Lowassa aongea na vyombo vya habari; akataa kugusia suala la Richmond/DOWANS

Lowassa aongea na vyombo vya habari; akataa kugusia suala la Richmond/DOWANS

Nakubaliana na Invisible kuwa 'ficha upumbavu wako'. Kumbe ni afadhali wale wa wizara ya Nishati na madini waliokacha mdahalo star Tv kuliko huyu aliyeamua kuanika upuuzi wake kwa wandishi wa habari.
Hivi anafikiri magezeti yataweka headings gani kesho?
Lowassa anasema "ninyi wanahabari na sisi wanasiasa tumekuwa tukitumia muda wetu mwingi kujadili watu na propaganda za kisiasa zisizo na tija...."
Hivyo yeye kama mwanasiasa licha ya kulaumu matumizi ya muda mwingi matika masuala hayo yasiyo na tija, leo ameendelea kufanya hayo hayo anayolaumu kwa kuwapotezea waandishi muda wao na kujadili watu(wanahabari) na propaganda za kisiasa (eti sijamhujumu JK, eti hatukukutana barabarani)
Ama kweli nyani haoni kundule
 
Tatanyengo,

Mfa maji haishi kutapatapa. EL anakoenda ndio mwisho wake ktk duru za kisiasa. Huenda anatafuta sababu za mwisho huo wa kisiasa.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
kumbe hata lowasa hawezi kufanya maamuzi magumu.ni heri angeendelea kukaa kimya.

Anajua kufanya maamuzi magumu ya kuiba mali za Umma tu. Angekuwa na busara na kutaka kujijengea heshima angejiuzuru kama alivyotakiwa kufanya na Chama chake.
 
Sasa niseme rasmi, IMETOSHA. Sintoendelea kuvumilia kuchafuliwa na vyombo vya habari. Nitachukua hatua kali dhidi ya magazeti yatakayonichafua na vyombo vya habari vyote vinavyonichafua. Ukinichafua nitakupeleka kwenye vyombo husika na niseme uhuru usio na nidhami ni fujo. Uhuru wa vyombo vya habari umekuwa 'abused' sana.

Hivi hapo kwenye red alikuwa ana maana gani vile??? Kama kweli vyombo vya habari vinamchafua ni kuhusu maswala yale aliyakataa kuyajibi. Sasa kwa nini asingeongelea yale watu walitegemea ili wapate majibu yake na wasiendelee kumchafua??

Kweli usanii wa siasa Bongo umezidi!!
 
Huu ni uwongo: Mwalimu Nyerere mnamsingizia bure, kama ni hivyo mbona alimkataa Kikwete na bado akaukwaa Urais: Nzuma aikataliwa na Mbeki na bado ni Rais, Huu ni unafiki wa kiafrika kwa sababu tu fulani anasema hivi na kila mmoja anashabikia

Alichofanya Lowassa ndicho hasa mweye akili angeweza kufanya. Sibishani na mawazo ya mtu na bishana na uzito wa hoja

Hutafanikiwa kwa kuwatisha waandishi wa habari. Fanikio lako ni kukiri na kutubu kwa wananchi wa Tanzania kwa madhambi uliyoifanyia nchi hii. Tuanze pale alipoishia marehemu Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere. Hakusita kukwambia ukweli kuwa wewe HUFAI kuwa Kiongozi wa nchi hii. Alikupa sababu za kusema vile. Bado hadi leo sijasikia au kuona sehemu au wakati wowote ukiomba radhi, badala yake umekuwa ukiendelea kujilimbikizia mali na kutafuta uongozi kwa gharama zozote. Lowasa mambo haya uwe unaongea na wajinga wanaoshindwa kukwambia ukweli juu ya taswira yako kisiasa nchini. UNANUKA ndugu yangu. Heba siku moja jaribu kupita Kariakoo mchana uone wananchi watakavyokupokea.
 
Umaskini wa mawazo hupelekea umaskini wa akili! Hivi kwa leo hii ni nani anaweza kuweka wazi vyanzo vya mapato yake!!!! Hii ni kutokutenda haki kwa mtaznzania mmoja kwa hasara ya watanzania wote yeye inclusive

Bwn Exaud Minja wacha kukurupuka mitaa zilipo hizo nyumba inafahamika, tena iliwekwa wazi hapa jamvini toka kwa kitengo cha uchunguzi wa uchumi SFC cha UK!!!!!!!! Mpaka acct za Bank zilizopeleka fedha na CO zilizotoa fedha!!!!!!!!! Hiyo ni cha mtoto je USD $300million zilizoko Swizz Bank vipi unayo majibu???????????????
 
Kama kukimbia kivuli hatukujui, basi ndiko huku; hajatangaza kugombea, kelele je akitangaza: Kumbuka JK na EL hawakukutana FB au JF ni marafiki wa siku Mingi

...hawezi kuwa rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa sababu:
  1. Aliiba mihela mbele ya baba wa taifa, hivyo akamlaani kwa kusema,
  2. Hafai kuwa kiongozi, na laana hiyo ilimtafuna pale Jk alipo mteua kuwa PM
 
Mh. Edward Lowasa kuwa mwangalifu sana na kauli zako kuwa eti humfanyii hujuma JK. Ulikutana na Spika mstaafu mmoja ukaongea nae mambo mengi. Kama kweli wewe ni Mkristo na una abudu kwa TB Joshua pia, jiulize, yale uliyoongea na mzee huyo sio hujuma kwa JK?

Ulikutana na Waziri Mkuu mmoja mstaafu (ambaye hakufukuzwa kama wewe). Ukaongea nae mambo mengi. Je, yale uliyoyasema sio hujuma kwa JK?

Umekutana na mzee mmoja anayemiliki vyombo vya habari. Ukaongea nae mambo mengi, je yale uliyayasema dhidi ya JK sio hujuma?

Leo unatoka hadharani na kusema kuwa eti hukukutana na JK mitaani, kama ungekuwa unamuheshimu na kumthamini rafiki yako usingeyasema hayo yote kwa watu wachache tu niliowataja hapo juu. Toka ufukuzwe ktk nafasi ya Uwaziri Mkuu, hebu tuambie ni mambo gani umeyafanya ya kumsaidia JK?
 
Huu ni uwongo: Mwalimu Nyerere mnamsingizia bure, kama ni hivyo mbona alimkataa Kikwete na bado akaukwaa Urais: Nzuma aikataliwa na Mbeki na bado ni Rais, Huu ni unafiki wa kiafrika kwa sababu tu fulani anasema hivi na kila mmoja anashabikia

Alichofanya Lowassa ndicho hasa mweye akili angeweza kufanya. Sibishani na mawazo ya mtu na bishana na uzito wa hoja

Nadhani unakumbukumbu za ajabu sana wewe. Mwl. Nyerere alimkataa JK kwa maneno yapi?
 
Falesy,

Kama kweli unaamini kuwa Lowasa anafaa kuongoza basi mpe mtihani mdogo sana. Kwa kuwa atawaongoza watanzania, hivyo basi hata wananchi wa Manzese, Buguruni, Kariakoo na Tandika ni watanzania pia na wapiga kura halali ktk nchi. Hebu mpelekeni huko akatoe hotuba kama wanavyofanya wana siasa wenzie. Nyie endeleeni kumtetea tu, hamjui munamuangamiza kisiasa mpendwa wenu.
 
Mh. Edward Lowasa kuwa mwangalifu sana na kauli zako kuwa eti humfanyii hujuma JK. Ulikutana na Spika mstaafu mmoja ukaongea nae mambo mengi. Kama kweli wewe ni Mkristo na una abudu kwa TB Joshua pia, jiulize, yale uliyoongea na mzee huyo sio hujuma kwa JK?

Ulikutana na Waziri Mkuu mmoja mstaafu (ambaye hakufukuzwa kama wewe). Ukaongea nae mambo mengi. Je, yale uliyoyasema sio hujuma kwa JK?

Umekutana na mzee mmoja anayemiliki vyombo vya habari. Ukaongea nae mambo mengi, je yale uliyayasema dhidi ya JK sio hujuma?

Leo unatoka hadharani na kusema kuwa eti hukukutana na JK mitaani, kama ungekuwa unamuheshimu na kumthamini rafiki yako usingeyasema hayo yote kwa watu wachache tu niliowataja hapo juu. Toka ufukuzwe ktk nafasi ya Uwaziri Mkuu, hebu tuambie ni mambo gani umeyafanya ya kumsaidia JK?
Ni yapi aliyasema...?
 
Nilitegemea atavua gamba kumbe ni blaablaa anapiga tu
 
Namhifadhi kwa sasa. Nataka alete watu wake wakanushe hapa nimlipue. Tumechoka na huyu mzee, tunamuheshimu sana lakini sasa anatuona wote wajinga labda kwa sababu tumekaa kimya naye anadhani hatujui anayoafanya. Anadiriki kuwaambia waandishi kuwa eti kuna kundi la watu wachache wanafanya juhudi ya kumchonganisha na JK, na kuwa yeye na JK hawakukutana mitaani. Swali la kujiuliza hapa ni kuwa: Huko kote ulikokuwa unaenda ulitumwa na kundi hilo unalodai linakuchonganisha na JK?
 
TO ME EL IS JUST A COWARD!!!

Kila siku anatisha, anaongea na vyombo vya habari vitu vilevile, he cant stand up and be counted... anatumia vitoto kama millya na kudhani anaweza kuinfluence, ni uppuzi mtupu

he should stand up kama Rostam... or even better

AS FAR AS I AM CONCERNED, HII TALK NA WAANDISHI HAINA MAANA, IT HAS JUST LOWERED FURTHER HIS RATINGS AND WAS A WASTE OF TIME

I AM ALSO WORRIED HIS DAYS COULD BE NUMBERED
 
Nilitegemea atavua gamba kumbe ni blaablaa anapiga tu

Akili hiyo anayo? Angepiga bao la nguvu sana ndani ya Chama na Serikalini kama angejivua gamba mapema. Yeye anadanganywa sana na baadhi ya wajumbe wa NEC kuwa watamtetea. Mimi sioni hoja ya kumtetea ktk kikao kijacho, SAFARI ITAMKUTA TU. Akiendelea kudanganya tena tutamuanika hadharani ili hata hao wanaojifanya kumtetea wakose pa kuanzia kuongea nae. Angekuwa smart angekuwa anawauliza wapambe wake kuwa, wana hoja gani ya msingi watakayoitumia kumtetea? Baada ya hapo angeona wazi kuwa mwelekeo wake uko vipi.
 
TO ME EL IS JUST A COWARD!!!

Kila siku anatisha, anaongea na vyombo vya habari vitu vilevile, he cant stand up and be counted... anatumia vitoto kama millya na kudhani anaweza kuinfluence, ni uppuzi mtupu

he should stand up kama Rostam... or even better

AS FAR AS I AM CONCERNED, HII TALK NA WAANDISHI HAINA MAANA, IT HAS JUST LOWERED FURTHER HIS RATINGS AND WAS A WASTE OF TIME

I AM ALSO WORRIED HIS DAYS COULD BE NUMBERED

Rostam is a man... though.
 
Wana JF,
Jamani hii kauli ya Lowassa kwamba yeye na Kikwete hawakukutana barabarani, halafu hakuongea chochote kuhusiana na dhana ya Kujivua gamba ina ujumbe gani kwa kijana Nape? NAPE; LOWASSA NA KIKWETE HAWAJAKUTANA BARABANI. Nawasilisha wadau
 
Natamani Cc ya ccm impitishe kugombea urais, mtamu sana huyu kugombea nae.
 
nimemaliza chaji ya simu yangu bure..

pole, nnahakika hiki si kilichotarajiwa na wengi, cjui angle ni ipi hapa, au ya sijakutana na kikwete barabaran? labda japo si ngeni pia, angeongeza kidooogo kusema wapi walikutana.
 
Back
Top Bottom