nape sio asset tena, ni liability!.

You are right Pasco.. i used to admire his political stand, tatizo lilianza alipoanza siasa uchwara!
 
na kwa mapenzi ya Mungu lowassa atakuwa rais wa ccm ila si wa tz. Jana si leo
 
Kuna siku watanzania watachoka kuchezewa kwa maneno ya kisiasa; Richmond siyo msukule inamilikiwa na mtu na kuna mtu kati yetu watz waliyeileta na kuhakikisha madudu yote yaliyofanyika yanafanikiwa. Huyo mtu pia siyo msukule; kwa jinsi hiyo hatuhitaji kuendelea kudanganywa kwa namna yoyote ile.
 
Nape & Chilligati wameingia cha kike, sasa ngoma itawarudia, wakubwa CCM wametamka wanapayuka, na JK kamjibu Sumaye kwamba watachukuliwa hatua za kinidhamu endapo Nape & Chilli watapatikana na makosa na kamati ya maadili juu ya kutukana wazi wazi kuhusu EL,
Ooohhh.... EL is so powerfuuuuuul....utamuuuu
 

unamtetea jk kama nani. Nilidhani na wewe ni radical. Hata FF anakushinda?
 
Usanii wa Jk utamfikisha pabaya. yaani yeye ndo aliyewaagiza akina nape wazunguke nchi nzima kuvua magamba kumbe Lowasa alijua kuwa hata yeye JK ni gamba. Labda Lowasa atuweke wazi hayo mafaili ya Mwakawago huko Zanzibar yalikuwa yanamhusu jk kwa tuhuma zipi ili watz tujue
 
Hii tuiite.... the come back of ENL!:A S-coffee:
 

ccm walishindwa nini kutumia vikao na kamati za maadili kumsema lowassa? Unaongea nini? Leo unasema baada ya miaka 15? Mkuu kuna maeneo mengi sana unajichanganya. Halafu sikujua kama najibu hoja yako kwa mara nyingine. Nasema bora kina FF
 
Lowasa anashangaza kidogo:
-Hakuyasema haya alipopewa nafasi na Sitta pale bungeni. Akaishia kuachia ngazi.
-Mbona anahusisha ya JK mwaka 1997 na yanayomkumba sasa yeye?
-Sitta na kundi lake wamalizie ripoti ya Richmond?
-Tuendelee na utaratibu wa kupewa Rais wa nchi na wenye fedha?
 

Kwa maana hiyo bunge liunde kamati ya kumchunguza kikwete na kashfa ya richmond, watanzania tuamke tushushe neti kumekucha tuikomboe nchi yetu tuhakikishe 2015 hawarudi ikulu watatumaliza!
HTML:
 
Hapa shida si Nape wala nani. hayo yalikuwa maadhimio na chama lkn kama kawaida yao ya kushindwa kufanya au kusimamia wanachokiamini, sasa wanageuka na kuwafanya wakina Nape waki hang.Nape kama anataka kuishi kwenye chama chao, hana budi kujifunza kuwa mnafiki. kaazi kwelikweli!
 
nilishasema tangu mwanzo jamani lowasa ndiye raisi wangu ajaye
 
Pamoja na yote hivi CCM wanataka kutuambia hawamjui alietenda kosa la Richmond?kama ni watendaji wachini kama anavyotuambia Lowasa je mbona sijasikia watendaji wa chini wamepelekwa mahakamani kutokana na sakata la Richmond? Ni nani aliyesababisha ufisadi wa Richmond?au hakuna,kama hayupo je hiyo tume ya Mwankyembe ilitoa ripoti gani kwa hiyo Mwankyembe na Tume yake walilidanganya bunge na wananchi?Hapa ni wazi kwamba CCM ni chama cha kifisadi naomba tuwe wakweli ndugu zangu,chama cha kifisadi hakiwezi kumkamata fisadi,hakiwezi kumfukuza fisadi na Serikali inayoundwa kutokana na chama cha kifisadi hakiwezi kuwashitaki mafisadi kwa sababu na chenyewe ni fisadi.Nilisema jana humu jukwaani hakuna anayeweza kumfukuza Lowasa CCM.mtakubali manenno yangu,hiyo gia ya suala Lowasa kurudishwa kwenye CC ni danganya toto,hiyo kamati ya maadili nani msafi humo atakaemwambia Lowasa toka CCM kwa kuwa wewe ni fisadi?sasa huko Dodoma sijui walienda kufanya nini kama tatizo kubwa la chama chao wamelitafutia gia ya kulizima.
 
aliyeliona jeneza hakulitumia, aliishia kulinunua, na aliyelitumia hilo jeneza hakulinunua wala hakuliona!
 
Haya ndiyo yaliyojiri ndani ya vikao vyao.
Lowasa aliwahi kuvunja ule mkataba maarufu wa City water wote tunakumbuka. Lowasa ametumia haki yake na apewe haki yake. By implication the Jk is part of the saga! I am very sorry!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…