Luhaga Mpina alikuwa Waziri Kigeugeu. Je, vigeugeu wanatufaa kama Taifa?

Luhaga Mpina alikuwa Waziri Kigeugeu. Je, vigeugeu wanatufaa kama Taifa?

GUSSIE

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2014
Posts
3,880
Reaction score
11,134
Huyu ni moja ya waasisi wa falsafa ya "wewe ni wewe daima hakuna kama wewe baba hapa Tanzania"

Luhaga Mpina ni vigeugeu kama vigeugeu Wengine, Huyu anatafuta chakula.

Alipiga kelele wakati huo akapata uwaziri, Baada ya kupata alijaa kiburi na dharau.

Ashakumu sio matusi huyu ni mfuasi wa falsafa za Sukuma Gang.

Wakati akiwa Waziri na watu walipokuwa wanaokotwa kwenye bahari, maziwa na mito aliyokuwa anaisimamia hakuthubutu kunyanyua mdomo wake mbele ya Rais.
 
Ndio maana Kila siku nahubiri humu ndani. Kamwe usiwaamini Wana CCM! Huwa Kuna mambo nikiwaza naishia kucheka!

Mfano, walisema mikutano ya siasa ni kupoteza muda, haifai! Jana nimepita njiani huko nikaona mabango ya kumsifia Mwenyekiti wao kwa kuruhusu mikutano.

2. Waliitwa vibaraka wa Wazungu. Leo hii yamejaa mabango kuwa Mwenyekiti wao analeta maridhiano, naangalia nacheka TU. Hawa watu wanakuaga na akili timamu kweli?.
 
Hatuwezi kujidumaza kifikra kwa kudharau hoja za wengine kwasababu ya yale waliyofanya siku za nyuma, huko ni sawa na kuliangamiza taifa.

Kama unaamini Mpina hana sifa za kusema kile asemacho sasa kwasababu ya past, basi nioneshe yule aliye mtakatifu ili niwe namsikiliza yeye.
 
Umetumwa kutetea mafisadi. Jitambue.
Bunge lote ni vigeugeu

Huyo hafai hata kidogo, Watu wa aina yake walikuwa wanamsifia JPM ghafla Leo wanasema wanampongeza Mama Samia kaleta demokrasia na uhuru wa habari

Kwanini walishindwa kumwambia JPM wakati huo, Wote waliimba mapambio ya kusifu

Leo wamegeuka wanamsifia Samia huku wakijua maisha magumu
 
Na wewe piga kelele upate uwaziri
Acha hasira
 
Kwahiyo CHADEMA ndio inaaminika ambayo ilituambia Lowassa ni fisadi na Wana ushahidi wa ufisadi wake baadae wakabadili gia angani
 
Na wewe piga kelele upate uwaziri
Acha hasira
Mimi ni mwana ccm Siamini Katika watu wajinga wanaomsagia mwana ccm mwenzao kunguni ili wapate cheo

CCM ni mfumo na taasisi, Tatizo hawa akina Mpina, Makonda, Sabaya, Ally happi na mnyeti waliamini Katika kuligawa Taifa hili

Hawa watu walilazimisha kuwa ndugu zetu wa upinzani ni maadui wa Taifa hivyo tusishiriki hata Katika ndoa, misiba au harusi

Walisahau Taifa hili tumeshaoana na kuzaliana hakuna Chadema wala ccm, Hakuna simba wala Yanga, Tumeshazaliana

Chuki za akina Mpina must stop
 
Kwani anachongea mpina ni uongo?
 
  • Thanks
Reactions: wwg
Kwani anachongea mpina ni uongo?
Ni uwongo mtu hana ushahidi wowote anadandia hoja kama watu wanaodandia hoja hapa JF za CAG wala hawaelewi maana ya Auditing

Mfano Auditor akija ofisi akakuta kweli watu walienda safari nje ya nchi kikazi na barua zipo kabisa na zimesainiwa lakini kwa kiburi Chao hawakuleta Airticket hao waliosafiri Wataandika kuna Safari hewa za madollar kadhaa, Issue inakufa pale wahusika wakisisitizwa walete Airticket zao

Wananchi huku hawaelewi wanapiga kelele tu ohooo watu wanafanya safari hewa wanalipana madollar

Mpina aliambiwa thibitisha kauli zako bungeni alishindwa

Amejawa chuki na lengo lake ni kukigawa chama

Hawa akina Mpina ni masalia ndani ya ccm, Next time huyu atakuwa kama Prof Kabudi
 
Kama hiki ulichoandika ndivyo mambo yalivyo, basi huu ni uzembe wa makatibu wakuu wa wizara, sasa kwanini hao makatibu wakuu nao wageuzwe mahakimu kuhukumu walio chini yao?

Huu ujuaji wenu umepitwa na wakati, mnatetea uzembe hamtaki uwajibikaji.
 
Back
Top Bottom