HEKIMA KWANZA
JF-Expert Member
- Mar 31, 2015
- 2,942
- 3,937
Uongo sio mzuri, Leo haikuwa ratiba ya geita ila mamia ya wanageita walikuwa wanamsubiri ikalazima chopa ishuke ili akawasalimie na akawaambia atakuja siku iliyopangwa
Kama uliangalia Taarifa ya habari ITV, LOWASSA aliongea, akasema kuwa miundombinu ya vyombo vya mawasiliano pale uwanjani havikuwa sawa! Unasemaje hakuongea, hata salamu?
Wana GEITA wametuelewa na tutaenda tena kabla ya Kampeni kuisha!
Lowassa is the talk of the Nation and the Next Prezoo of TZ...mark my words..!
Najua mnataka kuzusha kuwa hakuweza kuhutubia kwa sababu ni mgonjwa! Sio kweli hata kidogo!!
Sasa iweje vifaa vya mawasiliano vyenye matatizo Lissu aweze kuvitumia lakini Lowassa asivitumie?....
Maana shida ilianza tangu Chato sauti ilikuwa haitoki (Lowassa) akasema ni tatizo la vifaa vya mawasiliano.....Alivyofika Geita ndio ikawa shida....Ikabidi Lissu apande kutoaa sababu ambazo kimsingi hazikuwa na mashiko kwani vipaza sauti vyenye matatizo ndo hivyohivyo alivitumia kuomba kuahirishwa mkutano na vilikuwa vinasikika vizuri kabisa....
Nimeangalia ITV. Spika ndo zilikua na shida, na lowasa pia alijaribu kuongea, spika zikazingua
UKAWA walipodai kuwa Lowassa ni mwizi na fisadi, ni CCM waliomkingia kifua kwa madai yakuwa ni mtu safi, na kilichotokea ni ajali ya kisiasa tu (Kikwete).
Leo UKAWA wanapomkingia kifua na kumnadi ni CCM hao hao wanapiga kelele kwa madai ya Lowassa ni fisadi mkuu, tuelewe nini???!!. Kwamba alipokuwa kwao poa, Lakini akiwa kwa jirani ni nyoka???!!.
Hatuna muda mrefu tutaelewa sababu ya James Mbatia kukutana na waandishi wa habari usiku usiku! 'vifaa vya mawasiliano!
Hili ndio tatizo lenu kila siku,, maswali magumu majibu yenu huwa mepesi mpaka napata wasiwasi na umri na vichwa vya baadhi yenu eti "spika" mko serious kweli na dola mnaitaka kirahisi hivi??? yaani speaker zinafanya rais wenu ashindwe kuongea na wananchi??? mlikuwa wapi mapema kutojua hizo speaker ufanyaji wake wa kazi?? Muwe serious kidogo mueleweke,,,
Walijisahau kumdunga sindano?
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mheshimiwa lowasa alifika kiwanjani saa 11 na dkk 20. Lakini tukaambiwa mzee anaahirisha mkutano mpaka siku ingine, wakati tunajua huwa hatumii zaidi ya dkk10, kwa nini asingehutumia, mamia ya watu wanalalamika kuwa hawatoi tena kura kwa lowasa, wamekasirika kwa kumsubiri tangu asubuhi halafu ameshindwa kuongea nao..
Sindano nazo zinachoka...!