Ole jaminati
JF-Expert Member
- Sep 23, 2021
- 284
- 251
30 December 2025
Aliyewahi kuwa kada wa CHADEMA, ndugu Ludovick Rwezaura ameibuka leo na kulishambulia vikali Kanisa Katoliki kwa kuikosoa Serikali ya Rais Samia...
Fuatilia:
đź”´#LIVE:LUDOVIC LWEZAURA ANALISHAMBULIA KANISA KATOLIKI MUDA HUU, KWA KUIKOSOA SERIKALI YA SAMIA
View: https://m.youtube.com/watch?v=0K9HbIrg5bE
Ajitambulisha kama muumini wa kanisa katoliki, aliyebatizwa na anayepokea sakrament, Ludovick Joseph Rwezaura, amekosoa mwenendo wa hivi karibuni wa viongozi wa dini waandamizi ...
Anasema Kanisa Katoliki lina kashfa nyingi ikiwemo kutokusoma mapato kwa waumini (Cannon Law)...
Anasema mwaka huu Jimbo Kuu la DSM limekusanya Bilioni 5, lakini Askofu Ruwaichi hakuwahi kusoma taarifa...
huku akisisitiza kuwa tafakari hiyo haitokani na chuki wala uasi.
“Mjadala huu unatokana na imani kwamba, pamoja na kanisa kuanzishwa na Kristo, viongozi wake ni wanadamu wenye mipaka na wanaoweza kukosea, hivyo wanapaswa kuongozwa na Injili, unyenyekevu na mfano wa Kristo mchungaji mwema”,Amesema.
Akinukuu Sheria ya Kanisa (Canon Law), amesema waumini wanatambuliwa kisheria kuwa na haki ya kutoa maoni, ushauri na malalamiko yao kwa wachungaji wa kanisa kuhusu masuala yanayolihusu kanisa huku akibainisha kuwa hatua hiyo si uasi wala dhambi inapofanyika kwa kuzingatia misingi ya kanisa.
Katika tafakari yake, Ludovick Joseph Rwezaura amekemea matumizi ya madhabahu kama majukwaa ya siasa au lugha za matusi, akisisitiza kuwa mahubiri ya Kikatoliki yanapaswa kubaki kuwa chombo cha kufundisha Injili na kuimarisha imani ya waumini.
Aidha, mjadala huo umeibua hoja ya uwajibikaji na uwazi wa kifedha ndani ya kanisa, ambapo Ludovick Joseph Rwezaura amesema baadhi ya waumini wamekuwa wakihoji matumizi ya sadaka na michango yao, huku sheria za kanisa zikihimiza utoaji wa taarifa kwa waumini.
Akihitimisha, Ludovick Joseph Rwezaura amesema mjadala unaoendelea unapaswa kuchukuliwa kama fursa ya kujitafakari na kujijenga upya, akitoa wito kwa viongozi wa kanisa kuongoza kwa unyenyekevu na kwa waumini kuendelea kushikamana katika sala, amani na upendo kwa ajili ya mustakabali wa kanisa na taifa.![]()
![]()
![]()
Huyo jamaa elimu yake ikoje ? Kama ana njaa akachukue buku 7 zake pale lumumba na sadaka yake sio lazima na madhehebu yapo mengi ahamie huko