Lowassa aongea na vyombo vya habari; akataa kugusia suala la Richmond/DOWANS

Lowassa aongea na vyombo vya habari; akataa kugusia suala la Richmond/DOWANS

Hiki kitendo cha Edward Lowassa kuanza kushambulia vyombo vya habari inaashiria nini kama si kuwafunga midomo wananchi wa nchi hii kusema ukweli?
Watanzania wanajua Lowassa ni Fisadi, na watu wanasema Lowassa ni Fisadi hawajaongeza lingine, na yeye anataka kuwatishia vyombo vya habari pamoja na wananchi wa nchi hii ili wasiseme lolote.

Lowassa afahamu kwamba watu wamechoka kunyanyaswa, kudhalilishwa na wachache wanaoneemeka kwa kuwanyonya wazalendo wa nchi hii. na hata watu wasiposema mabaya yake, mawe yatasema!

Ametishia kuwapeleka mahakamani wale wote wanaozungumzia mabaya yake, huku kakwepa kujibu masuala muhimu yanayoikabili nchi hususana malipo ya dowans, kagoda na richmond!

Ametuonyesha mapema kuwa hafai kuwa rais wa nchi hii. Akiwa rais vyombo vyingi vya habari hasa ambayo yapo kinyume na yeye yote yanafungiwa maisha!
 
Tunashukuru INVISIBLE kwa kutubandikia hotuba yote ya Lowasa. Nimeisoma yote. Haina cha pekee zaidi ya kuwatisha wanahabari kuwa sasa amechoka kuchafuliwa na atachukua hatua. Maudhui ya hotuba yake kimsingi ni kujiwekea ukuta wa kutaka asisakamwe. Hatoi hoja za kwanini anasakamwa na kuzipatia majibu maridhawa. Ameniboa. Kwa mara nyingine tena amezidi kushusha chati yake katika majedwali yangu ya mizania ya kiongozi mahiri. Sioni ni kwanini tusiendelee kumwandama maana hajatoa maelezo kuhusu hilo. Na wanaomwandama tayari wana sababu nzito ambazo Lowasa hajazitolea maelezo. Tunataka Lowasa atuambie ni kwanini asistakiwe kwa kuliingiza taifa kwenye deni la Dowans akiwa mtendaji mkuu wa serikali (Waziri mkuu) huku tume ya mwakyembe ikimtia hatiani?, kwanini alitaka kututia kwenye janga la mvua za kutengenezwa bila kufanya utafiti wa kina hususan madhara yake kimazingira? Je, asingejiuzulu na mvua zake za kutengenezwa kutupwa si angekuwa ametuingiza kwenye janga jingine kubwa? Ni kwanini asistakiwe kwa kuwa na utajiri mkubwa usioelezeka usiolingana na kipato chake kinachojulikana katika matrix za kiserikali? Ni kwanini asistakiwe kwa kuchukua ardhi ya serikali inayomilikiwa na jeshi la magereza Morogoro na yeye kujijengea hoteli kubwa binafsi ya kitalii? Na yapo mengine mengi. Sisi tuna hoja za kumsakama lakini yeye hana hoja ya kutuzima kwa kutishia kutustaki. Ikiwa ni hivyo, basi tuendelee kumsakama ili aende mahakamani akatujibu hoja zetu maana ameshindwa kuzijibu kwenye press conference. Viongozi wa aina hii ni laana duniani. Ni heri wasingezaliwa!
 
Wananchi wa Monduli wanamwita fisadi. waliwahi kusema Fisadi ni Mkubwa kuliko hata Rais, hajachukua hatua!
Lowassa anadhani wananchi wa tanzania ni wajinga kama watu wa pori pori kule anakowakilisha!
Mtoto ukimtishia anaancha anachofanya, siyo watanzania wa leo!

aluta continue, Mapambano yanaendelea!
 
Mbona kachelewa kuchukua hatua. Halafu hizo ni hatua gani wakati aliyemtuhumu wa kwanza ni Baba wa Taifa. Mbona hakumchukulia hatua yeye? Maskini baba huyu anavuta shuka baada ya adhana ya alfajiri!
 
Wananchi wa Monduli wanamwita fisadi. waliwahi kusema Fisadi ni Mkubwa kuliko hata Rais, hajachukua hatua!
Lowassa anadhani wananchi wa tanzania ni wajinga kama watu wa pori pori kule anakowakilisha!
Mtoto ukimtishia anaancha anachofanya, siyo watanzania wa leo!

aluta continue, Mapambano yanaendelea!

Tena mapambano yanaendelea kwa kasi ya ajabu. Aliyaanza mwenyewe na sas mizimu imetibuka asije akalia.
 
Akakae kijijini kwake hatumtaki ..sisi tunataka Rais mwenye mapenzi na nchi yake ..sio magamba
ila watanzania wenzangu siwaelewi ..akitangaza azima yake utakuta asilimia 85 wamempa kura

Firstlady kama unamashaka na wa TZ basi kuwa na imani na Mungu anye control minds za watanzania wote na mwenye kuweza kusababisha situations zisiwe favourable kwa fisadi yeyote kushinda unless kama tuhuma hizi mbele ya mizani za Mungu zina piga null and void!
 
Kweli Magamba wanasiasa wote ni CRAP!!!!!!!! Unaita watu Monduli kuongea hayo, bora hilo la kujenga viwanda mengine yote ni pumbaaa:shock:

Sijamuelewa huyu mzee. Sasa kipya kipi hapa kupoteza muda wa watu kuongelea obvoius . Jamani what is this ? Oh sijakutana na kikwete barababrani sijui nini,.... sasa mbona hasemi walikutania nyumba , chumba , ofisi au msitu upi? Naogopa tu ban ... hilo tu.
 
Aliposema leo atazungumza na waandishi wa habari wengi tulijua anajivua gamba kwa mustakbali wa chama chake!
Hata hivyo ni afadhali hajachukua hatua hiyo ili chama kizikwe rasmi na yeye akiwa mule mule!
 
Nimeonewa sana,nimedhalishwa sana...na bado tutakuvua mpaka chupi.

Na bado kakumbushia yale yale ya wakati ule, wakati anaanza kuzungumza alianza kwa kusema "Nataka kuweka Kumbukumbu sahihi"

Lowassa amechoka akili
 
...hawezi kuwa rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa sababu:
  1. Aliiba mihela mbele ya baba wa taifa, hivyo akamlaani kwa kusema,
  2. Hafai kuwa kiongozi, na laana hiyo ilimtafuna pale Jk alipo mteua kuwa PM
 
we edward kwani lazima uwe rais? si ulishapiga hela? unataka roho zetu sasa?

Lowassa akiwa Rais watanzani tutatembea na viraka kwenye makalio! Hivi tu anaongoza kwa remote tuko hivi! akichukua basi tumekwisha!
 
Hayo ndiyo ya aliyekuwa Waziri Mkuu! Ama kweli huko mbele ni giza tupu kama tutaendelea kulea hawa Chumia Tumbo.
Nashauri sasa waandishi wa Habari kuchukua hatua,maana hizi style za kuita watu wazima na kuwageuza kama chekechea si nzuri na si yakistaarabu.
 
Ni hatua nzuri sana kuelekea kumhakikishia ushindi Dr Slaa 2015, huyu Mzee Lowassa inaonekana sasa hakamatiki ndini ya magamba. Anasubiria muda ufike tu amdondoshe JOKA LA MDIMU...
 
Kwa tabia yake hiyo ya kutaka kudumaza uhuru wa habari nchini hafai kuwa rais wala yeyote. Anasema uhuru bila nidhamu ni fujo. Nidhamu ipi anayoitaka? Kunyamanzia uporaji wa rasilimali za watanzania?????????????????
 
Hiki kitendo cha Edward Lowassa kuanza kushambulia vyombo vya habari inaashiria nini kama si kuwafunga midomo wananchi wa nchi hii kusema ukweli?
Watanzania wanajua Lowassa ni Fisadi, na watu wanasema Lowassa ni Fisadi hawajaongeza lingine, na yeye anataka kuwatishia vyombo vya habari pamoja na wananchi wa nchi hii ili wasiseme lolote.

Lowassa afahamu kwamba watu wamechoka kunyanyaswa, kudhalilishwa na wachache wanaoneemeka kwa kuwanyonya wazalendo wa nchi hii. na hata watu wasiposema mabaya yake, mawe yatasema!

Ametishia kuwapeleka mahakamani wale wote wanaozungumzia mabaya yake, huku kakwepa kujibu masuala muhimu yanayoikabili nchi hususana malipo ya dowans, kagoda na richmond!

Ametuonyesha mapema kuwa hafai kuwa rais wa nchi hii. Akiwa rais vyombo vyingi vya habari hasa ambayo yapo kinyume na yeye yote yanafungiwa maisha!
hiyo sentensi yako ya mwisho ametuonesha kuwa hafai kuwa rais chonde chonde huyo lowasa hafai hata kuwa mtanzania. Rais!!!!!!! hulo unakwenda mbali sana.
 
Back
Top Bottom