GE2025 Luhaga Mpina agoma kutishiwa nyau. Achukua fomu kugombea Jimbo la Kisesa

GE2025 Luhaga Mpina agoma kutishiwa nyau. Achukua fomu kugombea Jimbo la Kisesa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
143,138
Reaction score
288,731
Aliyekuwa mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kutetea ubunge Jimbo la Kisesa Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu, leo Jumatano Julai 2, 2025.

Mpina amekabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa CCM Wilaya ya Meatu, Nabothi Manyonyi.

=========================

Mbunge ambaye Jimbo lake bado linamdai Rais Samia, leo amechukua fomu kuomba ridhaa ya kuchaguliwa Tena, Bila kujali vitisho

Screenshot_2025-07-02-15-26-29-1.png


Angalizo: Sifagilii mambo ya CCM ila wakiparulana na kulogana huwa nachekelea
 
Dah,
Inaweza kuwa kama sakata la FAM alivyotaka kumtoa TAL kinyemela, mwishowe ikawa kinyume chake
 
Mbunge ambaye Jimbo lake bado linamdai Rais Samia, leo amechukua fomu kuomba ridhaa ya kuchaguliwa Tena, Bila kujali vitisho

View attachment 3391407

Angalizo: Sifagilii mambo ya CCM ila wakiparulana na kulogana huwa nachekelea
Kwa kweli mimi sikuona sababu ya rais kukasirika vile huyu mbunge aliwasilisha kero direct kwa mwenye nchi maana ukipata nafasi kama hizo tumia hapohapo..

Rais pale angetumia mwanya huo kuwaomba wanachi wapige kura kwa wingi ili kero hizo azimalize kabisa 2025 2030 sasa mambo yakaenda ndivyo sivyo..anyway kila jambo na wakati wake na kila uongozi na nyakati zake.
 
Mbunge ambaye Jimbo lake bado linamdai Rais Samia, leo amechukua fomu kuomba ridhaa ya kuchaguliwa Tena, Bila kujali vitisho

View attachment 3391407

Angalizo: Sifagilii mambo ya CCM ila wakiparulana na kulogana huwa nachekelea
...kuomba ridhaa ya kuendelea kumdai kwa niaba ya Wananchi wake!. Ila Mpina kama sio mtz vile ule ujasiri wa kuvuruga ziara ya watu sijui aliutoa wapi?🤣
 
...kuomba ridhaa ya kuendelea kumdai kwa niaba ya Wananchi wake!. Ila Mpina kama sio mtz vile ule ujasiri wa kuvuruga ziara ya watu sijui aliutoa wapi?🤣
Nsukuma huyo baah! Jamaa Katisha, namuombea Mungu ampiganie!!

Na wakilazimisha kisesa inajitenga kama nchi😁😁😁
 
Back
Top Bottom