A
Anonymous
Guest
Mitandao ya kijamii imekuwa na athari kubwa kwa watumiaji zikiwemo zenye matokea chana na zingine matokea hasi.
Moja wapo ya manufaa chana ni namna ambavyo mitandao ya kijamii imesaidia utangazaji wa biashara mbalimbali mitandaoni na upatikanaji wa bidhaa mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii. Biashara kama za mavazi, chakula, huduma na kwa sasa hata udalali wa nyumba za kupanga.
Upatikanaji wa nyumba za kupanga umekuwa rahisi kupitia mitandao ya kijamii. Vijana wanaoanza maisha wakiingia vyuo vya ngazi mbalimbali wamepata wepesi wa kupata nyumba kupitia mitandao ya kijamii. Lakini wapo wale wadogo ambao bado wapo sekondari nao wanapata uzoefu wa namna ya utafutaji wa vyumba, nyumba, viwanja, nk. Hivyo kuwajengea uzoefu pale watakapohitaji kwa siku za usoni.
Lakini kuna athari moja ambayo ninaiona ambayo huenda watu wakawa wanachukulia kawaida au masihara.
Kumekuwa na mtindo wapo madalali kutangaza nyumba na kutumia maneno kama “Hii ya kufichia nyumba ndogo” “Hii ya kumuweka Kibenteni”. Lugha hii ina athari kubwa sana kwa jamii. Kuna watu kadhaa ambao wanashuhudia kuwaza tofauti (kupata mtazamo tofauti/hasi) baada ya kuona mambo kama hayo na kuhisi kumbe inawezekana? Siku hizi wanatumia neno “Naenda kwa familia yangu kule Madale”.
Athari hii sio kwa vijana wadogo pekee bali hata kwa watu wazima. Maneno kama hayo yakitumika yanaweza kuinua hisia za kutenda jambo kama hilo na kuibua athari zaidi kama utengano katika ndoa ambao mara nyingi huathiri watoto. Sambamba na hilo inaweza kuchangia katika ukatiri wa kijinsia na muongezeko wa talaka (divorce) endapo jambo hilo litatekelezeka na kugundulika.
Kwa upande mwingine inaweza kupelekea ugomvi usio wa lazima endapo aliyepangishwa akikutwa na mtu mwingine (hili limeshuhudiwa mara nyingi huko mtaani).
Nitoe wito kwa mamlaka husika kulifuatilia suala hili ili kuweza kuleta uweledi katika matumizi ya mitandao. Madali pia ni vyema waache tabia hiyo na kuzingatia utangazaji wa biashara zao bila kuathiri watumiaji hasa vijana wadogo ambao ni rahisi kujifunza na kuiga vitu.
Mitandao ya Kijamii ni sehemu ambayo inaongoza kwa usambazaji wa taarifa kwa watu wengi na kwa uharaka zaidi hivyo athari zake pia huweza kuwa kubwa zaidi endapo mamlaka zitashindwa kufuatilia mienendo ya watumiaji.
Nukuu:
“Teknolojia yenyewe si nzuri wala mbaya, lakini jinsi tunavyotumia ndiyo inayotufanya kuwa hivyo.”“Technology itself is neither good nor bad; it’s how we use it that makes the difference.”
— David Wong (Mhariri Mtendaji—Craked.com)