warumi
R I P
- May 6, 2013
- 16,218
- 18,440
Msanii aliyefunga pingu za maisha juzikati na mwanaume mwenye asili ya Denmark , Janus Stanley Landrock , Lucy Komba amesema kadri siku zinavyozidi kwenda anazidi kunogewa na mapenzi ya mzungu wake na kuwaona Wabongo si lolote kutokana na kuwa waongo.
Msanii wa Bongo Muvi , Lucy Komba akiwa na mume wake mdenmark , Janus Stanley Landrock. Akieleza la rohoni mbele ya paparazi wetu, Lucy alisema anatamani angefahamiana mapema na mzungu huyo kuliko kuyumbishwa na mapenzi ya Kibongo ambayo yamejaa ahadi nyingi za uongo , tofauti na watu wa asili hiyo ambao wana msimamo mkubwa katika mapenzi .
"Nilipopataka siyo siri nimefika, kama ulaghai nishakumbana nao sana katika mapenzi ya Kibongo ambayo yalinikinaisha mno , lakini sasa sina mawazo kabisa katika haya mambo, wenzetu hawapendi kuchepuka hovyo akikupenda , anakupenda kweli ," alisema Lucy .
