sawa mh. wa richmond , lakini mbona hujatuambia kuhusu richmond, na pia kazi wanazofanya vijana wako pale arusha ambao wao wanasema wewe ni wao. hakuna kitu kitakachofanyika katika nchi hii halafu iwe sir, hakuna, kwa vile wewe unajua unachokifanya ktk serikali hii, unafahamu sana. kwa nadhani usijitetee cha msingi acha kuihujumu serikali ya jk, uache wewe pamoja na vijana wako. kwa sababu wewe unaweza kuficha lakini vijana wako hawawezi kuficha wanayasema yote kwa sababu si vijana wote ni wako wengine ni ndumilakuwili nimeamua kukueleza ukweli, yaani unaanza kukataa kuhusu hujuma baada ya kushindwa kuhujumu? ni ajabu. serikali hii imechaguliwa na watanzania unapoihujumu basi unawahujumu watanzania ambao wewe unadai unawaonea huruma. huruma gani mh. wakati ulikuwa tayari kuhakikisha unalazimisha kusaini mikataba gandamizi? na ya kifisadi. vijana gani unawatetea wewe ulipokuwa waziri mkuu hukujua kuwa kuna vijana wasio na kazi, leo hii wakati hupo madarakani unaanza kuona! hapana huu si uungwana huo ni udanganyifu. leo baada ya kuwepo pinda umeanza kuona ajira ya vijana ni tatizo ulikuwa wapi, au ulikuwa busy na mikataba feki sasa ndio unakumbuka. Samahani sana mh. inatosha ,uliowafanyia watz inatosha, kama unadhani ulikuwa mwema ila hatukukuelewa basi ni bahati mbaya, unaweza kudanganya monduli lakini huwezi kudanganya tz nzima. inatosha, ushauri, nakuomba kwa huruma yako usitaafu siasa ili ufanye kazi nyingine , unafahamika una kampuni na fedha, mashamba,majumba mengi ndani na nje ya nchi toka enzi za nyerere tunakuomba utuhurumie sasa watz. inatosha .umwogope mungu na pia fahamu jinsi ulivyo na ukwasi na jinsi hali wa watz wengine walivyo na shida na jinsi wanavyotaabika. ukijiona wewe ulivyo mbali na watz wengune ndio utajua kuwa wewe ni tajiri. pokea ujumbe huu