Lugha za wanawake zinavyowachanganya wanaume

Lugha za wanawake zinavyowachanganya wanaume

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
6,514
Reaction score
15,247
Habar wana JF,

Wanawake Wana lugha zao flan hivi ambazo huwachanganya Sana wanaume wengi, unajua inakuwaje? Nakupa mchongo ufuatao, wanachoongea Sicho wanachomaanisha na hapa ndo wanaume tunapo katishagwa tamaa na hawa viumbe kutoka Venus.

Unajikuta unajitoa Kwa nguvu zote kumcare mkeo lkn mwisho wa siku unapewa kauli Fulani ambayo kama inakufanya ujione kama vile hujawahi mfanyia mema hata moja, sasa kwa Sisi wanaume ambao hatuzijua lugha zao tunabakia na maswali kibao kichwani, usihofu Leo ntakupa mbili tatu ambazo zitakufanya ujue lugha za hawa viumbe na uache kuteseka.

Unaweza kuta mwanamke anakuambia yaani siku hizi hunipendi kabisa! Sasa hapo Mzee Baba unajiuliza Khaa inakuwaje mbona namfanyia vitu vingi ambavyo vinaonyesha mapenzi yangu kwake,daah anataka sasa mm nifanyeje,usipaniki broo! Hapo mwanamke anataka kusikia toka kwako neno nakupenda,so kama hujamwambia siku nyingi kuwa unampenda basi ujue hapo ana kiu na Hilo neno ajisikie kuwa anapendwa.

Anaweza kukwambia yaani siku hizi hatutoki kama zamani, daah ukivuta kumbukumbu zako ni kama wiki mbili hivi zilizo pita mlienda samu wea na Kula BATA, unaweza kudata ujue, chil broo! Hapa ujue siku hiyo huenda kavurugwa so anakupa ujumbe muende out akau mwagilie moyo wake apate Amani, hawa viumbe bhana inabidi uishi nao Sana Kwa akili la sivyo siku zote waeza panic mke wangu kila nikimfanyia hivi mbona kama haridhiki hivi! Hapana ni wewe Tu hujaelewa lugha zao.

Ebu Kwa Leo ishi na maelezo hayo machache,na uanze kujifunza kujua lugha zao la sivyo mkulungwa uta go MAN DOWN fasta Tu.

Ni hayo tu.
 
Tusiwaelewe tuishi nao kwa Akili tu
IMG_20220701_104625.jpg
 
Mwanamke ukishamuoa na kumtelekeza ghetto hutakiwi kuumizwa nae tena bichwa hata kama una bichwa kubwa kama la magufuli wa masoud Kipanya
 
Kila siku mada kuhusu wanawake tu! Kuishinao kwa akili,akili,akili!!!! This song is boring now.
Kila mtu apambane na bomu lake.
Inaonekana hapa kuna vijana wengi wa 18 to 22 years. Hili kundi huwa linapenda sana hiyo mijadala. Mwanaume akishafikisha above 30, mijadala inapungua, kazi yake inakuwa ni action tu.
 
Ongeza nyama nyingi mkuu hayo machache sio kitu kabisa
Nitakuja na episode 2....kujua zawadi ina score point ngapi Kwa wanawake na wanawake wakikwambia matatizo Yao wanatarajia nini, I will be back!
 
Mpaka leo haijulikani waliongea nini na shetani kwenye bustani ya eden, tutulie tuwe nao makini.
 
Back
Top Bottom