Wanaodharau Nguvu ya Lowassa, anawashauri watunze kauli zao mpaka ithibitike kuwa Amebakia CCM, kwa yeye mwenyewe kutamka hivyo. Kinachoendelea sasa hivi ni Lowassa kupima upepo ulivyo, na kadri siku zinavyozidi bila UKAWA kumtangaza Mgombea wao, ndio imani ya Lowassa kupokelewa UKAWA inavyozidi kuwa kubwa.
Naamini, kama Lowassa alijiuzulu RICHMOND ili kulinda mtu au taasisi aliyokuwepo, basi he won't lose anything kwa kuhamia upinzani, kwani atakuwa huru kusema ukweli.Kumbukeni wale 38 waliokatwa CCM sio wote wamefurahishwa na UBABE wa JK, wengi wameamua kufa na tai shingoni, kwa kuwa hawana popularity au politic mightiness ya Lowassa. Wengine ni wachumia Tumbo waliozoea kubebwa, wasioweza kusimama upinzani wakasikilizwa na yoyote yule, kwani ni wepesi sana kichwani. wengine wametega wakisubiria zamu ijayo, wako CCM kimaslahi na kimatumaini. and as long as posibility ya CCM kuendelea kubaki in power, basi hawa watu hata watukaniwe wazazi wao na CCM, wataendelea kung'ang'ana tu CCM.
Lowassa,kwa stage aliyofikia CCM hakuna kitu au cheo anachoweza kupewa, akaridhika zaidi ya uraisi. alipofikia CCM hata wakisema wamteue PM hatakubali, kwani it's not something he aspires anymore. Huyu bwana target yake ilikuwa kuwa Raisi, kama sio, basi angalau ashindanie huo uraisi.Huyu mtu ametumia miaka 20 y amaisha yake kuusaka uraisi, hivyo naamini kabisa, hataona shida kumalizia maisha aliyobakisha kutimiza ndoto yake, na muda pekee kwake ni sasa.
CCM, salama yenu ni kuwa Lowassa awe alijiuzulu bila kumlinda mtu yoyote yule!lakini kama alijiuzulu ili kumlinda mtu au serikali na akaweza kuweka wazi hili kwa watanzania MMEKWISHA.