PostGE2025 Ludovick Rwezaura alishambulia Kanisa Katoliki kwa kuikosoa Serikali ya Samia

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Hoja yako hapa ni nini?
Naona umetoa uwezekano wa Askofu kuondolewa madaraka ya kuliongoza Jimbo(japo Kwa msaada wa AI). Ni kweli uwezekano huo upo japo si rahisi hivyo isipo kuwa kwa grave reason. Ukiondoa sababu ya umri na afya(za kawaida) lakini sababu kuu Askofu kuondolewa madaraka ni Imani(yaani kuasi Imani au kufundisha mafundisho potoshi) na sababu za utovu wa maadili) hizi ndizo grave reason tena mambo yanaenda kimyakimya bila ushabiki na mbwembwe Wala huwezijua kirahisi. Lakini si kwa mambo ya Sasa hivi😆 ni maigizo tu haya. Mchakato wa kumpata Askofu ni makini sana, Askofu ni Ishara ya uwepo wa Kanisa kumwakilisha Kristo.

Utimilifu wa Jimbo ni uwepo wa Askofu. Canon law imempa Mamlaka kama Mchungaji mkuu, mwalimu mkuu na kiongozi mkuu wa Jimbo akisaidiwa na mapdre wake. Ndio maana Mamlaka ya kumshughulikia Padre ni Askofu wake kwanza na si Vatican. kama wale waliopeleka barua Kwa Nuncio.

Uaskofu ni Sakramenti, anaweza ondolewa tu Mamlaka ya kuliongoza Jimbo ( with a grave reason) ila Uaskofu hauondolewi na mtu yeyote akiwemo papa. Ni alama isofutika.
 
Na hao wanahabari hawana kazi? Utaendahe kumpa airtime mtu tapeli kama Ludovick?

Ignore this mind crippled creature.
 
Who is Habibu Mchange?
 
Info za ndani zaidi
Jina la baba yake : Lwazaura

Jina ake ; Joseph

Mkoa kuzaliwa ; Bukoba

Kabila : Mhaya

Watoto : 2 na 1 (private)


Dini ; Hasi katoriki toka 2009

Kazi : Uwalimu

Chama : CCM

Kadi yake ya Chama : 896-921**

Namba za simu : (Hidden file)

Makazi : Dodoma

Elimu ; Kozi fupi ya theology ya biblia baadaye akafukuzwa chuoni kwa makosa ya kinidhamu kabla hajamaliza

Askofu wake ; Kinyaia wa Dodoma

Amewahi kufundisha shule ya secondary ya St. Mary's High school ya chang'ombe baadaye kafukuzwa na hapo na kukimbilia dodoma kugombea udiwani, kwa bahati mbaya hakuweza kupita.
 
Hawa wanafadhiliwa na mtoto wa yullr mama....Kanisa katoliki ni wastaarabu sana. Wangeweza kuanika mambo mengi ya yale mauaji ya tarehe 29 ila wamenyuti tu. Vyombo hivyo vya habari huwa vinajaa hata kwa wakata vichwa
TEC hawana any classified info zaidi ya walizosema. Amini hivyo ndugu yangu. Kimsingi mbinu zote wameishiwa, wamebakiwa na mbinu ya kuchochea tu kupitia majukwaani na ile ya kwenda kushtaki Vatican, na Vatican iziambie mamlaka zake za ulaya waweke vikwazo hewa kwa Tanzania au kama kinachoendelea Naigeria na Venezuela. Hivyo kama unaamini kuwa TEC wana habari nyingine ya maana zaidi kuhusu tarehe 29, umajidanganya mwenyewe.
 
AI IPO kutusaidia kujua mambo ambayo hatuyafahamu. Naona watu wengine wanabeza matumizi ya AI. Msaka maarifa atatumia njia zote ili ajifunze, hata comment Yako ni shule pia kwetu.

Ludovick pamoja na mambo aliyobwabwaja ana hoja ndani yake. Si kweli kuwa Askofu ana Kinga kiasi wanavyofikiri hususan matumizi ya fedha za Jimbo etc.

Kuhusu kukemea yaliyotokea 29/10 TEC wapo sahihi na ni wajibu wao. Kwanza nilitegemea waende mbele zaidi waoneshe hata data sahihi za waliokufa kutoka katika hospitali, vituo vya afya na zahanati zao.

Kwa waliopeleka malalamiko Yako kwa Balozi wa Vatican nchini, nao ni haki Yao. Kuwabeza na kuwabananga si sawa. Kila mtu ana uhuru wa kufanya atakalo bila kuvunja Sheria!

Naamini umeona ni kwanini nilihangaika kutafuta AI isaidie katika Hili na imefanikiwa kwa kiasi chake. Hakuna anayesema waliopeleka malalamiko Wana nia ya kuona mfano Askofu aliyetamka ulofa avuliwe madaraka, la hasha ni kujaribu kumkumbusha kuwa naye ana mamlaka ya nidhamu.

Heri ya mwaka mpya!
 
Sio tu Askofu hata papa anaweza wajibika ila kwa (grave reason hasa ( kama kuasi Imani mf. Askofu Mkuu Milingo) na si porojo kama hizi). Kinachoendelea Sasa ni maigizo tu na ni nje ya utaratibu wa Kanisa (mazingira si sahihi yanayo onyesha kbs yana nia ovu ndani yake) yule bwana alisema ameitumia lesser evil kuita press, lakini kimsingi hakukua condition yoyote kujustfy press kuwa ni lesser evil dhidi ya uovu mkubwa ambao ungefanyika endapo asingeta press (aliyo andaliwa). nikuonyesha tu term hiyo anaijua ila ameitumia kinyume na matakwa yake kama maadili yanavyo dai.

Halmashauri za walei wanafahamu zaidi wanavyo tatua matatizo na wachungaji wao na namna wanavyo ratibu mambo ya fedha. Na kimsingi mambo ya fedha yapo chini ya walei siku hizi. Pia inakuhitaji uwe na full communion with church ndipo canon law in bind kwako. Huwezi tumia canon law kama huna ushirika kamili na kanisa.

Sasa hao wanachofanya ni nje ya utaratibu ( press ndio Mamlaka?). Motive zao ni ovu.
 
Ludovick31????
 
Mkuu ulipata majibu ya maswali hayo?
 
Sasa kuliko kujisemea humu tu, kama lina kashfa nyingi, kama anavyodsi, kwa nini asiende kushtaki polisi au achukue hatua ya kulishtaki kwa Balozi wa Papa nchini kama wenzake "wawakilishi wa Wakatoliki" walivyofanya? Nani anamzuia? Kama yeya ni Mkatoliki na Kanisa lake Lina kashfa nyingi, yeye amechukua hatua gani Kanisa liwe safi kama yeye alivyomsafi? Na kwa nini kwa usafi wake huo, aendelee kuwa kwenye Kanisa lenye kashfa. Labda atusaidie logic yake ni nini?
 
Mkuu ulipata majibu ya maswali hayo?

Mkuu njoo tunywe bia nipo keko ya juu ,bar ya giraffe ,ukifika muite muhudumu mwambie namtafuta nyoka .
Atakuleta Kwa bwana mmoja kipara kikubwa ,tumbo kama pipa la ulanzi na mfupi kama watu wa congo hapo jua umenikuta ,uje tufurahie kaka ,ya kale yalishapita kaka Sasa yamebaki historia
 
Asante mkuu, ila jamaako bado anasumbuwa, bado anafurahia shida za wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…