Lowassa aikana Richmond, asema alijiuzulu kwa heshima ya serikali na chama chake!

Lowassa aikana Richmond, asema alijiuzulu kwa heshima ya serikali na chama chake!

Kwa lipi FairPlayer! Haya kapata nafasi kuyasema jana tangu 2006?
- Alimpigia simu JK ili avunje mkataba. JK akamkatalia. Kwa nini asijiuzulu wakati huo?
- Kule kuisafisha kashfa hii kwa kutumia TAKUKURU yetu kulifanywa na nani?
-Alipewa nafasi tele na Sitta tena yenye kinga kamili. Akaiacha. Kaamkia NEC jana!
- Mwambie afunguke zaidi. Anadai katukanwa. Aende hata mahakamani angalau.

my dad was correct whe he said '' we have the president who cannot think beyond the next meal''

De'Levis,

Humu JF wengi ni mashabiki. Lowassa ni mchapa kazi wote tunajua, kile kipindi cha CRISIS hata wewe ungeweza kufanya maamuzi yasiyo sahihi. Na hiyo ndo kazi ya kiongozi kutoa maamuzi mazito. Sasa kumbe ilikua ni collective accountability. Akaamua kumwacha Prez akawa muungwana.

Leo kwa sababu za matumbo yetu tunamtukana huyu mtu shujaa wetu. Chenge kakamatwa na hela WAZI kabisaaaaa sijawahi kusikia rafiki yangu HALISI akimsema ni fisadi. Why Lowassa!

MWEMBE WENYE MAEMBE NDO UNARUSHIWA MAWE. LOWASSA ANAFAA NDIO MAANA MNAMPINGA.

Duh!
 
Duh kami ni picha nadani hapo ndo inaanza, tuendelee kutazama, kumbe jk ndo injinia wa yote?
 
De'Levis,

Humu JF wengi ni mashabiki. Lowassa ni mchapa kazi wote tunajua, kile kipindi cha CRISIS hata wewe ungeweza kufanya maamuzi yasiyo sahihi. Na hiyo ndo kazi ya kiongozi kutoa maamuzi mazito. Sasa kumbe ilikua ni collective accountability. Akaamua kumwacha Prez akawa muungwana.

Leo kwa sababu za matumbo yetu tunamtukana huyu mtu shujaa wetu. Chenge kakamatwa na hela WAZI kabisaaaaa sijawahi kusikia rafiki yangu HALISI akimsema ni fisadi. Why Lowassa!

MWEMBE WENYE MAEMBE NDO UNARUSHIWA MAWE. LOWASSA ANAFAA NDIO MAANA MNAMPINGA.

Duh!
-Awaombe radhi kwanza WATANZANIA kwa maamuzi hayo.
-Lowasa, mbali ya kuchapa kazi ni mwizi pia. Na wezi wote ni wachapakazi sana.
-Kwa nini ametuficha ukweli wote wa kashfa hii?
-Mwaka 1995 alichukua fomu ya kugombea Urais. Nini kilitokea?
 
mkuu Wilcard,

Kama ni rahisi hivyo basi Mwakyembe asingekua mgonjwa hivi sasa. Pia umesahau maadili na viapo vya baraza la mawaziri etc.

Sikutegemea yale maswali kutoka kwako kwa kweli maana umo humu muda mrefu.

Ila tutaendelea kufundishana kama kawa. Siasa sio kama uonavyo wewe au usomavyo kwenye magazeti.

Unafahamu maana ya neno PROPAGANDA?
 
-Awaombe radhi kwanza WATANZANIA kwa maamuzi hayo.
-Lowasa, mbali ya kuchapa kazi ni mwizi pia. Na wezi wote ni wachapakazi sana.
-Kwa nini ametuficha ukweli wote wa kashfa hii?
-Mwaka 1995 alichukua fomu ya kugombea Urais. Nini kilitokea?

Mkuu ni password yako kweli?. Maana naona unafikiri kama mtu magazeti yanamfikiria. Yaani vitu vinachujwa na kisha unamezeshwa!

Think a little bit basi.
 
Kama kuna kaukweli hivi!!!

Aliposikia Mwakyembe mgonjwa akawahi haraka haraka .....kumjulia Hali as if alikuwa miezi yote mitatu anayougua hajuwi.....Tabia typical ya wachawi....
Mwakyembe na manyanya watajuta sana kumfanyia kazi mtu ambaye hata kuwatetea hawezi......sana sana kuwakana....
 
Mkuu ni password yako kweli?. Maana naona unafikiri kama mtu magazeti yanamfikiria. Yaani vitu vinachujwa na kisha unamezeshwa!

Think a little bit basi.
Jibu FairPlayer. Hakuna mtu anayejua kuvitumia vyombo vya habari kama Lowasa. Mjanja sana wewe. Hakuna nilichomezeshwa. Sema tu neno moja na roho yangu itapona.
 
Lowassa amekana rasmi kuwa yeye hahusiki na mkataba wa Richmond!

images

Nanukuu:

Mwisho wa kunukuu

Hii leo si sahihi hata yeye (Lowassa) kuhukumiwa kwa kuzingatia kile kinachodaiwa kuwa ni mtizamo wa umma dhidi yake unaompa sura ya ufisadi, jambo ambalo amedai kwamba siyo la kweli.

Chanzo: Mwananchi
Sijui mnanengeneka na nini na huyu mwizi mkubwa!alijua hayo yote sasa alisaidia nini kama waziri mkuu na mzalendo???hivi mitanzania ina akili gani au amewapa mgao!?

Hili jamaa jizi hata sioni sababu ya kulitetea, mpanga mipango na mtekeleza mipango wote wa atia, then huwezi tekeleza mpango bila malipo sasa mbona hayo hayasemi?

Jizi kubwa hili acheni umawazo mgando!
 
Watanzania sasa amua wenyewe. Lowassa kwa mara nyingine amemshinda Kikwete je Bunge letu litaendelea kuchekelea kwa vile wote ni nyani wana mikia?
Haya chini ni maneno mazito aliyomwaga Lowassa akiamua kumwaga mboga baada ya Kikwete kutaka kumwaga ugali.

"Mwenyekiti utakumbuka kwamba mimi nilishaamua kuvunja mkataba wa Richmond mapema, lakini baada ya kukupigia simu ukiwa katika safari nje ya nchi ulisema tusubiri kwani ulikuwa umepata ushauri wa makatibu wakuu wa wizara, sasa leo hii ninahukumiwa nakuitwa fisadi kwanini?".

"Nilijiuzulu kuwajibika kwa ajili ya kuilinda Serikali yangu na kwa heshima ya chama changu, sasa kwanini leo nahukumiwa kwa jambo hili, tena natukanwa na wana CCM wenzangu na siyo wapinzani nchi nzima kwamba mimi eti fisadi?,"alinukuliwa akihoji Lowassa.

Kadhalika kada huyo wa CCM alinukuliwa akimkumbusha Rais Kikwete kwamba: "Mwenyekiti nikukumbushe mwaka 1997 kule Zanzibar, kina Mzee Daudi Mwakawago walikuja na mafaili yakiwa na tuhuma dhidi ya mtizamo hasi wa jamii dhidi yako, kwa hiyo wakati ule kama si busara za kina Mzee Mkapa (Benjamin) leo usingekuwa hapo ulipo".

Hapa Lowassa ameamua kuueleza umma kabisa kwamba matatizo ya Tanzania mengi yamesababishwa na Rais Kikwete. Na si hivyo tu bali ametaka umma ujue kwamba Kikwete tokea mwanzo alikuwa na matatizo na ndio maana ametoa point hiyo ya Mzee Mwakawago,

Siwezi kumtetea Lowassa lakini kwa akili za kiutu uzima nilizo nazo naweza kuchanganua kwamba Kikwete hana ujanja mbele ya Lowassa na vile vile Kikwete aliamua kuzima topic ili asiendelee kuaibika.

Labda kwa wale wenzetu wenye uwezo wa kuweka bayana yale yaliyo zungumzwa na wakina Daudi Mwakawago kuhusu Kikwete watutupie hapa ili na sisi tuendelee kuisoma nyakati ya Rais wetu..
 
sijui mnanengeneka na nini na huyu mwizi mkubwa!alijua hayo yote sasa alisaidia nini kama waziri mkuu na mzalendo???hivi mitanzania ina akili gani au amewapa mgao!???hili jamaa jizi hata sioni sababu ya kulitetea, mpanga mipango na mtekeleza mipango wote wa atia, then huwezi tekeleza mpango bila malipo sasa mbona hayo hayasemi????jizi kubwa hili acheni umawazo mgando!

Si utoe ushahidi wa wizi mkuu !! Mmepewa muda na nafasi kuwasilisha ushahidi wenu !!! Mangapi yana mtoa machozi Pinda na hajaweza fanya lolote la maana zaidi ya kwenda panda Karanga kijijini kwake...!!!
 
ngoma inogile asante mkuu kwa update maana huku kwetu hakuna access ya magazeti..well said lowasa aka kondoo wa kafara naamini lowasa ana mengi zaidi ya hayo..

lowassa kwaheri,kurudisha cc ndio jambo lililokuwa likitakiwa kwa kuwa nec unazo nguvu nyingi,sasa cc kule huna watu mzee,kwa heri
 
lowassa kwaheri,kurudisha cc ndio jambo lililokuwa likitakiwa kwa kuwa nec unazo nguvu nyingi,sasa cc kule huna watu mzee,kwa heri

hata hao cc hawana jeuri kwani wameambiwa walete ushaidi wa tuhuma zake na ikithibitika siyo kweli waliyomchafua wachukuliwe hatua za kinidhamu.
 
Wameniudhi sana NEC ya CCM. Badala ya kuikabidhi dola watuhumiwa wa ufisadi ili sheria ichukue mkondo wake wao wanalirudisha suala hili kwenye CC yao. Tumefikaje hapa pa kubembeleza wahalifu kiasi hiki? Waachieni akina Mramba basi ah!

Unategemea Rais atajikabithi kwa dola mkuu , Umeshatafuniwa kila kitu hapo na tena si kama wafanyavyo wana siasa wengine kukutana na waandishi wa habari, Lowassa kaamua kusema wazi mbele ya Rais kwamba yeye ndio chanzo.
 
De'Levis,

Humu JF wengi ni mashabiki. Lowassa ni mchapa kazi wote tunajua, kile kipindi cha CRISIS hata wewe ungeweza kufanya maamuzi yasiyo sahihi. Na hiyo ndo kazi ya kiongozi kutoa maamuzi mazito. Sasa kumbe ilikua ni collective accountability. Akaamua kumwacha Prez akawa muungwana.

Leo kwa sababu za matumbo yetu tunamtukana huyu mtu shujaa wetu. Chenge kakamatwa na hela WAZI kabisaaaaa sijawahi kusikia rafiki yangu HALISI akimsema ni fisadi. Why Lowassa!

MWEMBE WENYE MAEMBE NDO UNARUSHIWA MAWE. LOWASSA ANAFAA NDIO MAANA MNAMPINGA.

Duh!

nyie semeni yote lakini kama suala limepelekwa kamati kuu lowassa bai bai....!kila mtu anajua richmond ni ya swahiba wake rostam aziz,huo ndio ukweli,anavyotapa tapa watu wanamtizama tu lakini gamba lazima limvuke hana ujanja!hiyo ndio siasa
 
Kwa taarifa tu baada ya ripoti hiyo ya mwaka 1997 iliyotolewa na Daud Mwakawago, huyo Daud Mwakawago hatunaye tena, yupo ahera.

Hii ni kweli Mkuu...!The deceased's brother, Mr Yassin Mwakawago, said that Ambassador Mwakawago died at the Aga Khan Hospital in Dar es Salaam where he was admitted for the past nine days battling malaria and pneumonia.

"It is true that we lost our brother this morning (yesterday).He was suffering from malaria and in the process he developed breathing difficulties and he had to breathe by the aid of machine until this morning when he died," he said.

Halafu ugonjwa wenyewe mpaka kupelekea kifo chake ni kazi kweli kweli..!!!
 
hata hao cc hawana jeuri kwani wameambiwa walete ushaidi wa tuhuma zake na ikithibitika siyo kweli waliyomchafua wachukuliwe hatua za kinidhamu.

ukitaka ushahidi basi hata rostam aziz asafishwe....wewe uko tayari kumsafisha?kama la kwanini rostam umuone mchafu bila ushahidi na lowassa ndio uhitaji ushahidi wa mahakamani?yule kwisha habari yake kuna kina mwakawago wengine huko cc ndio watakuja na mafaili yake ya jinsi wananchi wasivyokuwa na imani nae!
 
Sasa Lowassa ataeleweka kwa msemo wake kuwa 'hakukutana na Kikwete barabarani.'
 
Back
Top Bottom