Elections 2015 Lowassa ashindwa kuhutubia Geita

Elections 2015 Lowassa ashindwa kuhutubia Geita

Nimeangalia ITV. Spika ndo zilikua na shida, na lowasa pia alijaribu kuongea, spika zikazingua
Unachanganya mambo...ITV hawajaonesha Geita Lowassa hajazungumza...Alipozungumza Spika zikaleta shida ni Chato.

Geita mjini ameongea Lissu tu kuahirisha mkutano.
 
Na kuchoka napo kupo hivi wee wafikiria ni kazi ndogo wafanyazo wagombea ? Kusafiri na kutoa hotuba kila ck inachosha jmn
 
Nampenda Hashimu Rungwe yeye Tabora kawaambia kibano mmekiona au bado? Kama hawajakiona, wachague tena CCM. Aliniacha hoi kabisa. Amewambia kibano kitakuwa pale pale na ugumu wao wa maisha utazidi.
 
Lowassa ata akifa tutapigia kula jeneza lake

duu hapo inatisha. yaani kulila jeneza! kwa nini usimpigie kura badala yake unampigia kula! .
ama kweli mashabiki wangu ni wasomi weledi. mtanitaka!
 
Naona watu wa ccm wawili hapa jf wanajitahidi kwenye comments kupambana na nyomi ya Team lowasa. Hamtaweza
 
hizo ni fikra zako mkuu na ninaziheshimu kwa kutumia kipengere cha democrasia ichukue mkondo wake...kupishana kimtazamo ni muhimu katika ujenzi wa nchi...nivyema mkajiandaa kuikosoa serikali ya lowassa iliiwaboreshee maisha kuliko sasa.

Mkuu, unabwabwaja tu ila hoja hakuna, Nakuomba ukae kimya. Eti Mungu Mungu! Kamwambie Mungu kama alimfikiria Lowassa, afikirie upya.
 
Naona watu wa ccm wawili hapa jf wanajitahidi kwenye comments kupambana na nyomi ya Team lowasa. Hamtaweza
Unakosea Chifu...

JF hatupambani....Wala hapatikani mshindi...

Tunasemezana tu kwa lengo la kuwekana sawa....Na kwa nini uwabrand watu wanaotofautiana nawe kimtazamo kama wana CCM?
 
Olala bado tu mnae ?? Kaa pembeni mabadiliko ndio sasa hakuna saa nyingine
 
Kwani Wewe Ndugu Yangu Mzalendo Unamdefine Vipi?Au Mzalendo Ni Yule Aliyesema Fisadi!Fisadi!Fisadi! Nchi Nzima Ikamuelewa,Leo Hii Yule Yule Anakataa Kile Alichokisema Na Kutaka Tena Kuwaaminisha Watanzania Kitu Opposite Na Kile Alichowaaminisha?Au Mzalendo Ni Yule Aliyewajenga Watz Katika Msingi Fulani Leo Hii Yuleyule Anataka Kuubomoa?Mzalendo Ni Yupi Unayemtaja,yule Aliyewaongoza Watu Vitani Na Kushinda Vita Nyingi Dhidi Ya adui Lakini Leo Hii Anamchukua Kamanda Wa Maadui Na Kumfanya Amiri Mkuu Wa Jeshi Na Kusahau Mbinu Zote Walizotumia Kushinda Vita Zilizopita?

UKAWA walipodai kuwa Lowassa ni mwizi na fisadi, ni CCM waliomkingia kifua kwa madai yakuwa ni mtu safi, na kilichotokea ni ajali ya kisiasa tu (Kikwete).

Leo UKAWA wanapomkingia kifua na kumnadi ni CCM hao hao wanapiga kelele kwa madai ya Lowassa ni fisadi mkuu, tuelewe nini???!!. Kwamba alipokuwa kwao poa, Lakini akiwa kwa jirani ni nyoka???!!.
 
hatukumkingia kifua na ndomana tukamkata,tena kwa kisu butu ili afeel pain vizuri na kwa taratibu....
 
Team mafidadi wanahangaika ili kujiokoa na jela ya Magufuli
Hatutaki watu waende jela, haisaidii lolote. Tunataka watu warudishe hela zetu. Ndio maana hatuichagui CCM, haijui vizuri shida ya wananchi ni zipi. Sasa akienda jela akarudi uraiani, hela zilizoibiwa zitarudi vipi? Chagua UKAWA fedha za mafisadi zirudishwe haraka serikalini tena haraka, sio kama CCM wanavyosema eti mafisadi wanarudisha hela kidogo kidogo, eti wakikamatwa nchi itatikisika!
 
Kuna watu humu wanajifanya wana akil sana,tukianza kudodosheana CV hapa itakuwa aibu

"Lowassa ata akiletwa na gar akapunga mkono tu inatosha sana,Hata akifa c tutapigia kura jeneza lake' Tumechoka binafsi naheshmu maamuz ya M/k wa chama.
 
Hatutaki watu waende jela, haisaidii lolote. Tunataka watu warudishe hela zetu. Ndio maana hatuichagui CCM, haijui vizuri shida ya wananchi ni zipi. Sasa akienda jela akarudi uraiani, hela zilizoibiwa zitarudi vipi? Chagua UKAWA fedha za mafisadi zirudishwe haraka serikalini tena haraka, sio kama CCM wanavyosema eti mafisadi wanarudisha hela kidogo kidogo, eti wakikamatwa nchi itatikisika!

He atakaerudisha nani? Huyo fisadi namba moja?!?!?
 
Back
Top Bottom