Lowassa umekuja CHADEMA kwa nia ya Urais au uliipenda CHADEMA kabla?

Lowassa umekuja CHADEMA kwa nia ya Urais au uliipenda CHADEMA kabla?

Dupe

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2013
Posts
1,668
Reaction score
811
Nilikuwa mtiifu mkuu wa CHADEMA, Nililia kwasababu ya CHADEMA ila kinachotekea sasa naona kama vile maigizo tena kwa wasanii wa Bongo Movie…!!!

-Toka lini Lowasa uliihitaji
CHADEMA?
-Kwanini nisiamini uchu na tamaa yako ya madaraka ndio iliyokutoa CCM na nakuja CHADEMA?
-Lowasa ulietuhumiwa katuka kashfa za uuzwaji wa lanch ya taifa…!!, Mvua za Thailand na Richmond pia leo kirahisi tu unatujibu watanzania mwenye ushahidi apeleke mahakaman…??

Mh Chenge aka macho ya Nyoka(Tiga Mumba) karibia kila dili alipiga pesa na mihamala ilionekana mfano ESCROW hajawah fikishwa mahakamani na CCM haohao leo sembuse wewe uliowah kuwa Waziri mkuu…!!??

Mh. Lowassa juzi nilikusikia unashangaa muuliza maswali eti ulistahili kupewa TUZO kwa kujiuzulu…!! Hivi umeona watanzania ni matahila kiasi gani mpaka utuambie upewe tuzo?

Mh. Lowassa nguvu kubwa uliitumia ukiwa CCM na mapesa ukamwaga ukiwa CCM umekosa hiyo chance ya kupeperusha bendela unakuja CHADEMA? Utaendeleza umwagaji hela? Utatumia nguvu ileile? Hivi ni nani alikuambia usipokuwa raisi wewe 2015 Tanzania itakufa?

Mh. Mbowe - hakika nilikuamini sana kuwa mtu mwenye misimamo ya thabiti hupendi masihala ila sasa nimekata tamaa naww kabisa, ingekuwa zile nchi zilizoendelea na kukomaa kisiasa bas leo wanchi wangekisa imani na chama chako na wewe mwenyewe maana umewauza wanachama kwa fisadi papa…!!!

Mh. Mbowe hivi uliwahi jiuliza kwanini Lowasa anautaka urahisi kwa nguvu zote hizo?

Mh. Slaa hakika wewe ni mwanasiasa pekee ambae utaishi katika roho yangu, ki ukweli nitakukumbuka kwa mengi kwa siasa zako komavu na zilizo bora ila ushauri wangu kwasasa ACHANA NA SIASA HIZI ZA KITANZANIA maana zakwako si za kiwango hiki.
 
Ndugu yangu kuwa mpole tu utakapoona Wanachadema wakishangilia kwa ushindi hapo utabubujikwa machozi ya furaha,tumechoka kuwa wapinzani
 
Hapo kawapiga la ubavu hahaha, lowassa ni uroho wa madaraka tu
 
Mtoa mada umeguza ndipo yaani umepiga Pentagon kabisa lazima uambulie mitusi kutoka kwa cdm wa vijiweni..Nimekubali maneno ya Lizaboni kwamba Mbowe si mwanasiasa ni mpiga dili
 
Last edited by a moderator:
Ndugu yangu kuwa mpole tu utakapoona Wanachadema wakishangilia kwa ushindi hapo utabubujikwa machozi ya furaha,tumechoka kuwa wapinzani
Nindoto kwa DJ wenu huyo hahaha sahulini hana akili yaku wapeleka kuleee kalongwa na pesa huyo
 
Objectives za CDM zinamatch na za LOWASSA
So shut up and keep quiet
 
Sasa kama ameona people's power hai-materialize kwanini asiboost na fisadi's power mambo yaende. Sema kawapiga cha juu kingi komaeni.
 
Bwana Dupe umeona mbali sana, haingii akilini MTU ajiunge Leo na chama siku mbili baadae achukue fomu ya kuwania uraisi. Kuna nyuma ya pazia. OK, ngoja tuone!
 
Ningemuona kidume angeenda Tadea au NLD,yeye anakimbilia sehemu tu ambazo anakuta ''ugali upo mezani''aanze kula.
 
Kuna watu vichwa panzi kweli wanahoji vitu kwa ushabiki wa hali ya juu.
Think out of the box fella.
Kuhama kwa Ndg. EL na kugombea uraisi CDM inaonyesha ukomavu kisiasa.
Kwanza inaprove haki ya mwanachama ndani ya CDM kuwa bila kujali muda wako kwebye chama bac wote mna hadhi moja.
2. Inaonyesha CDM/UKAWA si wabinafsi wa vyeo.
3. Hii imebadili kabisa taswira ya siasa Tz na kuprove demokrasia iliyotukuka.
Mwisho kabisa inaonyesha dhamira ya dhati ya UKAWA na EL kufanya mageuzi ya Kisiasa na uchumi
 
Na tujiulize kama amefuata madaraka tu na akiyakosa je ataendelea kubaki chadema?

Nauona mwisho wa chadema kuwa chama kikuu cha upinzani.
 
Sasa c Lowasa ni Fisadi? c mnasema CHADEMA wamempokea Fisadi? Nina imani WaTz wanachukia ufisadi, km Lowasa ni Fisadi basi kaeni kimya nyie Magamba wananchi wataamua, km vp anzeni kushangilia ushindi mwepesi…..
 
mm najiuliza, hiv katiba ya cdm inasemaje juu ya hili? kweli inawezekanaje mtu kujiunga juzi na chama na leo kuchukua form ya urais hivi chama hakikuwa na mtu makini wa kugombea nafasi hiyo ? mbona tunazalilisha viongozi wetu wa cdm.
 
Na tujiulize kama amefuata madaraka tu na akiyakosa je ataendelea kubaki chadema?

Nauona mwisho wa chadema kuwa chama kikuu cha upinzani.

Mie nimeishia kuichoma moto kadi yangu ya CDM ambayo nilipata 2007 nikiwa Chuo, naregret maisha yangu roho yangu imesinyaa sana kwasababu ya Mbowe. Naamini hauwezi ukakaa na mtu ambaye tayari mnatofautiana kisera na k8tikadi, kwa vile itikadi ya CDM siyo ile ya hawari binafsi nimejitoa ili nirudishe afya ya moyo wangu, kuipigania na kuililia nchi yangu siyo lazima niwe mwanachadema kwasababu ni jukumu langu kama mtanzania popot pale ..i love my country, Tz.
 
Lowasa analake jambo na hii nchi.Je ndugu zangu mnakijua hilo.
Tanzania na Watanzania tunapitia katika kipindi kigumu nafikiri kuwai kutokea katika taifa letu. Ni kipindi ambacho tunajiuliza kuwa tumwamini nani? Mbona wale tuliojua kuwa ni watu wa kuwaamini nao wamebebwa na nguvu ya fedha??? Tunapitia kipindi ambacho sio kwamba sie ni wa kwanza kukipitia la hasha hata wenzetu wa Italy na Thailand walishawai kukipitia ila tofauti ni kuwa hizi nchi ni za tofauti sana na Tanzania kuanzia kiuchumi hata kisiasa.

Kwanini nasema hivi?
Kutokana na hali halisi kuwa Tanzania ni nchi ambayo kimaendeleo tunaweza kusema kuwa ni kama ndege iliyo kwenye njia yake kuelekea kuruka, yaani ni nchi ambayo inafunguka zaidi kifursa kiasi ambacho kwa watu wakubwa wa ndani na wa nje imegeuka kuwa sehemu wanayoiangalia sana. Hii imetokana na fursa za maliasili, madini ambayo inasemwa hadi leo yaliyochimbwa ni asilimia 10 tu na mafuta na gesi.

Kwa matajiri na watu wenye nguvu ya kifedha ambao wanataka waendelee kumaintain status quo yao au wanataka waendelee kukua zaidi na zaidi wanajua kuwa wakiweza kuikamata Tanzania leo basi watakamata hizi fursa zote na siku ya mwisho Forbes itawatambua.

Matajili ni watu wenye akili sana na wanajuaga sana mahali popote pale, ukitaka kula mema ya nchi basi kikubwa ni kwa gharama yeyote ile muwekeni mtu wenu kwenye top post ya hiyo nchi. kwa nchi zingine top post kiserikali ni waziri mkuu kama italy na Thailand ila kwa Tanzania ni RAIS. Ukishamuweka tu malengo yako yote ya kibiashara yatatimia.

Kama nilivosema hapo juu kuwa yanayotokea leo Tanzania sio yameanzia hapa la hasha yameanzia huko mbele na mfano mzuri ni italy ambapo kulikuwa na Bilionea ambaye sasa yuko jela anajulikana kama Silvio Berlusconi na Thailand kulikuwa na bilionea anayejulikana kama Taksin Shinawatra. Kwa msio wafahamu hawa watu hawa ni matajili wakubwa sana na walitumia sana nguvu yao ya pesa kutengeneza ushawishi wa kisiasa kwenye nchi zao, kwa Thailand ilibidi jeshi(system) iingilie kati kumuondoa Shinawatra ila kwa italy ilibidi wapate msaada wa nje ili kuweza kuiharibu syndicate ya bwana Silvio Berlusconi na hata leo hii wanashukuru ni bora ameondoka na yuko jela.

Hali ilivokuwa Tanzania sasa:
Kwa hapa Tanzania kuna syndicate ilishajipanga tangu mda kuwa lazima mwaka 2015 tuweke mtu wetu. N i kundi kubwa lenye nguvu ya pesa tena sio kawaida ni sana ambalo lilijipanga kisawa sawa kuwa lazima tuikamate CCM na tuiforce imuweke mtu wetu. Walijipanga vizuri sana kuanzia makanisani, misikitini, bodaboda hadi vyuo vikuu. KWA KIFUPI walimpa mtu wao fedha nyingi sana ili ajenge ushawishi kwa sababu walijua weakeness kubwa ya watanzania/waafrika(na binadamu kwa ujumla) ni fedha. Zilitolewa hela zisizo za kawaida makanisani, misikitini na hata meeneo mengi kama bodaboda na vyouni, walitafutwa wahariri wa vyombo vya habari wakaongwa fedha nyingi sana na kwa kifupi hawa watu waliweza kununua asilimia 90 ya vyombo vya habari.

Walivofika dodoma walikuwa na uhakika kuwa iwe isiwe lazima nguvu ya fedha itatamalaki kiasi ambacho mtu wao atapita ambaye ni EL. ila hamadi kilichotokea dodoma kila mtu anakijua kwa sababu CCM walishtuka kuwa tunakoelekea tutakuja kulaaaniwa na vizazi vyote vijavyo vya watanzania kwa sababu hawa watu sio watu wazuri na hawana nia njema na mama Tanzania ikabidi kutokana na hali ilivokuwa waseme inatosha na lazima kweli ya haki ishinde dhidi ya fedha chafu.

Wakamkata na wakaamua kumchukua mtu aliyekuwa hana makundi, hajawekwa na wenye fedha na hana wa kumlipa fadhila wakati atakapokuwa anaendesha nchi yaani John Pombe Magufuli mambo yakatulia.;

Kwa upande wa hawa watu kibaya zaidi hawakuwa na plan b kwa upande wa CCM, walitawanyika ila kiongozi wao na mtu wao kwa sababu yeye nia yake kuu ni kuingia magogoni tu wakasema lets go the other side. Walijua wanayo pesa na wanayo pesa na kiukweli kwa upande huo hamna anayeweza kushindana nao, wakaenda kuwashawishi viongozi wa upinzani. Kuna taarifa zinasema kuwa walikubaliana kugharamia kampeni yote kuanzia uraisi hadi ubunge ya upande wa pili, walikubaliana kuwawezesha upande huo kifedha na viongozi wa upande huo waliwekwa sawa kifedha.

Ukiliangalia hili suala juu juu unaweza kufikiri ni jambo la kawaida sana ila hapana. Kuna kitu hapa ambacho watanzania lazima waamke na wakione nacho ni hadi hawa wameweza kuingiliwa na fedha???????

Katika dunia ya leo mwanasiasa anatakiwa awe mtu predictable na asiwe mnafiki kiasi ambacho mtu aliyempa kura anatakiwa awe na uhakika nae kuwa nilimpa kura huyu mtu kwa sababu anaamini katika A, B, C na hizo ndo zilizonishawishi mie kumuamini na kumpa nafasi kwenye akili yangu.

Mwaka 2007/8 Chama kilichojijengea sifa kubwa nchini Tanzania Chadema kilitoa kile kilichoitwa The list of Shame ambapo walitoa majina ya watu 11 wao waliowataja kuwa ni mafisadi, wanaolitafuna taifa na kuliangamiza taifa. Walisema kuwa wana ushahidi kamili usio na shaka juu ya hawa watu na kama hawa watu wanabisha waende mahakamani. Walisema hawa watu hawastahili kuwa mitaani sehemu wanayostahili kuwa ni jela. Na hiki ni kitu kilichowapa public trust ya kiwango cha juu kabisa, hiki ni kipindi ambacho chadema ndo ilianza kujijenga mioyoni mwa watanzania kuwa ni wakombozi wa kweli, watu wanaongea ukweli, sio waongo na yote wanayosema ni kweli tupu kwa hiyo ndo watu wanaostahili kupewa nchi.

Chadema hawakuishia hapo walizunguka nchi nzima kwenye mikutano na kampeni mbalimbali wakiendelea kuitaja iyo THE LIST OF SHAME, ambayo no 9 alikuwapo Edward Lowassa.

Sio huyo tu washirika wa Lowassa yaani mzee wa vijisenti na the Kings Maker Rostam Azizi washawai kutajwa na Chadema kuwa ni watu mafisadi na wasiofaa.

Kichwa cha mada kinasema ni ulaghai, unafiki na uzandiki kwa sababu pamoja na hiki chama kumtaja huyu mtu ila viongozi wao wamekula matapishi yao wenyewe na leo wamempokea huyu Lowassa na wanamnadi kuwa ni mtu safi, mwenye weredi na anayefaa.

Kuna kitu kimekuwa kikiendelea kwa hawa viongozi kutoa majibu mepesi eti siasa ni dynamics na sio static eti mtu unaweza kubadirisha gia angani wakifikiri watanzania ni mambumbumbu sana kiasi ambacho hawawezi kuhoji na hawafuatilii mambo yanayofanyika duniani huko.

Napenda kuwaambia viongozi wa Chadema kuwa katika siasa za 21st century mwanasiasa akisema jambo alafu ikitokea otherwise au ikitokea tofauti na alivosema au kuuaminisha umma uwa anajiuzuru. Mfano wa haya ni kama ilivotokea juzi Scotland pale waziri mkuu na kiongozi wa chama cha Scotish National Party alipojiuzuru nafasi zake zote baada ya kile kitu alichokuwa akiwaaminisha wascotland kuwa nchi yao inafaa kujitenga kufeli kwenye referundum. Sio huko tu hata England Ed Milband nae baada ya chama chake kushindwa kwenye kushawishi kitokana na sera zake alibidi ajiuzuru. Huu ndo ustaarabu mpya kwenye siasa kwa kifupi siasa za dunia ya leo ni kuwa endapo mwanasiasa ukisema jambo fulani lile jambo likija tokea tofauti na ulivouaminisha umma au chama chako inabidi ujiuzuru.

Sasa kwa Chadema na ukawa what thet were supposed to do ni kuwa kabla Lowassa hajatambulishwa rasmi au soon after kutambulishwa wale viongozi wote waliokuwa wanauaminisha umma na kudai wana ushahidi juu yake kuwa ni fisadi walitakiwa kula matapishi yao kwa wao kujiuzuru nyadhifa zao zote ndani ya chama chao na kuomba msamaha kwa jamii ya Tanzania kwa upotoshaji mkubwa walioufanya.

Ila kwa majibu mepesi wanayoyatoa kama aliyatoa jana Mchungaji Msigwa kwenye kipindi cha Madamoto, kama aliyoyatoa Lema au kama aliyoyatoa Lissu na ziadi na zaidi kama aliyoyatoa mwenyekiti wao Freeman Aikael Mbowe wakati anamkaribisha Lowassa basi its obvious kuwa HUU NI ULAGHAI, UNAFIKI NA UZANDIKI ULIOTUKUKA.

Nakataaa kudharauliwa na viongozi wa ukawa kuniona mie siwezi kufikiri ila wao ndo wanaweza kufikiri kwa niaba yangu.....

Tukutane Oktoba.

MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATANZANIA.
 
Back
Top Bottom