Mba Ta Sanja
JF-Expert Member
- Aug 31, 2015
- 383
- 44
Leo katika taarifa ya habari ya Channel Ten nimemsikia Rais wa awamu ya tano Ngoyai Lowassa akisema kwamba serikali yake itaangalia jinsi ya kuuvunja mkataba wa bandari ya Wachina Bagamoyo.
Amesema haoni mantiki ya kutumia mabilioni kujenga bandari moja Bagamoyo wakati bandari za Tanga na Mtwara ziko ovyo.
Kama kawaida wananchi wa Tanga wamesema kura zao zote ni kwa UKAWA na adui CCM lazima asome namba mwaka huu.....
VIVA UKAWA!
NOTE: Kwa msio fahamu kuna umbali wa kilomita 1200 kutoka Tanga mpaka Kampala (Uganda) ukilinganisha na kilomita 1500 kutoka Mombasa (Kenya) mpaka Kampala. Lakini Waganda wanatumia bandari ya Mombasa sana kwa sababu Tanga hamna kitu!
Mkuu maelezo yako yanaeleweka. Nadhani Lowasa asiingie madarakani na kusnza kulipiza visasi.Hapa tunaongelea Bandari ambayo inasafirisha Mizigo in bulk ya Uganda, kuwafanya Waganda waache kutumia Bandari ya Mombasa badala yake watumie yetu ni kama haiwezekani kwa maana hatuwezi kufanya huwo uwekezaji, elewa viwanda vikubwa Uganda viko Mji wa Jinja na hapo katikati ambapo ndipo Uganda Railway ilikopita ikitokea Mombasa na inakwenda mpaka Ziwa Viktoria ambako pia kuna Bandari inayoshusha mizigo na kusafirishwa kwa meli, sasa ili kuwafanya watumie Bandari yetu nilazima tufanye uwekezaji wote huwo, sasa kwa mizigo ipi ya maana ya ambayo Uganda wanayo?
It makes alot of sense kudevelop Northern Corridor ya Tanzania (reli na barabara kutoka Tanga mpaka kanda ya ziwa kupitia Moshi-Arusha). Kumbuka kwamba Uganda wamegundua mafuta na wanataka kuyaexport kupitia bandari ya Tanga, hivyo bomba pia litajengwa.
Fanya research kabla ya kuandika. Uganda ni nchi inayoimport goods worth over $4 billion per year, na kuexport $3.2 billion. Hizo ni ndogo kwako?
Na nani alikuambia hiyo corridor itakuwa inatumiwa na Uganda pekee?
Amka ndugu weka uchama pembeni sio kila kitu ni siasa!
Mji wa Kiislam? We nawe umepotea. Hakuna watu wanaokaa kikao kushauriana kwamba tuiue sehemu flan kwa sababu ni ya watu wa dini flani.....hizo ni propaganda umelishwa na probably watu wa CCM!Tanga wameiyuwa kwa makusudi kwa kuwani mji wa kiislam
Kwa sababu hakuwa serikaliniWakati mkataba unaingiwa mbona hakufanya chochote kuzuia??? Mnafiki mkubwa huyo....
Wewe wa ajabu sana, yaani akili zako zinakutuma kua ni sahihi kujenga bandari mpya kabisa Bagamoyo, 60km from dar es salaam badala ya kuzikarabati bandari za Mtwara na Tanga ambazo tayari zipo na zinafanya kazi? Ukiweka ushabiki pembeni ukajiuliza hili swali utajua kama huu mkataba unafaa kuvunjwa au uachwe uendeleeBangi za Arusha mbaya sana.... Kuvunja mkataba ulioridhiwa na serikali mbili si sawa na kuvunja yai viza...
Sijui nani anaemkaririsha Lowassa ahadi, atwambie akivunja huo mkataba fidia atatoa mfukoni mwake.?
Naona Lowassa anazidi kujiweka mbali na ikulu.
Umepata aisee wana sababu zao ambazo mimi na wewe hatuzijuiTatizo unasikiliza maneno ya wanasiasa na kuyaaamini na hapa namaanisha wote wa Ug, Ke na kwetu pia! Hawo wanasiasa wote hakuna kitu wanajua wao wanaongea tu kwa kufuata kile watu kama ninyi mnapenda kusikia na maamuzi wanayoyafanya ndiyo yanayokuja kuzigharimu nchi zetu!
Uganda hawawezi kutumia Bandari ya Tanga kwa ajili ya ku-export mafuta yao ni rahisi kihivyo tu!
Pili Tanzania hatuna fedha ya kuwekeza kwenye Ujenzi wa Reli mpya ya ktk Tanga mpka Uganda pmj na Bandari ili kukidhi soko la Uganda, hayo maneno yote unayosikia ya Bandari ya Bagamoyo hizo siyo fedha zetu ni fedha za ktk Uchina na mtoa fedha ndiyo anaamua ni wapi aweke fedha yake sasa kama wamechagua B'moyowana sababu ingawaje sizijui sababu zenyewe!
Tatu kama ukiniuliza mimi Tanzania kwa sasa hatuhitaji reli mpya ya ktk Tanga kwenda Uganda bali tunahitaji kwanza kuzijenga upya Reli zetu tulizonazo ili zifanye kazi kwa full capacity kama Reli ya kati iende sambamba na kufufua Bandari ya Kigoma ambayo ilikuwa inashusha mizigo ktk kwenye treni na kuipakia kwenye Meli kwenda Zambia, Kongo na Burundi, kufufua na kuijenga upya reli ya ktk Dar kupitia Ruvu na nyingine ktk Tanga mpaka Arusha, hivyo tunapaswa kuanzia hapo kwanza kabla ya kufikiria kujenga Reli ambayo haipo kabisa sijui mpka Uganda!
The same kwa Chuo cha Nelson Mandela kilikuwa kijengwe Mbeya,Lowasa akakihamishia Arusha