Lowassa aikana Richmond, asema alijiuzulu kwa heshima ya serikali na chama chake!

Lowassa aikana Richmond, asema alijiuzulu kwa heshima ya serikali na chama chake!

Waberoya wewe huyo? nendeni taratibu...

Heee kumbe waberoya nae kaingia kichwa kichwa kuamini lowassa kweli amepona kuvuliwa gamba?!!basi watu yaelekea huwa hamfuatilii mambo!wabaya wote wa lowassa walikuwa wanaomba usiku kucha suala la kujivua gamba baada ya kushindikana kwa hiyari liachiwe kamati kuu lakini baada ya kupata kibali cha nec!sasa hapo nani mshindi mnavyodhani??wabaya wa lowassa ama lowassa??maana kibali kimeshatoka na watu mnajifanya mmesahau hiyo badala yake mmekazania kulia lia kwa lowassa ili jumba bovu lisimuangukie peke yake!haitasaidia alitakiwa azicheze karata zake vizuri suala hilo lizimwe kwa nec kugoma kutoa kibali,kachemsha kampa rungu mwenyekiti atambe na kamati kuu yake anayoimudu vyema!
 
Lowassa ni chaguo la Mungu...
tuombe uzima mpaka 2015 atakaposhinda ktk uchaguzi na kututoa huku ktk nchi ya utumwani na kutupeleka ktk nchi ya kanani...
Tuseme inshaalah
 
Kwa wale wanaoshangilia "ushindi" wa lowassa baada ya suala lake la kuvuliwa gamba pamoja na suala la Nape na chiligati anaowalalamikia kuzunguka nchi nzima "kumchafua" kutinga mikononi mwa kamati kuu,leo nataka kuwakumbusha kidogo kuhusu Jakaya ili huku mkifurahia "ushindi" pia mumfahamu sawa sawa muungwana jakaya ni mtu wa dizaini gani,sina lengo la kutia mchanga kwenye kitumbua chenu cha furaha la hasha ila nataka tukumbushane muijua siasa pia.Wandugu wapendwa mnajua ilikuwaje mpaka Lowassa akawa sio waziri mkuu.....

Kiufupi ni Kwamba Lowassa aliingizwa choo cha stendi na Jakaya!
Lowassa aliutema uwaziri mkuu anaoupenda mpaka leo kutokana na "utoto wa mjini" utapeli wa kisiasa wa Rais Kikwete kwa swahiba wake Lowassa, wala haikua "ajali ya kisiasa".

Mpango mzima ulikua hivi:

Bunge kupitia Kamati Teule ilisoma ripoti yake kupitia mwenyekiti wake, Dk. Harrison Mwakyembe. Hali ilikuwa tete Dodoma na hata Chamwino ambako Rais Kikwete alikuwa amejichimbia.
Baada ya kusomwa kwa ripoti, taarifa zinasema Lowassa alikwenda Chamwino kuonana na bosi wake ili kupanga mkakati wa kuzima maasi ya wabunge wa CCM waliokuwa wamesisimka ili kummaliza Lowassa, rais Kikwete na serikali yao.
Katika mazungumzo yao usiku ule, Rais Kikwete na swahiba wake huyo wa zamani; – Lowassa akapendekeza eti jk aende upesi kukutana na wabunge wa CCM ili kuwaonya wasiiangushe serikali yao, Jk baada ya "kupima" akastuka.
Ndipo yeye akaja na maarifa ya kimjini kwa kumwambia Lowassa aandike barua ya kujiuzuru, halafu yeye jk aicheleweshe kuijibu hiyo barua kwa makusudi mpaka Bunge lihairishwe ili kumpa nafasi yeye jk kama rais kuonana na wabunge wa CCM ili kuzima maasi ya wabunge kabla ya mkutano mwingine wa Buge wa Aprili haujafanyika Dodoma.
Lowassa na ujanja wake wote eti nae bila ajizi aliamini na kuandika barua ya "kuigiza" kujiuzuru na kisha akaondoka kurudi Dodoma mjini usiku ule. Yaliyotokea Chamwino baada ya Lowassa kuondoka inabakia kuwa siri ya Kikwete mwenyewe na aliokutana nao. Usiku wa manane wa siku hiyo, Rais Kikwete aliamua kuwa barua ile ijibiwe na kukubaliwa. Ni kinyume na makubaliano yake ya awali na Lowassa!

Sasa leo tena suala la lowassa baada ya kupata kibali cha NEC liko mikononi mwa kamati kuu ambamo lowassa hayumo!Na watu wake eti wanashangilia "ushindi" wa ice cream iliyowekwa juani huku jakaya akiwa tayari amejeruhiwa na kutajwa kwenye sakata la richmond na pia ikikumbukwa Jakaya hana tena cha kupoteza kwa kuwa hawezi tena kuwa rais!mi nawaomba msiwe wajinga kama jamaa yenu kwa mujibu wa mwalimi nyerere ambae alifahamu ujinga wake zamani kabla kabla ya jk kuja kuthibitisha kwa kumuingiza choo cha stendi!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
lol........kumbe siku hizi ni choo cha stendi?sio cha kike???lol..........
 
Lowassa ni chaguo la Mungu...
tuombe uzima mpaka 2015 atakaposhinda ktk uchaguzi na kututoa huku ktk nchi ya utumwani na kutupeleka ktk nchi ya kanani...
Tuseme inshaalah

Labda mungu wa manyani!
 
Jakaya ana cha kupoteza, Urais kabla ya muda wake, manake msambaratiko wa ccm ni uchaguzi mwingine haraka. What about Jela kwa saga la richmond kwa rais ajaye unaliona?? things might get tough more than you think.
 
Lowasa hana makosa, hakutendewa haki hata kidogo. Tuishi kwa kumuogopa Mungu, kama kuna kundi linapanga njama chafu mbele ya kiumbe cha Mungu kisicho na makosa, basi subiri uuone jinsi ukweli utakavyojitenga na uwongo. Nuru na giza havitakaa pamoja hata siku moja. Lowasa atashinda kwa hili nina hakika 110%
 
we uko nchi gani bwana...huyo rais gani atakaempeleka gerezani mwenzake katika tanzania hii???na asimalize muda wake wa katiba ipi hasa itakayomtoa madarakani?labda jeshi liasi,wabongo kwa kupenda ku create fear isiyokuwepo hatujambo,tuliambiana hapa oooh jk akishika madaraka mkapa atanyea debe!kiko wapi?kwa mfumo wa ccm ulivyo mwenyekiti ana nguvu nyingi sana kupita maelezo jk muoga tu mwenyewe au ana ajenda ya siri na huyo lowassa wake,lakini kumshughulikia hashindwi hata chembe,hata wale uv ccm hawajui tu kwamba kugombana na mwenyekiti wa ccm ni hatari sana kwao kama mwenyekiti angekuwa strong,anaweza kuuvunjilia mbali huo umoja wao kama alivyotishia juzi!ipo mifano huko nyuma na wala haitakua mara ya kwanza,ngoja tuwakumbushe nyie vijana!

CCM inaweza kufanya kama ilivyopata kufanya huko nyuma:

Katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995, UVCCM iliweka msimamo uliokuwa unachagiza wagombea vijana wapewe nafasi ya kuwania urais. Majina yaliyokuwa yakitajwa wakati huo ni pamoja na ya kina Kikwete na Lowassa, waliokuwa wakiungwa mkono na kina Anne Makinda na wengineo. Joto lilipozidi, uongozi wa juu wa UVCCM uliondolewa na hali ikabaki salama.
Baadhi ya waliokuwa katika uongozi wa UVCCM wakati huo ni pamoja na John Guninita ambaye leo ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam. Vijana wengine wa enzi hizo ni pamoja William Lukuvi ambaye sasa ni mjumbe wa Kamati Kuu, Leonidas Gama ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Muhammed Seif Khatibu, John Henjewele na Said Mwambungu ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
Aidha, wachambuzi hao wanasema hata ‘kujivua gamba' kulikwishakufanyika ndani ya CCM japo kwa msamiati mwingine, lakini wenye maana karibu na huo.
"Mwaka 1984 walisema hali ya kisiasa ilikuwa imechafuka na kuchafuka huko kukaondoka na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Aboud Jumbe Mwinyi. Baadaye mkono huo wa CCM ukamfikia Maalim Seif Shariff Hamad na wenzake.
"Lakini hata huko nyuma, miaka ile kati ya 1960 watu kama Wilfreim Mwakitwange, Fortunatus Masha(baba wa lau masha), Choga na Kasanga Tumbo ambao walikuwa wabunge maarufu, walifukuzwa ndani ya TANU na chama hakikutetereka," anasema mmoja wa wachambuzi hao.
 
Lowassa is done.....huwezi 'kumjeruhi' mwenyekiti na ubaki salama lol
 
Kwa wale wanaoshangilia "ushindi" wa lowassa baada ya suala lake la kuvuliwa gamba pamoja na suala la Nape na chiligati anaowalalamikia kuzunguka nchi nzima "kumchafua" kutinga mikononi mwa kamati kuu,leo nataka kuwakumbusha kidogo kuhusu Jakaya ili huku mkifurahia "ushindi" pia mumfahamu sawa sawa muungwana jakaya ni mtu wa dizaini gani,sina lengo la kutia mchanga kwenye kitumbua chenu cha furaha la hasha ila nataka tukumbushane muijua siasa pia.Wandugu wapendwa mnajua ilikuwaje mpaka Lowassa akawa sio waziri mkuu.....

Kiufupi ni Kwamba Lowassa aliingizwa choo cha stendi na Jakaya!
Lowassa aliutema uwaziri mkuu anaoupenda mpaka leo kutokana na “utoto wa mjini" utapeli wa kisiasa wa Rais Kikwete kwa swahiba wake Lowassa, wala haikua "ajali ya kisiasa".

Mpango mzima ulikua hivi:

Bunge kupitia Kamati Teule ilisoma ripoti yake kupitia mwenyekiti wake, Dk. Harrison Mwakyembe. Hali ilikuwa tete Dodoma na hata Chamwino ambako Rais Kikwete alikuwa amejichimbia.
Baada ya kusomwa kwa ripoti, taarifa zinasema Lowassa alikwenda Chamwino kuonana na bosi wake ili kupanga mkakati wa kuzima maasi ya wabunge wa CCM waliokuwa wamesisimka ili kummaliza Lowassa, rais Kikwete na serikali yao.
Katika mazungumzo yao usiku ule, Rais Kikwete na swahiba wake huyo wa zamani; – Lowassa akapendekeza eti jk aende upesi kukutana na wabunge wa CCM ili kuwaonya wasiiangushe serikali yao, Jk baada ya "kupima" akastuka.
Ndipo yeye akaja na maarifa ya kimjini kwa kumwambia Lowassa aandike barua ya kujiuzuru, halafu yeye jk aicheleweshe kuijibu hiyo barua kwa makusudi mpaka Bunge lihairishwe ili kumpa nafasi yeye jk kama rais kuonana na wabunge wa CCM ili kuzima maasi ya wabunge kabla ya mkutano mwingine wa Buge wa Aprili haujafanyika Dodoma.
Lowassa na ujanja wake wote eti nae bila ajizi aliamini na kuandika barua ya “kuigiza” kujiuzuru na kisha akaondoka kurudi Dodoma mjini usiku ule. Yaliyotokea Chamwino baada ya Lowassa kuondoka inabakia kuwa siri ya Kikwete mwenyewe na aliokutana nao. Usiku wa manane wa siku hiyo, Rais Kikwete aliamua kuwa barua ile ijibiwe na kukubaliwa. Ni kinyume na makubaliano yake ya awali na Lowassa!

Sasa leo tena suala la lowassa baada ya kupata kibali cha NEC liko mikononi mwa kamati kuu ambamo lowassa hayumo!Na watu wake eti wanashangilia "ushindi" wa ice cream iliyowekwa juani huku jakaya akiwa tayari amejeruhiwa na kutajwa kwenye sakata la richmond na pia ikikumbukwa Jakaya hana tena cha kupoteza kwa kuwa hawezi tena kuwa rais!mi nawaomba msiwe wajinga kama jamaa yenu kwa mujibu wa mwalimi nyerere ambae alifahamu ujinga wake zamani kabla kabla ya jk kuja kuthibitisha kwa kumuingiza choo cha stendi!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Asante Mama Salma
 
majuzi hapa Muheshimiwa Lowassa aliiitisha kikao na waandishi wa habari akawaambia dhumuni la kikao hicho ni kuwaeleza taarifa aliyo nayo.
Then baada ya waandishi kufika ikabadilshwa ratiba na kuambiwa kuwa Lowassa kawaita kwa ajili ya kujibu maswali ya waandishi.

Nini kilifichwa pale?
Muheshimiwa Lowassa ni Rais wetu atakayetutoa ICU na kutupeleka ktk nchi ya Kanani.

Inshaaalah
 
jk hana ubavu wakumfanya lowassalolote...jk muoga na siasa za kitaalamu kama zq lowassa haziwezi

Thanx Chezo.
We una akili nyingi sana.
Na inavyoelekea ulizaliwa hospital na kupata huduma zoote muhimu, na ndio maana akili zako zimefunga na kukamilika
 
Lowassa na ujanja wake wote eti nae bila ajizi aliamini na kuandika barua ya “kuigiza” kujiuzuru na kisha akaondoka kurudi Dodoma mjini usiku ule. [/QUOTE]

Unajua nini? Wote ni wajanja, lakini kuna tofauti kubwa sana kati ya mjanja aliekulia Monduli na mjanja aliyekulia Magomeni!!!
 
Lowasa hana makosa, hakutendewa haki hata kidogo. Tuishi kwa kumuogopa Mungu, kama kuna kundi linapanga njama chafu mbele ya kiumbe cha Mungu kisicho na makosa, basi subiri uuone jinsi ukweli utakavyojitenga na uwongo. Nuru na giza havitakaa pamoja hata siku moja. Lowasa atashinda kwa hili nina hakika 110%

Mkuu unataka kuniaminisha kitu kigumu!
 
Mi siwaelewi kwahiyo mnataka kusema rais wa 2015 ni Lowassa na si DK Slaa tena??? Au tunaongelea wagombea tu
 
kwa hali ilivyo tete sasa na kwa mujibu wa mleta mada ni kuwa jk kajeruhiwa kweli. Na huyu jamaa akijeruhiwa huwa mbaya kuliko nyati. Lolote laweza tokea
 
kwa hali ilivyo tete sasa na kwa mujibu wa mleta mada ni kuwa jk kajeruhiwa kweli. Na huyu jamaa akijeruhiwa huwa mbaya kuliko nyati. Lolote laweza tokea

only Allah can stop Honorable Lowassa...
no one else.
Mark n bind it
 
Back
Top Bottom