Luhaga Mpina amlipua Waziri Makamba, amtuhumu kwa Uhujumu Uchumi. Atoa wito kwa TAKUKURU kumchukulia hatua

Luhaga Mpina amlipua Waziri Makamba, amtuhumu kwa Uhujumu Uchumi. Atoa wito kwa TAKUKURU kumchukulia hatua

Luhaga Mpina Mbunge wa Kisesa amesema Rais Samia alitaka mawaziri wamsaidie katika kujibu hoja za wananchi, hata hivyo jambo hilo halionekani sana kwa sasa, ambapo amesema mawaziri wapo kimya katika kujibu hoja za wananchi.

Mpina amesema wapo mawaziri hawajibu hoja za wananchi au huwa wanajibu kwa hoja nyepesi malalamiko ya raia, hali ambayo ameitaja kuwa sio kumsaidia Rais kama inavyotarajiwa.

Ametoa mfano wa waziri wa Nishati alivyojibu kuhusu ucheleweshwaji wa mradi wa bwawa la Mwl Nyerere ambapo Waziri wa Nishati alianza kulaumu kuwa Wabunge hawakutaka yeye awe waziri badala ya kujibu hoja iliyokuwa mezani.

Waziri ametolea mfano suala la kufuta tozo ya Tsh. 100 katika mafuta bila kufuata utaratibu. Ambapo amesema maamuzi ya waziri kufuta tozo hiyo amekutaja ni sawa na uhujumu wa mapato ya Serikali kwa kuwa fedha ya tozo hiyo ilikuwa katika bajeti ya Serikali ya mwaka 2021/22.

Kwa kushindwa kufuata taratibu za kuondoa tozo, Luhaga Mpina amesema Waziri wa Nishati amekuwa amefanya kosa la Uhujumu Uchumi. Na ameshindwa kutafuta kukielewa chanzo cha upandaji wa bei za mafuta nchini.

Kufuta tozo ya Tsh. 100 bila kufanya tathmini kumeipotezea Serikali Tsh. Bilioni 30. Hivyo, hakuwa na nia njema, achukuliwe hatua, atoa wito kwa TAKUKURU kumchukulia hatua. Amesema suala la kumchukulia hatua sio jambo la hiari, ni kwa mujibu wa sheria.

Mambo mengine aliyoyataja katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari ametaja kuwa Waziri Makamba ameshindwa kujibu kuhusu bei za mafuta na mfumuko wa bei.
Amejaa chuki tu dhidi ya Makamba!

Saivi Hakuna mgao na hali ya umeme umerudi kuwa kawaida! Kama kukatika umeme umeme haijaanza kukatika Leo wala jana!

Kuhusu bei ya Mafuta inabidi atuambie ni wapi duniani Mafuta hayajapanda bei!

Amejawa na chuki tu Huyu mpuuzi na mkabila! Wana hasira na Makamba wa watu Kwa kuendekeza upuuzi wao wa roho mbaya
 
Mpina atulie. Watu wa Kisesa wanazo shida nyingi zaidi. Makamba hawezi kufanya kazi y kuondoa tozo ya mafuta bila idhini ya baraza la mawaziri.
Wana chuki na Makamba wa watu kisa mjinga mwenzao kawaaminisha anahusika na kifo cha mungu wao!

Wamejaa ujinga tu ndo mana wanaua vikongwe kwao kwa kuwahisi tu kuwa ni wachawi
 
Makamba hawezi kufanywa chochote wala kuguswa.
Kama Baba yake alipewa jukwaa siku ile arushe madongo kwa JPM mnategmea nini?
Suala sio makamba kuguswa! Suala ni kumsakama mtu kwa chuki zako tu!

Makamba anahusikaje na kupanda kwa umeme? Kama sio ujinga ni nini hicho?
 
Makamba amefeli mapema sana
Hajafeli ila anafanyiwa hujuma na baadhi ya watendaji ambao kimsingi sio wazalendo, lengo lao ni kumuqngusha Waziri bila kujali gharama na adha wanazo zipata wananchi.
na hili ndio tatizo la kujaza watu wa aina moja ktk Idara za Serikali, matokeo yake ni hujuma za chini kwa chini.
tubadilike.
 
Back
Top Bottom