mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,309
- 4,798
Mwaramutse nshuti,
Mimi sina magari matatu kama ndugu yangu Makamura hivyo hulazimika kutumia usafiri wa umma kama daladala na bajaji kwenda kusaka mkate.
Adha kubwa ambazo nimekuwa nikikutana nazo kwenye usafiri huo ni maneno machafu, yasiyo na staha ya makonda na madereva. Imekuwa kama mtindo kwao, yaani kutamka hadharani maneno yanayohusisha sehemu za siri za kike imekuwa suala la kawaida sana kwao.
Hawajali jinsia, rika, hadhi ya waliopanda kwenye vyombo vyao vya usafiri, wao wanatukana tu bila aibu na kujiona wajanja. Mungu awasamehe.
Kuna siku nipo na kijana wangu ana miaka 7 tumeenda kupanda bajaji. Dereva bajaj kazinguana kidogo na mwenzake kisa abiria, aisee aliporomosha matusi hayo tena akitaja sehemu za siri za kike. Kiustaarabu nikamwambia bro hayo matusi yako naomba usitishe, huoni kuna mtoto? Eeeh si nakageuziwa kibao mimi nikatukanwa mbele ya mwanangu.
Jana mishale ya saa tatu nimekwea daladala ya Segerea, sasa ukishavuka Barakuda kuna foleni matata kutokana na ujenzi unaondelea Segerea Magereza. Dereva kachomekeana na kishandu mmoja, dereva kaanza kuporomosha matusi, sikupendezwa ikabidi kiustaarabu nimuulize, Bro tokea nipande hii gari pale Mwenge wewe ni matusi ya nguoni, hivi huna mama, dada, watoto wa kike? Nikaishia kutukanwa kuwa nina sura mbaya kama uchi wa mwanamke. Abiria wengine wakaishia kucheka. Kiustaarabu nikashuka na kukwea pikipiki nikaendelea na safari.
Hii ni mifano michache kati ya mingi ambayo nimeshuhudia. Hali ni mbaya sana, pamoja na vijana kuvurugwa lakini isiwe sababu ya kuondokewa na utu. Siyo kila mtu anapendezwa na lugha hizo, wengine tunataka kizazi kilichostaharabika.
Murakoze cyane.