Lowassa aikana Richmond, asema alijiuzulu kwa heshima ya serikali na chama chake!

Lowassa aikana Richmond, asema alijiuzulu kwa heshima ya serikali na chama chake!

Nape sioni kama kafanya kitu kibaya. Kama katibu mwenezi, alikuwa anafikisha ujumbe kwa wanachama wote juu ya yaliyoafikiwa kwenye kikao cha NEC cha April.Katika kikao cha Aprili NEC ilipitisha maazimio 26, lakini kubwa ni lile lililokuwa likihimiza vita dhidi ya ufisadi kuendelea na kutoa mwito kwa watu wanaotajwa na jamii kuhusika na ufisadi ambao wako ndani ya chama kujitathmini kisha kuchukua hatua za kuachia madaraka waliyonayo.
Azimio hilo pia lilieleza kwamba hao waliotuhumiwa wasipoachia madaraka chama kiwachukulie hatua mara moja.
Kwa maoni yangu naona alichokuwa akikifanya Nape ni kitu sahihi kabisa, ndio maana kila mtu alikaa kimya na hamna aliyemzuia.
Leo umejitahidi angalau kujieleza , hongera Fanya hivihivi kila mara
 
6: Makanisani Roman Catholic & Lutheran churches EL kashamaliza kazi, wanampenda na wengine mfano mzee wa upako, Anthony Lusekelo wazi wazi anampigia kampeni mapemaaaa.....
Askofu wa kanisa katoliki MZA aliwaambia waumini wake wakati wa kuendesha mchango kuwa "wakristo watakuwa tofali moja moja la kumjenga Lowassa!
 
Hadi sasa Lowassa njia nyeupeeee for Presidential candidate wa CCM 2015, na 7bu zipo wazi, read this
1. Mkapa alifurahia wakati Lowassa anaongea, meaning Ben is supporting EL, signs are clear
2: Sumaye, another powerful political leader & rich dude, wazi wazi anam support Lowassa tena kasema wakina Nape na Chilligati wachukuliwe hatua
3. Mzee Kingunge yupo 100% upande wa Lowassa, na ni baada ya kujua ukweli halisia kuhusu tuhuma dhidi ya EL are fake, publicized tu.
4: Hapa niseme JK yupo na Lowassa 100% na hawezi kuongea hadharani kwa nafasi alionayo sasa, ila dalili na matendo yapo clear, JK hadharani hajawahi mshutumu EL hata siku moja, hadi sasa ni marafiki....
5: EL ana support ya all rich dudes, Rostam, Karamagi, Chenge, na support kubwa hasa si kwa hawa financial power house wa CCM bali Wanachama wa CCM wanampenda saaaana, yaani leo NEC, CC, na wajumbe wa mikoa wa CCM, Lowassa ni lulu, signs are clear
6: Makanisani Roman Catholic & Lutheran churches EL kashamaliza kazi, wanampenda na wengine mfano mzee wa upako, Anthony Lusekelo wazi wazi anampigia kampeni mapemaaaa.....

What i see now & days to come-----
EL hana mpinzani CCM hadi sasa, na wazee wa CCM tayari wamemkubali, EL ni Field Marshall wa siasa za hapa TZ na atashinda Urais, ngojeni muoneee....
Nakubaliana nawe Mr President. Nasikia pia upo muafaka kati ya wakatoliki na waprotestant kuwa Rais ajaye atoke kwa waprotestanti na si mwingine bali Lowassa ingawa mwanzoni walimtaka Sitta wakaja gundua hana msimamo. Sitta na kundi lake hawatakaa kimya. Wana mpango wa kuyaanika yote yaliyobaki kwenye ripoti ya Richmond hata kama yatamuumiza JK.
 
Nape ni mtu niliyemwaminia sana CCM kuwa ni asset kubwa yenye very bright futute, alipoanza kupuliza vuvuzela la kujivua gamba, kuna kitu nilimweleza humu humu jf, sasa kimetimia!.

Masikini Nape sio asset tena, ni liability!.

You are right Pasco.. i used to admire his political stand, tatizo lilianza alipoanza siasa uchwara!
 
Kuna siku watanzania watachoka kuchezewa kwa maneno ya kisiasa; Richmond siyo msukule inamilikiwa na mtu na kuna mtu kati yetu watz waliyeileta na kuhakikisha madudu yote yaliyofanyika yanafanikiwa. Huyo mtu pia siyo msukule; kwa jinsi hiyo hatuhitaji kuendelea kudanganywa kwa namna yoyote ile.
 
Nape & Chilligati wameingia cha kike, sasa ngoma itawarudia, wakubwa CCM wametamka wanapayuka, na JK kamjibu Sumaye kwamba watachukuliwa hatua za kinidhamu endapo Nape & Chilli watapatikana na makosa na kamati ya maadili juu ya kutukana wazi wazi kuhusu EL,
Ooohhh.... EL is so powerfuuuuuul....utamuuuu
 
Uchungu wa kiume huujui...remember JK is our President..

Pili, hapa Lowassa anataka kujikosha na najua fika kwamba mwaka 1995 JK alimshinda Mkapa, pengine JK alikuwa na mpango wa Mapinduzi 1997 ama kuhama chama... ama hasira na Nyerere. Hivyo taarifa ilipomfikia Mkapa toka kwa Daudi Mwakawago Mungu amrehemu ndio maana kafa maskini kwa uzalendo wake - Mkapa akiwa rais akapuuza. sasa kimbelembele cha Lowassa ni kutaka kumtahadharisha JK wakati huyu ni President, yeye nani?.

Aaaaah samahani nimesahau wewe shabiki sii mchezaji!

unamtetea jk kama nani. Nilidhani na wewe ni radical. Hata FF anakushinda?
 
Usanii wa Jk utamfikisha pabaya. yaani yeye ndo aliyewaagiza akina nape wazunguke nchi nzima kuvua magamba kumbe Lowasa alijua kuwa hata yeye JK ni gamba. Labda Lowasa atuweke wazi hayo mafaili ya Mwakawago huko Zanzibar yalikuwa yanamhusu jk kwa tuhuma zipi ili watz tujue
 
Mkuu ni mawazo yako ukiwa mwanachama wa CCM sisi tunatazama tambala hili kutoka nje...Nape kafanya kazi alokabidhiwa na hakuwa mjinga kuinuka na kutaka Lowassa ajiuzulu pasipo kuwepo na maagizo ya kichama ama toka juu. Alipewa kazi hii makhsusi ili kumwangusha kisiasa kazi ambayo CCM ni wazuri sana kuwapa watu madaraka pale wanapojua watashindwa kutiiza..Kwanza vita kubwa ya ndani ni vijana ambao ni tishio kwa vizee vilivyokaa miaka nenda rudi nao walivyo mazuba wanakubali kuendeshwa kwa jina la bendera.

Halafu Lowassa kwa nini ayazungumze haya ya miaka 15 iliyopita katika mkutano wa CC hali angeweza kabisa kumkumbusha JK kwa barua ama wakiwa faragha. Kilitokea nini mwaka 1997 mbona hamsemi isipokuwa mnatuacha sisi tukisie tu kwamba JK alifanya jambo baya sana ambalo lingemwigiza matatizoni na yeye kama mshauri wa Mkapa aliweza kuyapoza.. Ati Leo asingekuwepo!...Wewe Mungu? na ndio majibu ya JK kulingana na imani yake Sii Mkapa wala Lowassa ambaye angeweza kuhukumu destiny yake..

Hii ni kashfa kubwa sana kwa rais wetu hayo makundi yenu nyuma ya Lowassa mtakuja jimaliza zaidi na beleive me JK haja solve kitu. Watanzania kwa ujumla wetu hatudanganyiki na watu wanaokitawala chama kuja vunjia heshima kiongozi wa Taifa ktk mkutano, maneno ambayo hakuna kiongozi yeyote mwenye uthubutu wa kuyasema kama sii kumtishia rais kitu gani...

Nape walitishia kuondoka na kuunda CCJ kwa sababu walipinga Ufisadi wa baadhi ya watu, leo nyie mnawakumbatia na kuwaita washujaa (mnanunuliwa kwa shanga) ati hawa waloona mabaya ni wasaliti.. Poleni sisi wengine tulishaondoka CCM zamani na wala hatuoni usaliti bali tunaitafuta haki na utawala unaojali maslahi ya Taifa.. Siasa za kubebana sii uzalendo wala utiifu bali ni ujinga, uroho na ulimbukeni..

Mwisho wa yote amefanikiwa kuyapata aloyataka na JK kavunja kikao cha Mafisadi na hivyo kumpa ruksa Lowassa kuanza kutimiza hasira yake maanake hamumjui huyu mtu alivyo na roho mbaya na visasi - Atawachafua kuliko kila kiti..Huyo Mtoto wa Mkulima unayemdharau ndiye kawashika wengi viongozi laa sivyo wengi wangekwisha malizwa na EL..Ni ushauri wangu tu mnaweza uchukua ama kuuacha lakini CCM haikuwa na matatizo haya kabla ya Lowassa kuwa na nguvu hii ndani ya chama.

ccm walishindwa nini kutumia vikao na kamati za maadili kumsema lowassa? Unaongea nini? Leo unasema baada ya miaka 15? Mkuu kuna maeneo mengi sana unajichanganya. Halafu sikujua kama najibu hoja yako kwa mara nyingine. Nasema bora kina FF
 
Lowasa anashangaza kidogo:
-Hakuyasema haya alipopewa nafasi na Sitta pale bungeni. Akaishia kuachia ngazi.
-Mbona anahusisha ya JK mwaka 1997 na yanayomkumba sasa yeye?
-Sitta na kundi lake wamalizie ripoti ya Richmond?
-Tuendelee na utaratibu wa kupewa Rais wa nchi na wenye fedha?
 
Watanzania sasa amua wenyewe. Lowassa kwa mara nyingine amemshinda Kikwete je Bunge letu litaendelea kuchekelea kwa vile wote ni nyani wana mikia?
Haya chini ni maneno mazito aliyomwaga Lowassa akiamua kumwaga mboga baada ya Kikwete kutaka kumwaga ugali.

“Mwenyekiti utakumbuka kwamba mimi nilishaamua kuvunja mkataba wa Richmond mapema, lakini baada ya kukupigia simu ukiwa katika safari nje ya nchi ulisema tusubiri kwani ulikuwa umepata ushauri wa makatibu wakuu wa wizara, sasa leo hii ninahukumiwa nakuitwa fisadi kwanini?”.

“Nilijiuzulu kuwajibika kwa ajili ya kuilinda Serikali yangu na kwa heshima ya chama changu, sasa kwanini leo nahukumiwa kwa jambo hili, tena natukanwa na wana CCM wenzangu na siyo wapinzani nchi nzima kwamba mimi eti fisadi?,”alinukuliwa akihoji Lowassa.

Kadhalika kada huyo wa CCM alinukuliwa akimkumbusha Rais Kikwete kwamba: “Mwenyekiti nikukumbushe mwaka 1997 kule Zanzibar, kina Mzee Daudi Mwakawago walikuja na mafaili yakiwa na tuhuma dhidi ya mtizamo hasi wa jamii dhidi yako, kwa hiyo wakati ule kama si busara za kina Mzee Mkapa (Benjamin) leo usingekuwa hapo ulipo”.


Kwa maana hiyo bunge liunde kamati ya kumchunguza kikwete na kashfa ya richmond, watanzania tuamke tushushe neti kumekucha tuikomboe nchi yetu tuhakikishe 2015 hawarudi ikulu watatumaliza!
HTML:
 
Hapa shida si Nape wala nani. hayo yalikuwa maadhimio na chama lkn kama kawaida yao ya kushindwa kufanya au kusimamia wanachokiamini, sasa wanageuka na kuwafanya wakina Nape waki hang.Nape kama anataka kuishi kwenye chama chao, hana budi kujifunza kuwa mnafiki. kaazi kwelikweli!
 
Pamoja na yote hivi CCM wanataka kutuambia hawamjui alietenda kosa la Richmond?kama ni watendaji wachini kama anavyotuambia Lowasa je mbona sijasikia watendaji wa chini wamepelekwa mahakamani kutokana na sakata la Richmond? Ni nani aliyesababisha ufisadi wa Richmond?au hakuna,kama hayupo je hiyo tume ya Mwankyembe ilitoa ripoti gani kwa hiyo Mwankyembe na Tume yake walilidanganya bunge na wananchi?Hapa ni wazi kwamba CCM ni chama cha kifisadi naomba tuwe wakweli ndugu zangu,chama cha kifisadi hakiwezi kumkamata fisadi,hakiwezi kumfukuza fisadi na Serikali inayoundwa kutokana na chama cha kifisadi hakiwezi kuwashitaki mafisadi kwa sababu na chenyewe ni fisadi.Nilisema jana humu jukwaani hakuna anayeweza kumfukuza Lowasa CCM.mtakubali manenno yangu,hiyo gia ya suala Lowasa kurudishwa kwenye CC ni danganya toto,hiyo kamati ya maadili nani msafi humo atakaemwambia Lowasa toka CCM kwa kuwa wewe ni fisadi?sasa huko Dodoma sijui walienda kufanya nini kama tatizo kubwa la chama chao wamelitafutia gia ya kulizima.
 
aliyeliona jeneza hakulitumia, aliishia kulinunua, na aliyelitumia hilo jeneza hakulinunua wala hakuliona!
 
Mkuu ebu acheni Ujinga wengine hapa tunatumia akili na sii masaburi... Sasa kama habari hii ni yakweli.. Lowassa alijuaje na kutaka kuuvunja mkataba ikiwa mkataba ulikuwa wa JK rais wake....Halafu JK kusema tu alikuwa akipata ushauri wa makatibu wake (watendaji wa kiserikali) inaonyesha wazi JK alikuwa akifuata sheria na taratibu za kiserikali laa sivyo asingewahusisha makatibu wakuu kama alivyofanya Lowassa na ushahidi upo akiwaamrisha hao makatibu na waziri wafuate maagizo yake....Tafuta jingine!

Hayo ya 1997 we are interested ni kujikosha na kutafuta huruma za JK...Hata mahakamani mkosa baada ya kupatikana na kmakosa, hupewa muda wa kuomba, kujieleza kabla ya kuhukumiwa kifungo..
Haya ndiyo yaliyojiri ndani ya vikao vyao.
Lowasa aliwahi kuvunja ule mkataba maarufu wa City water wote tunakumbuka. Lowasa ametumia haki yake na apewe haki yake. By implication the Jk is part of the saga! I am very sorry!
 
Back
Top Bottom