Luhaga mpina amvaa Bashe, Tuna changamoto ya mnunuzi mmoja katika zao la pamba, hii kesi haijaisha

Luhaga mpina amvaa Bashe, Tuna changamoto ya mnunuzi mmoja katika zao la pamba, hii kesi haijaisha

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina ameendelea kuikosoa vikali Wizara ya Kilimo kwa kuruhusu mfumo wa mnunuzi mmoja katika ununuzi wa zao la pamba, akidai kuwa mfumo huo unaua ushindani na kushusha bei ya mazao ya wakulima.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Mwandoya, Wilayani Meatu Mkoani Simiyu, Mpina amesema mfumo huo umesababisha bei ya pamba kushuka kutoka Sh. 1,700 hadi Sh. 1,150 kwa kilo, jambo ambalo linawaumiza wakulima wa pamba kote nchini.

“Wizara ya Kilimo hawana pamba, Bodi ya Pamba hawana pamba. Mkataba huu umefungwa na nani? Na kwa nini hauna hata bei iliyoandikwa? Tunafunga mkataba wa kuuza pamba, lazima ieleweke bei ni shilingi ngapi!” alihoji Mpina.

Ameongeza kuwa haoni mantiki ya kuwa na mnunuzi mmoja wa pamba huku mazao mengine kama mtama, mpunga na mifugo yakiuzwa kwa mfumo huru wa ushindani.

“Tunauliza, kwa nini mkataba huu uwe kwenye pamba tu? Kwanini turudi kule tulikotoka?” alisisitiza.

Mpina amesema ataendelea kuishauri na kuisimamia Wizara ya Kilimo ili ibadili mfumo huo usio na tija kwa mkulima.

 
Mpina kuna kitu anakijua na huenda Mama ana baraka zake katika hili sakata yaani yuko nyuma ya Bashe yeye kama yeye au watu wake.

Kwa kifupi, Bashe na Mama huenda wana masilahi katika hili.
 
Mpina Yuko sahihi,na wajibu hoja zake.

Mpina arudi Bungeni Kwa CCM hiyo hiyo.

CCM inatakiwa iwe na Wabunge Wachache machachali hakuna sababu ya kuwa na watu wote wa ndio Mzee.

Harafu ni dhana ya kijinga kudhani kila mwana CCM ambae hakubaliani na Baadhi ya hoja za serikali kwamba ni mpinzani.

Mwisho na wewe Mpina haiwezekani Sasa Kila kitu Cha Serikali unapinga,utakuwa na matatizo.Mrisho Gambo Huwa hapingi Kila kitu.

View: https://www.instagram.com/reel/DLPCwqwutq4/?igsh=MW5ydnRqZm9xbGdnZA==
 
Mpina kuna kitu anakijua na huenda Mama ana baraka zake katika hili sakata yaani yuko nyuma ya Bashe yeye kama yeye au watu wake.
Sio swala la kitu kukijua,mambo anayoongea Yako clear kina Bashe wanatakiwa kujibu hoja.Kwa nini mnunuzi mmja na ambae hakuna bei maalumu ya kununulia?.

Na Mama asimkate Mpina arudi Bungeni, haiwezekani tuwe na watu wote wa ndio Mzee.
 
Polepole alisema ccm ukijifanya umenyooka hutoboi, kweli hayo nayaona, ni ngumu kumwona mpina bunge lijalo.
 
Sasa Mpina utaendelea kufuatilia wapi wakati muda wako umeisha na jina lako tumeshalikata?
 
Back
Top Bottom