Lowassa aongea na vyombo vya habari; akataa kugusia suala la Richmond/DOWANS

Kumbe Lowasa mwoga kiasi hiki, hafai kuwa rais. Alikuwa na jambo kubwa(kumwaga ugali) aliseme leo lakini kapigwa mkwala akabadilika dakika za majeruhi na kuja na upupu huu. Fisadi ni fisadi tu hawezi kuwa jasiri hata siku moja ,siku zote mwenye hatia ni mwoga.
 
Wakuu,

Lowassa kaondoka hapa Monduli muda si mrefu na inasemekana kaitwa Ikulu.

Alichoongea hakikuwa kwenye mpangilio unaoeleweka na imezidi kushangaza kuona anaondoka mida hii. Tunafuatilia tutawafahamisha zaidi
Nimekubali msemo wake kuwa yeye na rais hawakukutana barabarani. Kwa hiyo urafiki mbele au kwanza watanzania na matatizo yao shauri yao
pili kumbe ikulu kunaendeka tu? na kweli hawa wawili wananufaika na matatizo yetu
 
Wakuu,
  • .
  • Kuna waliofikia kudai eti namhujumu Mhe. Rais. Wengine eti nna mpango wa kumpindua kwenye Halmashauri kuu ijayo. Sina mpango wa hujuma na hata mabaya ya rais Kikwete siyafahamu.

teh tih toh jamani naombeni ruhusa ya kucheka.. tih toh.. ha ha haaaa... aa my Lowasa.. Ha he he.. Kuna yule informa wako anayesomasoma vijarida na vihabari na kukupasha yaliyojiri kwenye habari.. akipitia Humu jamvini ataona hapo nilipobold Red.. akurudishie taarifa kwamba kuna mtu mmoja jamvini amecheka sana uliposema hata mabaya ya mzee huyajui.. Mtu mzima kuogopa mtu mzima mwenzako ooooovyo.. unaogopa mpaka kivuli chako.. Pole. we?.. Halafu Ntakuvuruga mimi.. sipendi mtu mzima aongee hovyohovyo mbele ya watanzania. Lazima utuheshimu watanzania yaani sisi tuwe jalala la kudanganywa kila mchao?!. kwanini uongee ujingaujinga wakati ukweli unaujua.. Kuna siku mliwahi hata kutaka kurushiana ngumi na mzee kwenye Korido ya Hoteli kule nairobi.. unadhani cctv camera za hoteli hazijawarekodi??? na sababu yenyewe ya ugomvi wenu ni ya kipuuzi na aibu.. kha.. mnisamehe Mods.. Huyu Mheshimiwa anakera sana sometimes.. wacha niondoke zangu humu jamvini kama kuna mtu kanikera basi Lowasa zaidi.. nijizuie nisijefurisha zaidi.. BYE!!
 
Hivi siku hizi kuna direct flight kutoka Monduli mpaka Dar? Au amekodi Charter?
 
bishop hiluka unakosea kukopi majina yoooote ya cureent users...kama huna cha kupost ka usome coment za wenzako
 
Lowasa amepatwa na msongo mkubwa sana, kuna kitu alitaka kusema inaonekana alizuiwa wakati tayari kaita waandishi. Ningeomba video yake ili tuone (body language) ilikuwaje. Kuna wakati Invisible alisema kakatisha akaingia ndani. Sidhani kama aliwaita waandishi kuwaambia hajawatuma vijana wa Arusha, haiwezekani kuwa aliwaita kuwaambia hajakutana na JK barabarani. Jk kesha mtosa inawezekana swaga la Igunga linawachanganya wavua gamba hivyo wamevuta pumzi. Je simu ilitoka kwa nani ???????? Please invisible come out .............
 
Hapo bana hata akiongea maneno mengi kiasi gani,
Kama tu hakuzungumzia Richmond, Dowans, Kujivua Gamba na uenyekiti wa CCM mwaka 2012 basi mkutano wake huo utakua ni sawa vijiwe vya kahawa tu kwa ajili ya kupitishia muda jua lizame
 


salma kwa hili la leo huyu jamaa lazima apakwe matope ..anacheza na akili za watu..aache ujinga kabisa na ajue kuwa kuna watu tunamfaham vizuri tu....na leo ameamua kupindisha ukweli..ameona aibu kuwaambia wandishi wa habari dakika za mwisho kuwa hawezi kuongea nao ila akaona ni heri apoteze mda kwa kuongea ushenzi....nimeomba mwongozo kwa mod bado kimya
 

sijui nitumie theory gani za fikizikia kukupata frequency zako ..
usomeki ila unaonekana ni mwanga mkubwa kwenye hili giza totoro kwa sie wenye hamu ya kupata ukweli wa mambo
ila ngoja niendelee kuconnect dot ntafunguka tu.............
 
Uhuru wa vyombo vya habari unakuwa abused.

Sija muelewa,...
unakuwa abused kwa kumuandika sana au unakuwa
abused na magazeti yanayo eneza chuki za kidini?

Kwa jinsi alivo sema kwamba ata shitaki magazeti yanayo mfuata fuata
ina maanisha kwamba angekua raisi huyu waandishi wa habari wote
angesha biga "kimya" kwa style yoyote ile.
Possibly it will be the end of JF akiwa raisi,...hell never.
Next time when you get sick,don't come back.
I wish it will be soon before 2014.

He doesn't have the qualifications to be a president.
Ni dikteta asiye na manufaa,( udikteta mwingine mzuri lakini).
 
Ama kweli Lowassa kiboko. Masaa mawili na nusu tu tangu thread ianze Replies 227 and Views 4,365 ? Je hiyo siku muafaka ukifika itakuaje?!
 
Shukrani mkuu je tunaruhusiwa kuuliza maswali pia au hakuna maswali na majibu? Maana tuna lundo la maswali moja wapo ni ile nyumba kule London atuambie hela hiyo imetoka wapi???

Kuwa na nyumba London sio utajiri ni rahisi sana, kule nyumba zinauzwa kama magari na thamani ya nyumba iliyotumika ni ndogo sana, mahesabu huwa yanapigwa kutokea nyumba ilipojengwa. Kutokana na muda ambao amefanya kazi EL hata kama ni wewe kama ungekuwa na akili za maendeleo ungeweza kuwa na zaidi ya hata alivyonavyo EL pamoja na kuwa mengi ni maneno wala sio kweli. Ukiulizwa nyumba iko London mtaa gani na ni plot namba ngapi huwezi kujibu.
 
There are currently 838 users browsing this thread. (219 members and 619 guests)

Kweli siasa imeshika hatamu!
 

Inaonekana umeandika kiushabiki shabiki kitu ambacho si kizuri kwa mwaandishi. Ilitakiwa utoe vile alivyojibu na vile alivyoulizwa pasi na kuingiza ushabiki na kuacha suala kwa wasikilizaji au wasomaji watoe uamuzi.

Ok lakini thanks kwa taarifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…