Lowassa aongea na vyombo vya habari; akataa kugusia suala la Richmond/DOWANS



Serikali unayodai inahujumiwa ni serikali yenye uzuri gani hiyo kwamba inahujumiwa. Ni mafanikio yepi iliyowahi kuwa nayo na kwamba baada ya EL kuwa nje sasa anaihujumu. Tutajie hayo mazuri ambayo yanaweza kufunika mabaya waliyoyahsis wote wawili-kuunda kundi la kimafya (mtandao) character assassination vs waliwahis washindani wao, wezi wa EPA, mikataba ya madini JK akiwa waziri wa mamabo ya nje, corruption to the media, kutajirisha wanawe kwa mgongo wa ikulu, udini na ngunaisation ndani ya serikali na sehemu za maamuzi. Sasa kwenye madhambi yote haya ni lipi JK wako alijaribu kusahihisha likahujumiwa na EL. Tuambie na utoe source of information. Tunataka facts based on researched findings na sio kuongea mambo ya kubuni hapa.

Halafu mlitaka atukane ili tushindwe kumtofautisha na nepimwnye kuporomosha matusi?
 
"I think this is enough for your stomach" watu matumbo yalikuwa yanaunguruma ndiyo maana kamanisha hivyo, cha maana alichoongea ni hicho cha vijana na ajira, ni bomu haswa

hiki ndo cha msingi nachokiona aichoongea maana anapigia kelele kwa sana hata kabla ya kwenda huko kwenye matibabu.
 
Katika hilo la usiri wa serikali hakuna haja ya kusubiri Katiba mpya, Katiba mpya haitakua "kikombe cha babu" kwa kila tatizo.

Sasa hivi kuna muswada umekaliwa wizarani miaka enda rudi kuhusu uhuru na haki ya Mtanzania kudai taarifa au siri feki za serikali, tunahitaji Freedom of Information Act sasa.

Kwa mfano, wiki hii tumesikia unofficially kwenye mablogu ya Wamarekani kwamba Tanzania imenunua jumba la maghorofa kibao east side of Manhattan kwa ma bilioni ya shilingi. Kwa nini tusisikie kutoka kwenye vyanzo vyetu na kuonyeshwa ma nyaraka hukusu hela yetu? Mpaka Wamarekani watuwekee kwenye ma blogu? Kwa nini hatuna haki ya kujua taarifa za kina jumba ni la nini, balozi amerudisha jumba analokalia sasa au? Jumba limelipiwa mortgage au cash? Kwa bajeti ya fungu gani? Limehitajika kwa nini? Ni ofisi au ni kathiri la wakuu wa nchi kukutana na mapozeo yao wakiwa US kuomba misaada? Hatujui na hakuna mwandishi wa habari wa kibongo anaeweza kufukua taarifa kama hizi. Tunadai haki ya habari za shuguli za serikali sasa.
 
kaongea ubuuzi tupu hoja za maana kaacha. Kikao hakikuwa na maana yoyote sana ni majungu
 
Tofauti na RA, EL hawezi kutema ugali kabisa kwa sasa. Huyu mheshimiwa ana imani kubwa kutinga magogoni 2015 na kampeni zake ziko wazi, nawashangaa mnapokaa na kumsubiri ateme ugali. Kimsingi mimi namwona anajibu tuhuma nyingi zinazoelekezwa kwake na maadui wa humo humo CCM kwa sasa.

Nadhani kikubwa tunachoweza kukiona hapa ni kwamba vita ndani ya CCM kwenyewe imepamba moto, sina data za ndani lakini kwa sisi watazamaji tunaona wazi na kuna ushahidi wa wazi kwamba mpambano upo na ni mkali kiasi cha kuwafanya wanaopambana kushindwa kuficha kucha zao. Ni ajabu leo hii kusikia kila mmoja ndani ya CCM hii hii yenye kujisifu kwa amani kulalama anataka kutolewa roho na mwana-CCM mwenzake, mikwaruzano ya wazi kwenye vyombo vya habari, matukio ya kijangili na ki-ushirikina ya wazi wazi kabisa ni dalili tosha kabisa kwamba sasa mambo yanaelekea kulazimika kukaa sawa. EL kasema hakuna aliye juu ya sheria, kama ni sheria isiwe kwa mmoja tu... yaani anamaanisha kwanini mnafuata yeye peke yake wakati hajafanya dhambi peke yake? kama ni sheria kwanini msianze huko juu kabisa? na kama hamuwezi kuanza huko juu kabisa basi mwacheni aendelee na mambo yake.
 
Wengi wetu tuliokaa mkao wa kula toka jana na kudhani kiranja wa Monduli atamwaga ugali baada ya mpangaji wetu wa Magogoni kumwaga mboga miezi kadhaa ilopita tumepigwa na butwaa baada ya EL kuongelea ajira ya vijana hahaha!

Wakubwa hawakoseagi mazee na mdogo lazima aombe msamha mkubwa anapotangaza kichapo!
 
Mtu ana uwezo wa kukupotezeeni muda hivi halafu mnamdown play kwenye urais.Mtakoma kuwajuwa mafisadi.Na wanaosema eti mwalimu alimkataa kama kigezo,hawajiulizi kwanini JK nayeye alikataliwa lakini bado ni rais wenu?
 
watu wakuogopewa nchi hii kwa unafii, uzandiki na wizi , ni kingunge, msekwa, mkapa, jumanne, el, jk na vibaraka wao ambao wanawatumia kwa wakati tofauti ili kupoteza mwelekeo au kupoza misuko suko yao . kila moja atyakuja na hili mafisadi wachukuliwe hatua nk nk wakati mafisadi wenyewe ni wao wao
 
All in All warudishe mali zetu walizokwiba sitaki kusikia oooh sijui ntawashitaki sijui mnaongea sana rudisha mali zetu full stop.
 
  • Kuna waliofikia kudai eti namhujumu Mhe. Rais. Wengine eti nna mpango wa kumpindua kwenye Halmashauri kuu ijayo. Sina mpango wa hujuma na hata mabaya ya rais Kikwete siyafahamu.
Kwa wenye ufahamu hili ni tusi kubwa sana kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano,kwa kuwa kama Rafiki wa karibu wa Rais mbali ya kuwa Kiongozi hawezi kuamka kuita waandishi wa habari na kuwaambia kuwa ''HATA MABAYA YA RAIS KIKWETE SIYAFAMU''kwa kuwa anasisitiza HAKUKUTA NA RAIS KIKWETE MITAANI atambue kuwa Wananchi wataendelea kumbana kusema UKWELI MPAKA PUMZI YA MWISHO.

Kitendo cha kuchanganya mafaili na kuendelea kukalia kuti kavu au kwenda na kiberiti cha gesi kwenye kituo cha Petroli na kutishia kuwasha sigara asitegemea baadae tena akawaita Watanzania wakati maji yakiwa shingoni kuwa ANATAKA KUSEMA UKWELI kwa KUWA ALIPOONA ANA NAFASI YA KUONGEA UKWELI WA KILE ANACHOKIJUA AKAWACHANGANYA WATANZANIA NA NGONJERA ZAKe ZA UIGIZAJI HATA KWA WATU WAZIMA AMBAO WAMECHOKA KUIGIZIWA.

Yakifika shingoni na akataka kumsingizia huyo aliesema hata Mabaya yake hayajui huku akijua kweli hayajui JE KWANIANI AKATOA KAURI YA KITATA KAMA HIYO ni heri angekaa kimya kama alivyokaa kimya kuhusu Richmond na Dowans.

Wakati wa kuwazuga Watanzania umekwisha watu wameshajua mchezo wa KUTISHANA kuwa ukimwaga mboga mie namwaga ugali.Yule ambae amepewa nafasi na masikio ya watanzania kuwa ASEME kisha AKAKIMBIA KUONGEA MADA na kuishia KUTISHIA WATU WAZIMA NYAU IMEKULA KWAKE .MTU MZIMA MMOJA KESHA ONGEA KUWA DENI LA RICHMOND NA DOWANS LILIPWE NA WALIO JIHUDHURU.

OLE WAKE ALIYETISHIA WATU NYAU KIBANO KITAKAPOZIDI AKATAKA KUWAINGIZA WASIOKUWEMO WAKATI AMESHATAMKA VINGINEVYO HAKIKA HATA KAMA NI KWELI WATANZANIA HAWATAMPA NAFASI HIYO YA KUWAINGIZA WASIOKUWEMO WAKATI ALIPEWA NAFASI HIYO AKACHANGANYA MADESA.

KWAHERI IMEKULA KWAKE MSALA HUO YEYE NA UMMA HAUNA MWINGINE ZINGINE NI NGANO--=KIBANO KAMA KAWAIDA.
 
Heshima yenu wakuu.
Mimi kila siku nasikia Lowasa hashikiki,Lowasa ni kisiki cha mpingu,Lowasa hamna wa kumvua gamba,Lowasa hamna wa kumpinga,Lowasa ndo Rais mtalajiwa na maneno mengi yanaoonyesha kana kwamba bila Lowasa hamna linalowez kuendelea katika siasa za ccm.
naomba kufahamishwa,Lowasa ana nini cha maana hadi achukuliwe kitahadhali kiasi hiki?
kwa upande wangu mimi namuona mtu wa kawaida saana.au kwakuwa alijihuzulu uwaziri mkuu?.mimi naona mh.WENJE ni bora kuliko Lowasa.
naomba kujuzwa.mia
 
Anafata masharti ya mganga wake.
 
Mi nilidhani leo angejibu mapigo,kumbe toafuti! Yaani naona hajagusa yale magumu na mazito sana sana ni kujisogeza karibu na mkuu.Na nilikuwa na hofu siku ambayo yeye angeongea badala short speech within half hour
 
HIvi hamjui kwamba Lowasa ana Shahada ya Sanaa za Maonyesho ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam?
 

Ndugu wana habari, nitakuwa ni mtu wa mwisho kufikiria au kupanga kumhujumu mwenyekiti wetu wa chama na rais ambaye nimemuunga mkono kwa dhati kwa muda mrefu na kushirikiana naye katika harakati nyingi za kifikra na za kiuongozi katika ngazi mbalimbali na kwa miaka mingi. Nilipata kulisema hili na leo nalirudia tena. Mimi na na Rais Kikwete hatukukutana barabarani.

Swali sasa,ina maana kama yeye atakuwa ni mtu wa mwisho,hao walioanza anawajua?Kwa nini awe wa mwisho kama hamna wa kwanza,wapili........?Kumbe mpo kweli mnaomhujumu ila mmegawanyika wakwanza,wapili na wewe EL umeamua utakuwa wa Mwisho!!!Sasa sijui zamu yako itakuwa lini,tunasubiri kwa hamu!!
 

Umenikumbusha maombi yangu huko 2007 nilipoweka agano na Mungu naye akaahidi kuwa lazima mafisadi yatoane roho wao kwa wao ili watanzania wabaki salama bila mikono yao kuchafuka damu ili Jehova aendelee kuwa baba yao na hao waovu wakaungane na baba yao mkuu wa uovu na uasi huko kuzimu.

Nilidhani majira na wakati bado lakini sasa naona saa ya wokovu wa taifa langu ukaribu mno....

Tatizo langu kubwa ni kuwa wale wanaotakiwa ku take charge watakuwa taken by surprise kwamba how comes iwe rahisi hivi kwa Goliati kuangukia pua hata pamoja na mwili wake wote kuwa covered na bullet proof? Wanasahau kuwa God of Israel is a comonder in chief who has never failed in any battle!
 
Wana JF,

Nimeisoma Hotuba yote ya Mheshimiwa Mbunge Lowassa, na nimeweza kuichambua kwa mtazamo wangu na nyie mnisaidie kidogo
Kwanza ni kama ameng'ata na kupuliza, kingine ni kuwa ni kama amejitoa ki-indirect iwapo hakutaka kuonyesha au kum-point mtu yeyote
Ila naamini anajua kila kitu kinachoendelea kwenye siasa, CCM na Serikalini, hata Issue za Richmond, Dowans na sasa Symbion, nasema hivyo kwa sababu amesema mwenyewe hajamjua Rais Barabarani, maana anamjua nje na ndani, iweje aje atuambie hajui madhambi ya Rais ????

Kikubwa ambacho wengi wetu tulitarajia kusikia kutoka kwake ni majibu ya maswali ambayo amehusishwa kwa namna moja au nyingine, hata kama ni kweli au anasingiziwa.

My Take: Bado hajawapa Watanzania kile kitu ambacho tulitegemea kukisikia kutoka kwake,

Napenda Kuwakilisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…