Kwa wale wanaoshangilia "ushindi" wa lowassa baada ya suala lake la kuvuliwa gamba pamoja na suala la Nape na chiligati anaowalalamikia kuzunguka nchi nzima "kumchafua" kutinga mikononi mwa kamati kuu,leo nataka kuwakumbusha kidogo kuhusu Jakaya ili huku mkifurahia "ushindi" pia mumfahamu sawa sawa muungwana jakaya ni mtu wa dizaini gani,sina lengo la kutia mchanga kwenye kitumbua chenu cha furaha la hasha ila nataka tukumbushane muijua siasa pia.Wandugu wapendwa mnajua ilikuwaje mpaka Lowassa akawa sio waziri mkuu.....
Kiufupi ni Kwamba Lowassa aliingizwa choo cha stendi na Jakaya!
Lowassa aliutema uwaziri mkuu anaoupenda mpaka leo kutokana na utoto wa mjini" utapeli wa kisiasa wa Rais Kikwete kwa swahiba wake Lowassa, wala haikua "ajali ya kisiasa".
Mpango mzima ulikua hivi:
Bunge kupitia Kamati Teule ilisoma ripoti yake kupitia mwenyekiti wake, Dk. Harrison Mwakyembe. Hali ilikuwa tete Dodoma na hata Chamwino ambako Rais Kikwete alikuwa amejichimbia.
Baada ya kusomwa kwa ripoti, taarifa zinasema Lowassa alikwenda Chamwino kuonana na bosi wake ili kupanga mkakati wa kuzima maasi ya wabunge wa CCM waliokuwa wamesisimka ili kummaliza Lowassa, rais Kikwete na serikali yao.
Katika mazungumzo yao usiku ule, Rais Kikwete na swahiba wake huyo wa zamani; Lowassa akapendekeza eti jk aende upesi kukutana na wabunge wa CCM ili kuwaonya wasiiangushe serikali yao, Jk baada ya "kupima" akastuka.
Ndipo yeye akaja na maarifa ya kimjini kwa kumwambia Lowassa aandike barua ya kujiuzuru, halafu yeye jk aicheleweshe kuijibu hiyo barua kwa makusudi mpaka Bunge lihairishwe ili kumpa nafasi yeye jk kama rais kuonana na wabunge wa CCM ili kuzima maasi ya wabunge kabla ya mkutano mwingine wa Buge wa Aprili haujafanyika Dodoma.
Lowassa na ujanja wake wote eti nae bila ajizi aliamini na kuandika barua ya kuigiza kujiuzuru na kisha akaondoka kurudi Dodoma mjini usiku ule. Yaliyotokea Chamwino baada ya Lowassa kuondoka inabakia kuwa siri ya Kikwete mwenyewe na aliokutana nao. Usiku wa manane wa siku hiyo, Rais Kikwete aliamua kuwa barua ile ijibiwe na kukubaliwa. Ni kinyume na makubaliano yake ya awali na Lowassa!
Sasa leo tena suala la lowassa baada ya kupata kibali cha NEC liko mikononi mwa kamati kuu ambamo lowassa hayumo!Na watu wake eti wanashangilia "ushindi" wa ice cream iliyowekwa juani huku jakaya akiwa tayari amejeruhiwa na kutajwa kwenye sakata la richmond na pia ikikumbukwa Jakaya hana tena cha kupoteza kwa kuwa hawezi tena kuwa rais!mi nawaomba msiwe wajinga kama jamaa yenu kwa mujibu wa mwalimi nyerere ambae alifahamu ujinga wake zamani kabla kabla ya jk kuja kuthibitisha kwa kumuingiza choo cha stendi!!!!!!!!!!!!!!!!!!