Lowassa aongea na vyombo vya habari; akataa kugusia suala la Richmond/DOWANS

Lowassa aongea na vyombo vya habari; akataa kugusia suala la Richmond/DOWANS

kwa kweli Mh. EL amenifurahisha sana! yaani amefafanua vitu ambavyo vilikuwa vinaumiza sana vichwa vya watu; yaani EL kumhujumu JK? wala nilikuwa sipati picha! ama kwa hakika huyu ndiye Rais wa 2015; yaani anaongea vitu nyeti mpaka vinasisimua masaburi ya watu!
 
Huu ni uwongo: Mwalimu Nyerere mnamsingizia bure, kama ni hivyo mbona alimkataa Kikwete na bado akaukwaa Urais: Nzuma aikataliwa na Mbeki na bado ni Rais, Huu ni unafiki wa kiafrika kwa sababu tu fulani anasema hivi na kila mmoja anashabikia

Alichofanya Lowassa ndicho hasa mweye akili angeweza kufanya. Sibishani na mawazo ya mtu na bishana na uzito wa hoja

Nasubiri unikumbushe hapa, unasema Mwl. Nyerere alimkataa JK. Hebu tueleze, alimkataa kwa maneno gani? Mimi ninakumbuka each and everything vilivyotokea ktk kikao kile.
 
Je walikutana wapi? maana hii si kauli mpya, aendelee zaidi, nahisi kama ina maana kubwa nyuma yake.
 
pole, nnahakika hiki si kilichotarajiwa na wengi, cjui angle ni ipi hapa, au ya sijakutana na kikwete barabaran? labda japo si ngeni pia, angeongeza kidooogo kusema wapi walikutana.

Huyu mzee hana wanashauri wazuri, wakati watanzania wanasubiri kwa hamu kusikiliza hatima yake na sakata lilimtoa madarakani la RICHMOND, yeye anatuletea "uzuri" kuwa hakukutana na JK mitaani, hilo linamsadia nini mwananchi anayeishi Manzese?
 
attachment.php
 
Wana JF,
Jamani hii kauli ya Lowassa kwamba yeye na Kikwete hawakukutana barabarani, halafu hakuongea chochote kuhusiana na dhana ya Kujivua gamba ina ujumbe gani kwa kijana Nape? NAPE; LOWASSA NA KIKWETE HAWAJAKUTANA BARABANI. Nawasilisha wadau

unataka kujibiwa hapa? Eeeh! Aisee watu hawana kazi kwelikweli. Mnabaki kuanzisha majungu tu!
Hivi ukijibiwa na wanajamvi, then? Utayafanyia kazi?
Think twice before you post anything JF.
 
Nasubiri unikumbushe hapa, unasema Mwl. Nyerere alimkataa JK. Hebu tueleze, alimkataa kwa maneno gani? Mimi ninakumbuka each and everything vilivyotokea ktk kikao kile.

Inaonekana huna kumbukumbu sahihi ya kutetea hapa. ONYO: Siku nyingine usiwe unakurupuka na kuanza kusema bila kuwa na uhakika na unachosema... Ngrrrrrrrrrr......!!!!!!!!
 
Bora umelijua leo mkuu...yule jamaa sound system kama woofer ya kichina!
 
Hii kauli ni nyepesi sana na inatia kinyaa sana...sasa kama akukutana na kikwete barabarani au popote pale inamaanisha nini? maana hizo ni porojo tu...Sisi hatuambie kwanini yeye ni mwizi wa mali ya umma na kwanini haachi na sasa anataka malipo ya Dowans...?
 
Wengi wetu tuliokaa mkao wa kula toka jana na kudhani kiranja wa Monduli atamwaga ugali baada ya mpangaji wetu wa Magogoni kumwaga mboga miezi kadhaa ilopita tumepigwa na butwaa baada ya EL kuongelea ajira ya vijana hahaha!

ni hivi lowasa ames0mea shahada ya uigizaj ambayo ni FINE AND PERFOMING ARTS(FPA)sasa usimshangae
 
Huyu fisadi alitakiwa kuwa gerezani tu,kuwa kwake nje kunacreate confusion kwa watanzania tu.Tunahangaika na umeme,nabado tunahitajika kulipa Dowans mabilion kwa ufisadi wake halafu anajifaraguwa!Kikwete peleka huyu kibaka Ukonga asitutie hasira hapa!!!
 
sawa mh. wa richmond , lakini mbona hujatuambia kuhusu richmond, na pia kazi wanazofanya vijana wako pale arusha ambao wao wanasema wewe ni wao. hakuna kitu kitakachofanyika katika nchi hii halafu iwe sir, hakuna, kwa vile wewe unajua unachokifanya ktk serikali hii, unafahamu sana. kwa nadhani usijitetee cha msingi acha kuihujumu serikali ya jk, uache wewe pamoja na vijana wako. kwa sababu wewe unaweza kuficha lakini vijana wako hawawezi kuficha wanayasema yote kwa sababu si vijana wote ni wako wengine ni ndumilakuwili nimeamua kukueleza ukweli, yaani unaanza kukataa kuhusu hujuma baada ya kushindwa kuhujumu? ni ajabu. serikali hii imechaguliwa na watanzania unapoihujumu basi unawahujumu watanzania ambao wewe unadai unawaonea huruma. huruma gani mh. wakati ulikuwa tayari kuhakikisha unalazimisha kusaini mikataba gandamizi? na ya kifisadi. vijana gani unawatetea wewe ulipokuwa waziri mkuu hukujua kuwa kuna vijana wasio na kazi, leo hii wakati hupo madarakani unaanza kuona! hapana huu si uungwana huo ni udanganyifu. leo baada ya kuwepo pinda umeanza kuona ajira ya vijana ni tatizo ulikuwa wapi, au ulikuwa busy na mikataba feki sasa ndio unakumbuka. Samahani sana mh. inatosha ,uliowafanyia watz inatosha, kama unadhani ulikuwa mwema ila hatukukuelewa basi ni bahati mbaya, unaweza kudanganya monduli lakini huwezi kudanganya tz nzima. inatosha, ushauri, nakuomba kwa huruma yako usitaafu siasa ili ufanye kazi nyingine , unafahamika una kampuni na fedha, mashamba,majumba mengi ndani na nje ya nchi toka enzi za nyerere tunakuomba utuhurumie sasa watz. inatosha .umwogope mungu na pia fahamu jinsi ulivyo na ukwasi na jinsi hali wa watz wengine walivyo na shida na jinsi wanavyotaabika. ukijiona wewe ulivyo mbali na watz wengune ndio utajua kuwa wewe ni tajiri. pokea ujumbe huu
 
kwa kweli Mh. EL amenifurahisha sana! yaani amefafanua vitu ambavyo vilikuwa vinaumiza sana vichwa vya watu; yaani EL kumhujumu JK? wala nilikuwa sipati picha! ama kwa hakika huyu ndiye Rais wa 2015; yaani anaongea vitu nyeti mpaka vinasisimua masaburi ya watu!
Mmmmh!! Hapa sina la kuongea.
 
Huyu mzee hana wanashauri wazuri, wakati watanzania wanasubiri kwa hamu kusikiliza hatima yake na sakata lilimtoa madarakani la RICHMOND, yeye anatuletea "uzuri" kuwa hakukutana na JK mitaani, hilo linamsadia nini mwananchi anayeishi Manzese?

EL siyo msafi ... neither is Malaika. Unapotetea mmoja ya hawa wawili then either utakuwa unafaidika na mfumo wao uliopo au utakuwa unatumia masaburi kufikiri. Inafahamika kuwa hakuna urafiki wala uadui wa kudumu katika siasa, wote hao wanalifahamu hilo, so suala la kwamba mmoja amemgeuka mwenzake hapo sio la ajabu. Alichofanya Malaika kwa mwenzake sio kizuri japo anajificha nyuma ya migongo ya wapambe wake na kuwashambulia wenzake. Na kadhalika anayoyasema Lowassa kwa baadhi ya watu kuhusu Malaika sio mazuri pia. Kinachoendelea hapo ni vita ya usaliti kwa wote wawili, wote wanazungukana na matokeo yaweza kuwa mabaya sana.

Press release ya EL ina ujumbe kuliko unavyoweza fikiria, he has just sent a very stong message kwa Malaika & co. kuwa aache kutumia wapambe na media kumchafua na kwamba bado ana hold a number of key secrets ambazo zaweza kuleta vurugu nchini au hata kupelekea kupoteza uhalali wa kuongoza serikali kwa Malaika (kuangusha serikali ya Malaika) endapo ataamua kutapika. Kwa waelewa, ujumbe umefika, waweza ona idadi ya "line" za wakubwa zilivyokuwa busy that time and few minutes before, na masikio ya wa-tz yaliyoelekezwa monduli, ina maanisha nini?? maana yake ni kwamba wananchi wengi bado wanaamini kuwa kuna siri kuhusu machafu ya serikali katika sakata la uraisi 2005 & 2010, dowans/richmond, RITES, ATC, meremeta, etc. ambayo bado wanafichwa, na mmoja wa watu wanaoweka weka huo uchafu bayana ni EL, but also it might cost someone's life for the truth to be revealed.

Btw, kiapo cha UWT kinasemaje?? Will they let that happen?? Mwenye code name ya Malaika bado ni "malaika" kweli in that sense au ameshageuka na kuwa "Luc..."?? Let's see kama some one might dare!

My 0.02!!
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Tufikie mahali tukatae hii mikutano na waandishi wa habari kukiwa na masharti ya kutojibu mambo ambayo kutokana na nafasi za viongozi, wanapaswa kuyafahamu. Nini maana ya Lowassa kukataa kusema chochote kuhusu Richmond/Dowans wakati ndio swala lililomkosesha kazi?? Kwanini asiseme chochote wakati si sehemu ya serikali na hana kiapo cha kuficha siri??

KATIBA mpya ituondolee usiri katika mambo yanayohusu nchi. Kila kitendo cha kiongozi lazima kiwe halali na kihojiwe, taarifa sahihi na za ukweli lazima zipatikane. Inaumiza kama mtu anakataa kujibu maswali yenye umuhimu kwa jamii na hufanya mahojiano mazima yamhusu yeye na nafsi yake tu!
 
"Kuna waliofikia kudai eti namhujumu Mhe. Rais. Wengine eti nna mpango wa kumpindua kwenye Halmashauri kuu ijayo. Sina mpango wa hujuma na hata mabaya ya rais Kikwete siyafahamu."


Anaposema maovu ya JK hayafahamu ana maana gani? Aliwahi kusema serikali haina uwezo wa kufanya maamuzi magumu alikiwa analizungumza kama jambo zuri? Hivi serikali mbaya inawezekana kuongozwa na rais asiye na mabaya? Ukitaka kudanganya hakikisha unatembea na notebook otherwise utaumbuka.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Tufikie mahali tukatae hii mikutano na waandishi wa habari kukiwa na masharti ya kutojibu mambo ambayo kutokana na nafasi za viongozi, wanapaswa kuyafahamu. Nini maana ya Lowassa kukataa kusema chochote kuhusu Richmond/Dowans wakati ndio swala lililomkosesha kazi?? Kwanini asiseme chochote wakati si sehemu ya serikali na hana kiapo cha kuficha siri??

KATIBA mpya ituondolee usiri katika mambo yanayohusu nchi. Kila kitendo cha kiongozi lazima kiwe halali na kihojiwe, taarifa sahihi na za ukweli lazima zipatikane. Inaumiza kama mtu anakataa kujibu maswali yenye umuhimu kwa jamii na hufanya mahojiano mazima yamhusu yeye na nafsi yake tu!

Ni wamoja na yule aliyekuja akawaita waandishi alafu akawakataza kutumia vitendea kazi vyao na masharti kibao, japo yeye ndio kawaita, je wamkumbuka? kama wana uhusiano vile! au ndio strategy?
 
"Gazeti flani linaloniandama lilishafikia hatua ya kusema ndo nahusika na maasi ya vijana wa UVCCM, ni uwongo na wala sihusiki kwa namna yoyote na vijana wa Arusha. Nilikuwa nje kwa matibabu, ningejuaje nini wanapanga vijana?"
.......? Do huu ugonjwa utakuwa hatari sana maana Nigeria, Malasia, Singapore, India, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani???? Nilifikiri viongozi wetu wanatibiwa India??
 
Back
Top Bottom